Unapenda nini Hapa duniani ?

Lakini mkuu, kusudio la Mungu hapo mwanzo lilikuwa kuwa binadamu wote tuwe sawa ktk angle zote, so unaposema inge-bore, unamaanisha nini?
Halikua kusudio la Mungu kutufanya tufanane, lingekua basi wote tungefanana mpaka unyayo. Alichotupa ni uwezo wa kujiwezesha kuwa sawa kifikra, kiutendaji n.k
Huwezi kuwa mvivu/hujitumi alafu hapo hapo ukataka kulingana na mtu anaejishughulisha day in, day out.
 
napenda ningekuwa na akili nyingi kama za wana sayansi za fizikia na hesabu niweze kugundua mavitu muhimu.
ili muda wangu mwingi niutumie kugundua vitu.
lakini naona nimepishana na huo ubongo wa akili nyingi.
 
Mimi napenda 1.kula 2.kulewa kidogo 3. Kuwa na marafiki wabishi. 4.mazoezi 5.mapenzi 6.kulala sana 7.ubishi 8.matani 9.kuvaa vizuri 10. Kuoga kwa siku mara tatu kama dosi .je wewe unapenda nini ?

mimi hapo 1, 5 na 6.

Mimi napenda 1.kula 2.kulewa kidogo 3. Kuwa na marafiki wabishi. 4.mazoezi 5.mapenzi 6.kulala sana 7.ubishi 8.matani 9.kuvaa vizuri 10. Kuoga kwa siku mara tatu kama dosi .je wewe unapenda nini ?

Napenda maisha yenye amani yaliyojaa furaha na upendo mwingi. Ideally ningependa kila mtu ampenda mwenzake kama anavyojipenda yeye mwenye ili dunia iwe ni sehemu inayoheshimika na kukalika. Siyo kama sasa, kila mtu amejawa na frustration za maisha, kudanganyana, ufisadi, dhuluma, chuki, infedelity, choyo ubinfsi nk. Haya ni machukizo na kero kuu mno machoni pangu!
 
Mimi napenda 1.kula 2.kulewa kidogo 3. Kuwa na marafiki wabishi. 4.mazoezi 5.mapenzi 6.kulala sana 7.ubishi 8.matani 9.kuvaa vizuri 10. Kuoga kwa siku mara tatu kama dosi .je wewe unapenda nini ?

mimi kama askari, napenda kwa saana! Pombe, Mbuguma/wanawake, na Vita. Sina kumb2 nyingine.
 
Napenda kusoma kitabu cha "Basic Information Before Leaving Earth".
 
mimi kama askari, napenda kwa saana! Pombe, Mbuguma/wanawake, na Vita. Sina kumb2 nyingine.
mkuu mbuguma kwa huku kwetu ni ng'ombe jike ambaye hajazaa, sijui wewe umemaanisha nini iyo mbuguma. pia sijui wewe ni askari yupi, mwanajeshi au polisi? kama ni polisi basi umesahau kuwa unapenda sana rushwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom