Unataka kucheka? Msikilize Lema alivyomtoa jasho wakili kesi ya Ubunge Arusha...

Angeanza hivi; "Moja, mbili, tatu...haya wote tuseme Peoples's ........powerrrrrrrr" hapa nina uhakika sauti mojawapo ingekuwa ni ya hakimu na huyo wakili pia
 
Huyo wakili aligombea singida mashariki kwa ticketi ya Magamba akapigwa chini kwenye kura za maoni za ndani ya CCM na hata kama angeshinda ni lazima angepigwa chini na Tundu Lissu ambaye ni Mdogo wake wa kuzaliwa yaani tumbo moja baba mmoja mama mmoja.... ambaye alikuwa anamsubiri kwa ham sana amgaragaze.

anataka kulipiza hasira zake za kushindwa kwa Lema yamemkuta aacche kabisa vijana ............
 
Labda sipo katika good mood ndo maana sijacheka ila nimegundua jamaa alikuwa anajitetea kijanja na kumchallenge wakili katika njia nyepesi!!!big up lemma!huyu mnyamwezi namkubali gwanda za chama zinavyomkaaga!!!
Usilete usharobaro hapa Lema ni mchaga wa Hai na sio Mnyamwezi!.......
 
Hahahaha. . .Poeples Power imenifanyia usiku wangu uwe mzuri. Hamna kesi tena hapo kwahiyo huyo wakili aangalie uwezekano wakuimaliza kabla hajaaibika zaidi.

He... huwa unaingia huku mwanakwetu?? Mh ama kweli peoples power inagusa wengi....
 
Jamani mie nimecheka hadi mbavu zinaniuma. Lema amenipa Raha sana kwa majibu yake. Hebu soma nawe uongeze siku za kuishi kwa kucheka na kupanua mapafu yako.......

Lema, wakili ‘wapigana vijembe' mahakamani

15 March 2012

Peter Saramba, Arusha | Mwananchi


VIJEMBE na malumbano kati ya shahidi wa kwanza wa upande wa utete, Godbless Lema na wakili, Alute Mughwai anayewawakilisha wadai katika kesi kupinga matokeo ya ubunge katika Jimbo la Arusha Mjini, ni miongoni mwa mambo yaliyotawala ukumbi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha jana.

Hali hiyo ilimlazimisha Jaji Gabriel Rwakibarila, kuingilia kati mara kwa mara na kutoa muongozo ili kuokoa muda wa mahakama.

Malumbano hayo yalisababishwa na aina ya maswali kutoka kwa wakili Mughwai na majibu ya Lema ambaye ni Mbunge wa Arusha Mjini na ambaye ni mdaiwa wa kwanza katika shauri hilo lililofunguliwa na wapiga kura watatu.

Walalamikaji hao ni, Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo wanaoimba mahakama, kutengua ushindi wa Lema kwa madai kuwa alitumia maneno ya kashfa na udhalilishaji dhidi ya aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Batilda Burian.

Baadhi ya hoja zilizozua malumbano kati ya wakili na shahidi huyo ni pamoja na hatua ya Mughwai kuhoji kama shahidi anajua mila na desturi za kabila la Waarusha (Wamaasai) na Wachagga zinazowabagua wanawake katika nafasi za uongozi wa kimila na zile za kupigiwa kura

"Mimi siyo kiongozi wa kimila, bali ni kiongozi wa kisiasa na kiserikali, hivyo sijui mila na desturi za uongozi wa kimila za jamii ya Waarusha, Wamaasai na Wachagga. Kwa nafasi yangu ya ubunge mimi ni kiongozi wa makabila yote yaliyoko katika Jimbo la Arusha Mjini wakiwemo Wanyaturu na wewe (wakili Mughwai),"

Akijibu swali kuhusu sababu za kutokuwapo kwa mwanamke aliyewahi kuchaguliwa kushika nafasi ya ubunge katika wilaya za jamii ya Waarusha, Lema alidai wengi wamejitokeza kugombea akiwamo mgombea wa Chadema aliyegombea katika Jimbo la Longido lakini hawakuchaguliwa.

Alisema wanawake hao hakuchaguliwa katika kura za jumla au kura za maoni ndani ya vyama kama ilivyotokea kwa wakili huyo aliyeshindwa kwenye katika kura za maoni ndani ya CCM katika Jimbo la Singida Mashariki.

"Baadhi walishindwa kwenye kura za maoni kama wewe ulivyoshindwa kule Singida Mashariki. Wengine walishinda kura za maoni lakini hawakuchaguliwa na wananchi kwenye uchaguzi mkuu kama ilivyokuwa kwa Dk Burian hapa Arusha," alidai Leman na kufanya wasikilizaji kuangua kicheko.

Shahidi huyo aliendelea kumrushia maneno wakili Mughwai baada ya kudai kuwa amedanganywa na wateja wake kwa kumweleza kuwa aliomba Dk Burian asichaguliwe kwa sababu siyo mkazi wa Arusha.

Alidai kuwa kisheria, Mtanzania yeyote ana haki ya kugombea ubunge katika jimbo lolote bila kujali ukazi wala asili yake ya kuzaliwa.

"Kwamba nilisema Dk Burian asichaguliwe kwa sababu ni mkazi wa Zanzibar ni hoja ya uwongo na mufilisi, wateja wako wamekudanganya sana kuhusu hilo kwa sababu hoja hiyo isingefanya asichaguliwe ndiyo maana mimi ni mchaga wa Hai, Kilimanjaro lakini nimegombea Arusha na kushinda na leo ni mbunge wako," alidai Lema.

