Unapochoma msitu kutafuta panya kwetu

bantulile

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,574
602
Kule kwetu kuna msimu wenyeji hutafuta kitoweo cha panya. Utafutaji wa kitoweo hiki huhusisha kuchoma msitu ili kuwafukuza panya na baadye kuwakamata wanapokimbia kutauta kujiokoa na moto uliochomwa kwenye msitu ambao ndiyo mazingira yao.
Kutafuta kitoeo si hoja, lakini kuchoma msitu ndiyo hoja. Ukilinganisha kipato cha panya na kipato kitokancho na msitu, msitu una faida zaidi kuliko panya wanaopatikana kutokana na kuchoma msitu.
Kusimamisha ajira, kupandisha vyeo watumishi na uhamisho kwa watumishi kwa minajiri ya kuwatafuta watumishi hewa hakuna tofauti na muwindaji wa panya anavyoharibu msitu kutafuta panya kitoweo cha siku moja.
Kuwaadhibu watumishi tena wenye utumishi wa kutukuka kwa kutafuta watumishi hewa nashindwa kuelezea kwa lugha ambayo sitakwepe lungu la makosa ya mtandaoni lakini wenye akili wataelewa neno linalofaa kwa uamuzi wa namna hii.
Kupandishwa cheo ni haki na stahili ya mtumishi. Uhamisho wa kutoka sehemu kwenda sehemu nyingine ya kazi ni haki pia ya mtumishi na huambatana na sababu zinazokubalika kiutumishi na kifamilia, lakini muhimu zaidi vitendo vyote viwili vinaongeza moyo wa kazi na kuboresha utendaji.
Serikali inapoangalia kitu kimoja tu na kuacha kuona mambo mengine muhimu ni hatari. Mtumishi anayetegemea kupandishwa cheo si mtumishi hewa na wala hajatenda kosa lolote, haingii akilini ni kwa vipi anapewa adhabu kwa kosa ambalo hakulitenda yeye katika utumishi wake? Ni vipi mtumishi anayestaafu kwa mujibu wa sheria anayestahiri kupandishwa cheo sasa amesimamishwa kupandishwa cheo ili kupisha zoezi la kuwasaka watumishi hewa ataipata haki yake hiyo. Serikali makini haiwezi kutafuta haki yake huku ikipora haki za wengine. Serikali haipo wa ajiiri yake yenyewe ipo pia kwa ajili ya watumishi wakiwemo wanaozuiwa kupandishwa vyeo na kuhama. Hawa nao pia ni watanzania lolote linalofanywa kwa ajiri ya kuboresha maisha ya watanzania haipaswi kuwaumiza.. Kuamua mambo yanayohusu maslahi ya watu bila ridhaa yao hakuna tofauti na ubeberu, maana beberu hupand jike hadi hata bila ridhaa yake.
Ama kweli ' Kchwa cha kuku hakistahiri kilemba'
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom