UNAMTUMIA HELA ALAFU ''mbona nikidogo hivyo?'' ni sawa?

MARCKO

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
2,258
274
Jf naomba maoni kidogo. Eti demu wako anakuomba hela na hali yako iko vibaya ; lakini unajipigapiga unamtumia ka elfu 20. Eti ana sema mbona kidogo hivyo? Hata bila kushukuru. Is it fair?
 
ukiona hivyo ujue kuna jamaa linatoa zaidi yako! hatua ya uchumba au galfriend na Boyfriend siku hizi ni PASUA kichwa mno, always kuna kuna na udanganyifu mkubwa sana na kutoridhika, so mkuu kaza moyo!
 
Haya mapenzi ya kuombana hela enzi zetu hayakuwepo. Ina maana mkiachana inabidi arukie tawi lingine, sio? Manake kila wakati anahitaji supplier? Kha!
 
Kweli ubinadamu kazi.

Huyo jua tu hana shukrani, na mtu asiye na shukrani ni mtu asiyejua kuridhika. Unaweza ukamfanyia hata mambo makubwa na bado usisikie asante yake, ukaishia kuambulia malalamiko. Kama unaweza ongea nae, mweleze kwamba hulazimiki kumfanyia chochote (wewe sio baba yake) hivyo kama unayomfanyia hayamtoshi atafute anaeweza zaidi. Asikubabaishe!!
 
Huyo kakufanya ATM machine yake! Anataka tu akitaka hela kidogo,achomoe kama elfu 50 hv.Pole sana,huyo sio mwanamke wa kuishi nae,atakuaibisha huyo siku ukiishiwa ndani ya nyumba.Pia umchunguze sana,pengine kuna anamlea tofauti na wewe,na pengine anapata donge nono zaidi kuliko unalompa. LAKINI NAJIULIZA,KWA NINI WANAWAKE WANAKUWA HIVYO? Ndo maana wengi wanaishia kumegwa na mwishowe wanaachwa.
 
Swadakta. Hili ndiyo jibu . mama nimekukubali.
 
Huyo hakufai moyo wake unapenda pesa zaidi ila nawewe kama humwelezi ukwel kuhusu hali yako kiuchumi "utakula vumbi" maana vijana wengi tunajifanya wajanja tusionekane hatuna kwa mabinti. Na kama anaelewa ila havumilii wala kuridhika kwakidogo umpatiacho achana nae maana hata kama utamuoa ndo atakua anakuhesabia akisema "...kwani wewe unatumia pesa ngapi nje?,...siku ile ulinunua viatu nikanyamaza, juzi umenunua suruali nikakuangalia tu,...na jana nilikukuta umenunua soda unakunywa na rafiki zako...." habari kama hizi zitakufanya upasuke kichwa. TRAIN YOU WIFE, IT IS NOT GOOD TO LIVE ALONE BUT DON'T LOOK FOR AN ANGEL.
 
Inategemea wewe ulianza naye vipi,,
kama ulijitapa kwake kwamba wewe ni mtoto wa Jei Kei obviously ukimtumia 20K lazima atahoji..
Tafakari, chukua hatua.
 
Huyo kakufanya ATM machine yake! Anataka tu akitaka hela kidogo,achomoe kama elfu 50 hv.Pole sana,huyo sio mwanamke wa kuishi nae,atakuaibisha huyo siku ukiishiwa ndani ya nyumba.Pia umchunguze sana,pengine kuna anamlea tofauti na wewe,na pengine anapata donge nono zaidi kuliko unalompa. LAKINI NAJIULIZA,KWA NINI WANAWAKE WANAKUWA HIVYO? Ndo maana wengi wanaishia kumegwa na mwishowe wanaachwa.

point of corctn;
SI WANAWAKE WOTE WAPO IVYO...
na ndo maana kuna wanawake wengine wanatunza maboy frend/wachumba/waume zao.
 
Unajua ili kuepuka mambo kama hayo siku nyingine unatakiwa umwambe hela unayotaka kumtumia kabla. Reaction yake haiwezi kuwa mbaya maana hiyo mtakuwa mshakubaliana kabla. Sasa wewe amekwambia ana shida ya M unasema hiyo sina ila ntakutumia kidogo alafu unatuma 20.
 
kama kidogo,mbona na yeye anaomba?mwambie na yeye akugaie.asie na shukurani.huyo atakupelekesha.ajipange atafute mwenyewe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom