Unatafuta Mchumba? Ushauri wa Bure wa Michelle Obama

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
3561018.jpg

Mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama Tuesday, November 17, 2009 10:32 AM
Mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama, ameamua kumwaga busara zake kwa kuwashauri wanawake ambao hawajaolewa na wanatafuta wachumba kuwa wasitafute mwanaume kwa kuangalia ana cheo gani au kwa kuangalia akaunti yake ya benki imejaa pesa kiasi gani. Akiongea na jarida la Glamour la Marekani, Michelle Obama alitoa ushauri bora kwa wanawake ambao hajaolewa jinsi ya kumtafuta Mr.Right.

Katika ushauri wake Michelle Obama alisema kwamba ni vizuri kwa mwanamke anayetafuta mwanaume wa kumuoa kutumia muda mwingi kumfahamu vizuri mwanaume atakayemtongoza badala ya kuangalia zaidi pesa zake na cheo chake.

Akiongea na jarida hilo Michelle Obama alitoa siri zake kwa wanawake zilizomfanya aweze kumnasa Barack Obama, rais wa kwanza mweusi wa Marekani.

"Kama unatafuta mapenzi ya kweli, usijali sana akaunti yake ya benki, cheo chake au umaarufu wake" alisema Michelle Obama na kuongeza "Usijali sana mali alizo nazo angalia moyo wake na utu wake".

"Njia rahisi ya kujua kuwa umempata mwanaume sahihi ni kwa kuangalia jinsi anavyomjali mama yake na anavyowazungumzia wanawake wengine na jinsi anavyoonyesha hisia zake kwa watoto ambao hawafahamu na muhimu kuliko vyote ni jinsi gani anaonyesha kukujali".

"Na unapokuwa kwenye hatua za mwanzo za uhusiano na mwanaume, lazima uwe mwenye furaha. Usiendelee kukaa kwenye uhusiano na mwanaume ambaye hakufanyi uwe mwenye furaha badala yake anakufanya uwe mwenye huzuni wakati wote".

"Kama utakuwa kwenye uhusiano na mwanaume kama huyo, usikubali kuolewa naye kwani hautokuwa na furaha kwenye ndoa", alimalizia Michelle Obama.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3561018&&Cat=7
 
Hizo sifa za mwanaume bora zote ninazo kama kuna mtu yupo single na anahitaji kuwa na bwana ani Pm tafadhali..
 
SIO UWONGO, mi mwenyewe ninazo,
ila wanawake nikiwafuata wananiambia sina mvuto,
ushamba wangu wa malezi ya kijima nipeleke kijijini kwetu,
KAZI KWELIKWELI

Duh pole sna kwa nini usitafute anae endana na malezi yako my kaka!! ila utapewa mwema na Mungu achana na hao!!!
 
"Njia rahisi ya kujua kuwa umempata mwanaume sahihi ni kwa kuangalia jinsi anavyomjali mama yake na anavyowazungumzia wanawake wengine na jinsi anavyoonyesha hisia zake kwa watoto ambao hawafahamu na muhimu kuliko vyote ni jinsi gani anaonyesha kukujali".

"Na unapokuwa kwenye hatua za mwanzo za uhusiano na mwanaume, lazima uwe mwenye furaha. Usiendelee kukaa kwenye uhusiano na mwanaume ambaye hakufanyi uwe mwenye furaha badala yake anakufanya uwe mwenye huzuni wakati wote".

"Kama utakuwa kwenye uhusiano na mwanaume kama huyo, usikubali kuolewa naye kwani hautokuwa na furaha kwenye ndoa", alimalizia Michelle Obama.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3561018&&Cat=7

Good advice, lakini je inatekelezeka? nakumbuka kuskia kwamba hata yeye amepitia makashkash makubwa na hata huko mwanzo sigara ilimnyima raha, sasa ina maana hakukosa furaha??

I believe in marriage zilizoandaliwa na mungu kwahiyo kila moja ina majaribu yake, mengine yooote ni majaaliwa yake muumba na si binadamu

Ndoa haina dummy run!!!
 
Back
Top Bottom