Kauli ya kudanganywa na wateja wake, ilionekana kumkera wakili Mughwai na kuamua kumuonya kwa mara nyingine sahidi huyo kuacha tabia ya kumpiga misumari kwa kumrushia maneno, badala yake ajibu maswali anayomuuliza.

"Kwa mara nyingine nakuonya usinipige misumari kwa kunirushia maneno. Wewe jibu maswali yangu," alisema wakili Mughwai.

Wakili Mughwai anayesaidiana na Modest Akida kuwakilisha wadai katika shauri hilo, aliingia kwenye malumbano mengine na Lema alipomzuia kumalizia kukariri maneno yake kuhusu mikopo kwa wanawake, aliyoyatamka katika mikutano yake ya kampeni kitendo kilichomfanya shahidi kukataa kujibu swali lake hadi atakapomaliza kukariri maneno yote.

Kitendo hicho kilichomfanya Jaji Rwakibarila kuingilia kati na kumruhusu amalizie.

Lakini alipoanza kukariri maneno hayo, kuhusu taratibu ngumu za mikopo kwa wanawake, wakili Mughwai aliingilia kati na kumtaka ajirejeshe nyuma na kuzungumza kama vile anahutubia mkutano wa hadhara mwaka 2010, kitendo kilichomfanya mbunge huyo kuanza kwa kauli mbiu na salama ya Chadema ya ‘Peoples' huku wasikilizaji wakiitikia power….

"Hapana, hapana, hiyo ya peoples' power acha kwa sababu muda hautoshi, rudia tu maneno yako kuhusu mikopo kwa akina mama kwa kukariri maneno halisi uliyoyatamka kwenye mikutano yako ya kampeni kuhusu hoja hiyo," alisema wakili Mughwai akimkatisha Lema.

Awali hoja kuhusu utata juu ya elimu ya mbunge huyo iliibuka baada ya wakili Mughwai kuhoji taarifa zake za elimu zilizopo katika kumbukumbu za nyaraka za bunge, hoja iliyojibiwa na shahidi huyo kuwa imetokana na makosa ya uchapaji uliosababishwa na Bunge lenyewe akidai tayari aliiandikia ofisi ya Bunge kuelezea hilo na kutaka marekebisho.
Kawaida ya punguani ni kuchekesha watu walio serious. Umesikia elimu ya LEMA ilivyozua utata hapo mahakani au hilo unalimezea? Jamaa elimu yake ya chuo kikuuu kasomea chini ya mti na Mvua ilipoanza kunyesha akatimua kabla ya ku-graduate, teh teh teh.
 
Huyu Mughwai alifikiri atapanda umaarufu kirahisi kwa kumwangusha Lema kumbe baada ya kesi hii atakuwa amepata aibu kubwa ya kutemewa mate barabarani na kujimaliza kabisa kisiasa na kiprofessional. Baada ya hii kesi itabidi ahamie Zanzibar kama Masumbuko Lamwai kwa sababu hapa Arusha hatapata tena mteja labda hao magamba wenzake.
 
Sasa ni dhahiri kwamba Lema ni kiboko yao wana ccm wote na washabiki wao. Manake kila wakijaribu kumkabili anawamaliza papo hapo bila kuchelewa.

Iwe ni Spika wa bunge, waziri mkuu, wakili, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, ocd, rpc, meya ama mkurugenzi ikiwa tu unataka kumkabili Lema na akili ya kiccm lazima atakuaibisha, na bado hadi hii kesi inakwisha yataibuka mengi sana, just stay tuned!!
 
Ngoja tuone mpaka mwisho wa kesi itakuwaje. Lakini nahofia kwa mtindo huu inaweza kufika 2015 kesi haijaisha.
 
Kawaida ya punguani ni kuchekesha watu walio serious. Umesikia elimu ya LEMA ilivyozua utata hapo mahakani au hilo unalimezea? Jamaa elimu yake ya chuo kikuuu kasomea chini ya mti na Mvua ilipoanza kunyesha akatimua kabla ya ku-graduate, teh teh teh.

Jee. . . Hilo la elimu nalo ni mojawapo kati ya madai ya msingi katika kesi yenu wana magamba?? na kama unadhani hivyo ni vichekesho subiri siku ya hukumu ndio utajua alikuwa anachekesha au vipi....poleni mmeanza kuweweseka kwa majibu ilihali hukumu bado??
 
hahahaaa! Wakili kapata aliyemzidi ujanja. Mawakili aina hii huwa wanatunyanyasa sana kwa maswali hasa anapomtetea mteja (jambazi) wake.

tamaa ya pesa na kutafuta maujiko matokeo yake ndio hayo....matokeo yake unatoka na masiziya jikoni badala ya ujiko
 
Kilichokuchekesha nn sasa?

Well, napenda Lema/cdm washinde kesi hii pale Arusha,,lkn kwa hapa hakuna cha kuchekesha bana!


mkuu uliwahi kusikia hata hii kauli inayosema "Kigumu chama cha magamba inapigwa mahakamani na watu wakaitika kigumuu????/
 
Hivi kweli huyu wakili wa ccm kasoma kweli?nina wasiwasi na vyeti vyake,Lema songa mbele,Peoplessssssssssssssss
 
Teh teh teh teh teh teh teh teh teh teh aaaaaaaaaaaaaaa! Jamani mbavu sangu, eeee Yesu rua mangi.
 
Back
Top Bottom