unamkumbuka Mwl yupi shuleni/chuoni kwako ayekuwa na tabia ya 'ajabu'??

Mimi kwa upande wangu simzungumzii Mwalimu wangu, but kuna Afande mmoja alikuwa Makongo Sekondari, sijui kama alikuwa ni Mwalimu kabisa au vipi, ni marehemu now, Afande Miraji, nilikuwa napewa stori zake za vituko, alikuwa ni noma, yaani wanakuambia akikupa adhabu, hutomsahau, akiwa anakutafuta, akikukamata utakiona cha moto, anaweza kukutia aibu mbele hata ya demu wako, wanaJf waliosoma Makongo, hapana shaka watakuwa wanamjua, cause alikuwa ni maarufu sana sana Makongo, alikuwa ana vituko vingi sana, alishawahi kuwalazimiza wanafunzi wakiume mahardcore, waimbe na kucheza taarabu mbele ya wenzao, nasikia pia alipokuwa akipigisha kwata utajuta kuwa mwanafunzi wa Makongo, kina Babu Ayubu, hawawezi kumsahau kabisa, cause mpaka sauti yake alikuwa anaiigiza vizuri kabisa

eeh! R. I. P
 
Kuna huyo madamme alikuwa kiherehere kweli yani anaingia dom la boys ka ladies room kuja kuamsha watu asubuhi,ikapangwa mbinu jamaa akachukua shuka na kujifunika usoni baada ya kumsikia anakuja huku chini akiwa uchi antenna juu,madame kuja jamaa akawa anamfwata straight we! Madame alisepa na akakoma kale katabia

madam nani? Shule gani? Alikuwa kaolewa?
 
Mwl wa nidhamu, shule moja huko kanda ya Kasikazini. Huyu yeye alikuwa anawaamusha wanafunzi saa kumi usiku kwa ajili ya machakamchaka. Na alikuwa ngumi mkononi. Alikuwa anakuja kimya kimya bwenini, na kuwasha taa huku akitoa sauti kali ya kutoka nje. Basi madogo walikuwa wanatoka nje na chupi tu kwa hofu.
Bweni moja waliamua kumtega kwenye swichi ya umeme. Jamaa kama kawaida alipofika mlangoni, kutaka kuwasha taa akakutana na waya wa umeme na kupigwa shock. Jamaa aliruka sana na kuanza kusema 'hamniwezi, hamniwezi huku akiondoka'. Nisikilizie tibwili lake asubuhi, bweni shughuli ilikuwepo. Lakini huyo ticha alikuwa noma kwa kuamsha mchakamchaka utafikiri alikuwa hajaoa, kumbe alikuwa na mke na watoto kadhaaaaa.

Hahahaaaaa. Huyu ni mwl Mpande, e bwana eeee huyu alikuwa kiboko! Kusimamia nidhamu yeye, mchakamchaka yeye, akikuta mjini unaye, ukikorofishana na kiranja unaye.

Yaani yeye alikuwa mwl wa zamu fulltime.

Kutokana na kutusumbua kukimbia mchakamchaka kila siku, siku moja tukiwa form six tuliamka saa nane usiku, tukawa tunakimbia kuzunguka nyumba ya headmaster huku tukiimba kwa sauti. Tulizunguka kama mara ishirini hivi. Asubuhi yake ilikuwa ni noma, maana headmaster alimaind akatuambia tukimbie huku akitufuata kwa gari.

Mpande alikuwa ni zaidi ya headmaster ingawa hakuwa, yaani kila kitu yeye.

Sitasahau adhabu zake za kuwachukua wanafunzi wa korofi hasa form one, anawapakia kwenye gari na kuwapeleka stand ya bus, huku akiwachimba mkwara: unajifanya mjanja, unarudi kwenu! Anaongea na makondakta, dogo anakatiwa ticket fake halafu anaambiwa subiri gari.

Madogo walikuwa wanasubiri hapo stand weee mpaka saa 12 jioni, halafu baadaye anamrudisha shuleni. Dogo akifanyiwa hivyo harudii tena Kosa.

Bweni alilotegwa umeme nadhani ni Dom 35, Karume.
 
aaaaa Ngui weeee aka baba kadoda wa pale mkwawa..nakumbuka ulivokuwa unajificha kwenye mahindi kutuvizia tukiwa tunatoka makanyagio kununua maandazi kwa mama Amuru.....
 
Kulikuwa na Ticha moja second master huko Mara sekondari anaitwa Bachubira nickname (luba) ana nata kinoma ngumi mkononi shule haikuwa na fensi wanafunzi wa bweni walitoroka kwenda Musoma town kudadadadeki anakariri huyo hadi kisogo hata akikuona mbali atakuatambua, umesimama paredi anapita kila mstari unashangaa anakudaka NILIKUONA MJINI unatoka uwanja wa karume kucheki mechi taja na wenzako na kweli hasingizii mtu,adhabu ya hapo uchague kuingia mgodini(kutapisha choo/karo) au suspension.Kulikuwa na jamaa mmoja mfupi sana ukienda nae town lazima mkamatwe watu walimkimbia eti nuksi!

Akiwa anakuja mabwenini utasikia mtu anatoa muruzi kisha anaita machaleeee! utasikia vishindo watu wanatimuka au bila hata sababu bora wasikutane nae uso kwa uso maana atakubambikia kesi hapo hapo mfano ni denti alinyoa kipara akapigwa suspension ya wiki mbili mpaka nywele ziote.

Kuna jamaa mtundu alikuwa mcheza serekasi alimweza siku moja, ukaguzi usafi ni kila thursday anakagua ndefu,kucha,mikanda mipana n.k akamkuta jamaa kwa makusudi kavaa laba za kike ticha kamvua kakatiza huku jamaa akimfuata akisema nipe viatu vya mama! sitosahau hiyo vunja mbavu
ni hadith nyingi ntantoa nyingine naogopa kujaza ukurasa.

Hii kiboko, nipe vyatu vya mama!
 
Hahahaaaaa. Huyu ni mwl Mpande, e bwana eeee huyu alikuwa kiboko! Kusimamia nidhamu yeye, mchakamchaka yeye, akikuta mjini unaye, ukikorofishana na kiranja unaye.

Yaani yeye alikuwa mwl wa zamu fulltime.

Kutokana na kutusumbua kukimbia mchakamchaka kila siku, siku moja tukiwa form six tuliamka saa nane usiku, tukawa tunakimbia kuzunguka nyumba ya headmaster huku tukiimba kwa sauti. Tulizunguka kama mara ishirini hivi. Asubuhi yake ilikuwa ni noma, maana headmaster alimaind akatuambia tukimbie huku akitufuata kwa gari.

Mpande alikuwa ni zaidi ya headmaster ingawa hakuwa, yaani kila kitu yeye.

Sitasahau adhabu zake za kuwachukua wanafunzi wa korofi hasa form one, anawapakia kwenye gari na kuwapeleka stand ya bus, huku akiwachimba mkwara: unajifanya mjanja, unarudi kwenu! Anaongea na makondakta, dogo anakatiwa ticket fake halafu anaambiwa subiri gari.

Madogo walikuwa wanasubiri hapo stand weee mpaka saa 12 jioni, halafu baadaye anamrudisha shuleni. Dogo akifanyiwa hivyo harudii tena Kosa.

Bweni alilotegwa umeme nadhani ni Dom 35, Karume.

mpande mzee wa panda juu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom