Unapotaka kununua programu

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Katika manunuzi ya haswa ya program ( software ) kuna njia kuu 2 za ununuzi moja ni kwa njia ya mtandao ambayo unaweza kudownload hapo hapo program hiyo pamoja na leseni yake nyingine ni kwa njia ya mtandao lakini unaletewa kwa njia nyingine ya usafirishaji katika mfumo wa cd nyingine ni ile ya moja kwa moja kwenda dukani au kwenda kwa wakati wa uuzaji programu hizo na ukanunua ukapewa programu hiyo .
Unaponunua program hizi inabidi ujue utaitumiaje utakapoipata au kama wewe ni msimamizi wa mtandao fulani katika kampuni fulani ujue leseni ya program hiyo ni ya watu wangapi , kujua kama leseni ni ya watumiaji wangapi au la inaelezwa katika tovuti ya program husika pale unapotaka kununua .
Sasa inapotokea kwamba leseni ya program hiyo ni ya mtu mmoja ( single user ) wewe ukaitumia kwa zaidi ya mtu mmoja hili ni kosa hata kama programu hiyo umeinunua kwa bei halali au kwa njia halali lakini katika matumizi ndio umefanya makosa makubwa , makosa hayo yanaweza kutambulika pale tu mmoja wa watumiaji anapotakiwa kupdate kitu fulani katika program hiyo na kutakiwa kudhibitisha umiliki wa program hiyo .
Suala lingine ni kuhakiki pale unaponunua program hiyo kama duka , mtu huyo au kampuni hiyo imeidhinishwa kuuza program hiyo au kutoa msaada kwa bidhaa zinazohusu program hiyo ,jijini dare s salaam kuna maduka mengi na watu wengi wanaojiita ni certified professionals wa bidhaa Fulani lakini ukweli sio ukitembelea katika tovuti ya program husika hawatambuliki
Kama mtu hatambuliki na mtengenezaji bidhaa ina maanisha huna ruhusa ya kutoa support kwa baadhi ya mambo bila kuwa na vibali ,kuna kampuni inaitwa AccessData kampuni hii inatengeneza program za kurecover data zilizopotea katika computer pamoja upelelezi unaohusiana masuala ya mitandao na mawasiliano
Unapotaka kutumia bidhaa za kampuni hiyo kwanza lazima uwe mwanachama wakati unapokuwa mwanachama unafanya mitihani Fulani hivi unakuwa na leseni ya kipindi cha miaka 3 kwahiyo kila miaka3 unatakiwa kufanya mitihani hiyo unapofaulu unapatiwa leseni mpya ya kuendelea na shuguli maana yake unaweza kufanya kazi zinazohusiana na bidhaa za kampuni hiyo popote duniani kutokana na leseni yako inavyosema .
Kwahiyo kampuni mbali mbali kubwa na bodi mbali mbali zina mitihani yake ya kuweza kutambua wataalamu wa bidhaa zao popote walipo duniani ,sasa wewe unayetaka huduma unatakiwa utembelee tovuti mfano ya Toshiba global – utaenda east afrika - tanzania ( ukifika Tanzania utaona watu wanaotambulika na Toshiba kama watoa support kwa bidhaa za Toshiba )
Cha mwisho ni kwa wewe mtumiaji kujua specifications za komputa yako kama zinaendana na specifications za hiyo programu , mfano unaponunua autocad 2009 unatakiwa uwe na ram ya angalau mb 512 na kuendelea unapokuwa na chini ya hapo computer yako inaweza kuwa slow katika utendaji wako wa kazi baadaye ulalamike programu haifai ina matatizo kumbe ni wewe mtumiaji ulikosea
Pia kila mara unatakiwa ufanye update katika programu hizo ndio maana suala la memory ni muhimu sana kuangalia kabla ya kufanya maamuzi ya kununua programu mmpya
 
Back
Top Bottom