Unapopanda Daladala liendeshwalo na mtoto!!

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
Naam,,, Msafiri kafiri ama? Niko ndani ya daladala naelekea katika shuhuli zangu za miangaiko. Nigeuzapo macho kumtizama dereva wa daladala hili nistuka kidogo,,,, ni mtoto! Mtoto kabsaaaa,,, kama ana hata miaka 18 ni Mungu anajua. Nikafikiri labda ni mtoto wa mwenyegari anampelekea dereva gari asubuhi hii. Nalazimika kumuuliza "kijana wewe ndo dereva wa hii gari?" anajibu ndio 'blaza, kwani vipi?' sikuwa na la kujibu. Nikaanza kusali kimya kimya maana gari ilishajaa sasa na tunaanza kuona MAKEKE YA DREVA,, mara aovateki,,, mara apite pembeni ya barabara (wenyewe wanaita kutanua). Kali ni pale aliposimamishwa na askari wa usalama barabarani!!! Nilishangaa ndo kwanza akabadili gea na kuongeza mwendo halafu akampa ishara askari kuwa atarudi, askari naye akampa ishara ya dole gumba. Naam,,,, wameshaelewana,,,,sikuwa na imani tena. Niliomba kushuka kituo kilichofuta.

Jioni ya siku hiyohiyo nikabahatika kukutana na kipindi kwenye TV fulani hivi. Mheshimiwa afande Kombe alikuwa akizungumzia pamoja na mambo mengine, UTARATIBU NA SHERIA ZA KUPATA LESENI YA KUENDESHA MAGARI YA ABIRIA. Nilichosikia ni kuwa ili dereva aruhusiwe kuendesha magari ya abiria ni lazima awe na umri usiopungua miaka 30 ndo apate leseni daraja C. Sasa najiuliza hawa watoto wanapata wapi leseni hizi? Kwa nini mamlaka husika zinaruhusu watoto hawa kuchezea roho za watu? Askari wa usalama barabarani wanaliona hili ama hawaoni? Tutakuwa tunasema uongo kama tukidhani kuwa AJALI HIZI MBAYA zinazotuangamiza kila siku kuwa zinasababishwa na ASKARI WA USALAMA BARABARANI?
Ningeshauri mamlaka husika kufuatilia na kuwanyanganya leseni daraja la C kwa watoto wote walio chini ya miaka inayotakiwa kisheria.
TUONEANE HURUMA KIDOGO.
 
Eeka Mangi inaelekea wewe mwenyewe unaendekeza huo uvunjaji sheria. Unaweza kueleza ni kwanini ulibakia kusali tuuuu badala ya kuripoti kisa hicho kwa mamlaka husika? Ungewafahamisha hata Emergency Police au Mamlaka inayoshughulika na usafiri wa nchi kavu na majini. Hukutenda wajibu wako. Je namba za hiyo gari unazo? Usilete uozo wako katika JF- eleza hatua ulizochukua. Mungu hawezi kukusaidia wakati wewe hujaonyesha nia yeyote.
 
^^ Inatia shaka kuchukua hatua za haraka haraka na hasa baada ya kuona hata hao wanaosimamia usalama barabarani hawakuweza kumsimamisha shoferi huyo...
 
Nadhani hata kitendo cha kupost hapa ni Hatua Mojawapo! Wengi pengine wangekaa kimya tu.

Ukitizama mambo yanavyokwenda Tz inasikitisha sana. Corruption is everywhere! Tunahitaji mabadiliko lakini sijui tuanzie wapi!
 
Eeka Mangi inaelekea wewe mwenyewe unaendekeza huo uvunjaji sheria. Unaweza kueleza ni kwanini ulibakia kusali tuuuu badala ya kuripoti kisa hicho kwa mamlaka husika? Ungewafahamisha hata Emergency Police au Mamlaka inayoshughulika na usafiri wa nchi kavu na majini. Hukutenda wajibu wako. Je namba za hiyo gari unazo? Usilete uozo wako katika JF- eleza hatua ulizochukua. Mungu hawezi kukusaidia wakati wewe hujaonyesha nia yeyote.

Ni wangapi wewe umewahi kuwaona hawana stahiki ya kuwa na leseni daraja hilo ukawaripoti polisi wakachukuliwa hatua? Wajibu wangu niliona ni kuweka hapa jamvini ili tuone kwa pamoja tutafanya nini. Kutumia kalamu hii ni wajibu wangu. Kama askari anaonyeshwa ishara ya mzunguko na anakubalina kumbiwa hana akili, je mimi ningeripoti ingekuwaje?
Kwa taarifa nilizozipata hapa kila traffic anazo gari zake anazopokea hela jioni siku hiyo na kama dereva hakupeleka anahesabiwa jana na leo. Upo!
 
Back
Top Bottom