Unatamani kuwa mfanyakazi bora ??

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Kwa ufahamu huo vijana wengi hasa wa ulimwengu wa tatu wanasaka elimu kwa udi na uvumba ili waweze kumudu kufanya kazi maofisini. Wengi wao wanakimbilia madarasani kusomea sayansi, kilimo, biashara na hata sanaa, kwa hili hakuna ubishi kwani waalimu wa masomo hayo wako wengi mitaani.

Lakini pamoja na watu kutafuta elimu na kazi bado uchunguzi unaonyesha kuwa kuna wasomi wengi wanashindwa kumudu kufanya kazi pindi wanapoajiriwa kwenye makampuni au serikalini. Wengi wao wamejikuta wakiingia kwenye migogoro kiasi cha kuwafanya washindwe kutumia uwezo wao kuleta tija maeneo waliyoaminiwa kama wafanyakazi.

Ni ukweli ulio wazi kuwa kuna wafanyakazi wengi wanatumia muda mwingi kufitiniana ili kulinda nafasi zao zisichukuliwe na wengine. Wapo wanaokwenda kwa waganga kusafishwa nyota, wanaorogana, wanaonuniana, wanaoacha kazi kwa maelewano mabovu na wakuu wao wa kazi na wengine wamejikuta hawawezi uongozi licha ya kuwa na vyeti kibao kutoka katika vyuo vikuu vyenye sifa ulimwenguni.

Lakini wataalam wa jamii wanasema watu wengi wanashindwa kukabili changamoto za maisha ya kazini kwa sababu walipokuwa darasani walifundishwa masomo si namna ya kufanya kazi kwa tija tena mbele ya mchanganyiko wa watu wa kabila, rika, ufahamu na ujuzi tofauti.

Kwa kuzingatia hili nimeona ni vema leo nikaleta mada hii ya njia nane za kuwa mfanyakazi bora kazini ili kuwaelelimisha watu waachane na majungu, ushirikina na kutumia elimu kufikia kilele cha ubora cha ufanyakazi wenye kuwavutia waajiri na wafanyakzi wenzao.

EPUKA KUWA MTU WA TUZO
Mtu anayefanya kazi ndani ya jamii anatakiwa kuepuka sana kuhangaika kutafuta tuzo za ufanyakazi bora wa mwaka, kwani wataalam wanasema tuzo hizo zitamuweka kwenye kioo zaidi na kuwa mtu wa kutazamwa na kutegwa kila mara katika majukumu yake, ambapo kosa dogo linaweza kumfanya akosolewe kwa kulinganishwa na tuzo alizonyakuwa.

USIKWARUZANE NA WENZAKO
Unapokuwa kazini epuka kwa nguvu zako zote kuingia katika mikwaruzano na wafanyakzi wenzako na hasa bosi wako, liwe jambo la lazima kwako kutafuta suluhu kila linapokuja jambo la kukuondoa katika ushirikiano mwema na wenzako. Mikwaruzano itakufanya uwe na maadui wengi kazini ambao watakuwa tayari kukuacha uharibikiwe katika kazi zako.

WEKA REKODI YA MAFANIKIO
Unapokuwa kazini hakikisha kuwa ufanyaji kazi wako unakuwa ni wenye mafanikio. Hakikisha kuwa kila unapopewa kazi ifanye kwa moyo na uhakikishe kuwa inafanikiwa. Hii itakupa sifa kubwa kwa wafanyakazi wenzako na hata kwa wakuu wako wa kazi. Jenga mazingira ya kuonekana ni wa muhimu katika eneo fulani ili ikitokea nafasi moja ya kufanya au kusimamia kazi ya aina yako hata wenzako waone haki kukupa wewe kwa imani kuwa itakamilika kwa mafanikio.

ZINGATIA SUALA LA USAWA
Wewe kama ni mfanyakazi bila kujali cheo chako hakikisha kuwa kila mfanyakazi anapewa nafasi sawa katika mawazo na moyo wako. Usiwe mtu mwenye kuchagua watu kwa kuwapenda zaidi wenye uwezo na kuwadharau wasiokuwa na uwezo.

Ukifanya hivyo utajikuta ukichukiwa. Uwe mtu mwenye kugawa majukumu sawa na isiwe tu kwa wale ambao unaona wanakusaidia kimwili au kiroho.

ELEWA NINI KINAHITAJIKA
Watu wengi waliopo makazini hawafahamu mambo yanayohitajika sehemu zao za kazi. Ndiyo maana wanajikuta wakifanya kinyume cha mahitaji. Kuna wengine wanatumia ukali sana kwa watu wapole na wanakuwa wapole kwa watu wakorofi ukitofautisha hivyo utajikuta huwezi kupata tija na matokeo yake umuhimu wako kazini utapotea.

USIWE MPINGAJI SANA
Kuna watu ambao wako makazini lakini wanajulikana kwa upingaji. Kama jambo fulani litaletwa basi yeye lazima alipinge na kujifanya anahoja za nguvu. Hii ni kasoro pia. Unapokuwa kwenye jamii usiwe mtu wa kusema hapana kwa kila linalotoka kwa wenzako, wasikilize, waulize na mara nyingine hata kama unaona kuna upungufu basi ungana nao hata
kwa kusema tujaribu.

JITAMBUE NA UWATAMBUE WENZAKO
Jitambue mwenyewe jinsi ulivyo kitabia ili ujue udhaifu wako. Pamoja na hilo watambua wenzako. Hii itakurahisishia kujua jinsi ya kuchangamana nao bila kuhitilafiana. Fahamu kuwa wanadamu hawako sawa, usawa unapatikana pale mmoja kati yao atakapoamua kwa makusudi kuvumilia kasoro za mwenzake na kujivumilia pale anapohisi upande wa pili hamfanyii sawa na matakwa yake.

UWE NA MAONO
Maisha ya kazini yanahitaji sana wafanyakazi wenye maono, yanataka kila mtu atengeneze picha ya mafaniko, aone mwanga wa mbele na awe na sura ya kumuongoza kufikia huko. Mfanyakazi hatakiwi kukaa tu bila kufikiria nini kitatokea baada ya miaka sita kazini kwake.

Akiwa msomi wa kompyuta awaze kwa muda huo atamudu vipi nafasi yake au atakuwa amechuja na mwingine atahitajika kuziba nafasi yake. Tunashauriwa nusu ya maisha yetu tufikirie mafanikio na nusu tufikirie vitu vyenye maana. Huu ndiyo ‘uchawi’ utakaokufanya uwe mfanyakazi bora.
 
jamani tuongezee hapa naona ni hoja nzuri tu kwa wanaotaka kua wafanyakazi bora wa mwaka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom