Unapoanza Kazi - Bana Matumizi bana Matumizi

ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,161
1,460
Based on True story - From Dar to Kigoma Ujiji.

Kuna vijana wawili walipata post kuanza kazi ya uhasibu katika ofisi ya Mkuu wa mkoa - Kigoma, hiyo ilikuwa post yao ya kwanza kabisa baada ya kuhitimu masomo yao ya juu hapo mlimani.

Maisha lazima yaanze hata kama ni pembezoni mwa nchi, vijana wakafika na kutafuta chumba na sebure wakishare kubana matumizi. Kilichofuata ni kuweka bajeti safi ili wapate savings at the end of each month.

Ile nyumba walipanga kulikuwa na wapangaji wengine na majirani pia, vijana hawa walizoelewa ghafla kwa usheshi wao hasa wakitoka kazini mida ya saa 11 na nusu jioni.

"Kawapokeeni kaka zenu wamerudi hao" alisikika mama mmoja kila siku akiwaambia wanae watatu mara tu ifikapo jioni. Watoto hawa watatu miaka 8, 6, 4 walipenda kukaa na vijana hawa hadi wahakikishe wamekula ndipo wanarudi kwa mama yao, na hii ikawa routine.

Vijana wakapiga skuti wakaona bajeti yao inayumba yumba, wakasema tutumie mbinu kali tuweke pilipili kwanye msosi tuwadhibiti hawa madogo - ikafika next day mzee pilipili kichaa kibao kwenye kikuku robo walichonunua kulumangia ugali - madogo kama kawa haoo - - shikamooni kaka James na Chris - vilisikika vikiamkia huku vikicheki menu pale kwenye mkeka sebureni ( hawajanunua meza bado)

Pilipili ikuwa imekolea si masihala, washikaji wakajifanya wapo busy kidogo ili kucheki game inakuwaje - duh madogo wakapiga tonge moja moja --- mmmhh wote wakaangaliana kwanza, baada ya sekunde kama kumi hivi yule mdogo (4) akasmile kidogo na kuwaambia wenzake kwa kuwanongoneza --- "Eti wameweka pilipili leo --- aaaa lakini hizi si kali kama zile za babu " - wale kaka zake hawakumjali wakaendelea kupiga menu as if hakuna chochote kile.

wale vijana wakaangaliana na kusemezana mioyoni mwao - Ama kweli ndiyo maana hapa Kigoma pakaitwa mwisho wa Reli.
 
NDIO MZEEEE..........HUKO NI MWISHO WA MATATIZO.......:smile::smile:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom