Unapotafuta Mchumba Online....

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Kama ni kwenye Facebook, Myspace, Bebo au Hi5, unapotafuta mchumba au mpenzi kwenye internet basi kitu cha kwanza kabisa omba picha ili usije ukakumbana na kitu usichokitegemea.
Katika miaka hii ya teke linalokujia, mambo ya kutafuta mwenza kwenye internet si jambo geni, kumekuwa na tovuti nyingi za kulipia za kutafuta wachumba au wapenzi.

Kwa wale wasiopenda kutumia pesa zao kwenye tovuti hizo wengine baadhi wamekuwa wakiitumia mitandao kama Facebook, MySpace, au Hi5.

Si ajabu kusikia kwamba takwimu zinazoonyesha kuwa mtandao wa Facebook unaongoza kwa kusababisha kuvunjika kwa ndoa za watu, yote kutokana na vishawishi vinavyotokana na mitandao hiyo ambayo lengo kubwa lilikuwa ni kuziunganisha jamii katika masuala mbali mbali ya kila siku.

Kwa wale watakaoamua kutafuta wenza online basi kitu cha kwanza cha kuzingatia ni picha ya mhusika ili umuone mtu utakayekutana naye au la unaweza kukutana na mtu mwenye sifa au maumbile ambayo hukuyategemea.

Angalia picha hizi ambazo zimekuwa zikitamba linapozungumziwa suala la kutafuta mpenzi online.

gonga hapa

NIFAHAMISHE .: PHOTO GALLERY :.
 
Hata picha si anaweza kukuwekea ya jilani yake badala yakuweka yakwake?!
 
Mapenzi ya kukutana online mengi ni uzushi na wizi mtupu. Hata lengo la mtandao kukutanisha wa2 limepoteza muelekeo sasa mtandao unatumiwa kama kijiwe cha kutafutia mabwana. Wizi mtupu
 
Back
Top Bottom