Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 301
Marafiki mnachanganya sana elimu na uongozi! shauri lenu.
Ni sawa tusichanganye uongozi na elimu na si kweli kwamba kuwa elimu kubwa lazima utakuwa kiongozi mzuri, tutambue vile vile kuwa na elimu kubwa kama u-prof. haukuzuii wewe kuwa kiongozi mzuri.wakati nwingine napata shida sana na jinsi tunavyo dhani kuhusu kiongozi bora, hii habari ya fulani anafaa mara filani. urais si mchezo inataka utashi wa mtu mwenyewe binafsi wala si elimu tu au makongamano yake
Elimu katika uongozi inategemea na field ya elimu uliyonayo mfano si kila aliye na degree anaweza kuwa mwalimu. Prof. Sarungi na Prof. Baregu wote ni wanasiasa lakini tofauti iko kwenye fields zao Sarungi ni Medical doctor wa mifupa wakati Baregu ni Dr. wa Political Science, kwa hiyo unaweza kuona wazi ni yupi ambaye siasa inaweza isimpige chenga kwa mbali.
paulss amezungumzia utashi, mchukulie Dr. Shein na prof. Baregu, wote ni wanasiasa na niseme ni wasomi kwa elimu zao lakini wenye utashi tofauti. Unaweza kuona wazi kabisa ni yupi kati ya hao wawili aliye na utashi binafsi wa siasa na yule anayelazimisha siasa. Kwa hiyo naweza kusema kuwa Prof. Baregu ana vitu vyote mlivyovitaja yaani Elimu, field ya elimu yake na utashi, achilia mbali utashi wa yeye kutangaza nia hata historia yake shuleni/chuoni.