nachid
JF-Expert Member
- Apr 14, 2011
- 936
- 203
dah! bahati mbaya sina namna ya kukuwajibisha lakini ulichofanya si sahihi hata kidogo, dawa huwa hazitangazwi hovyo kama wewe ulivyoandika na ndio maana hata ukisikiliza vipindi vya redio madaktari huzungumza ugonjwa, dalili, vipimo lakini itakapokuja dawa hawataitaja maana dawa na dose ziko individualized, aina utakayotumia wewe siyo nitakayotumia mimi, hali kadhalika dosi utakayotumia wewe siyo nitakayotumia mimi, maana japokuwa twaweza kuwa na tatizo moja lakini mwili wako ni tofauti na mwili wangu hali kadhalika severity of disease kwako ni tofauti na kwangu, sasa wewe hapo unapopromote hiyo dawa kisha mtu akaenda akajinywea hovyo akifa au akipata madhara itakuwaje?
social media ni nzuri lakini uncontrolled medical promotion and advertising ni mbaya sana, kwanza ni kinyume cha sheria kutangaza dawa kwenye vyombo vya habari ndio maana hujawahi kusikia dawa yoyote ikitangazwa gazetini au kwenye redio au tv, with exception of ALU, na hii ALU ilifanywa makusudi ili wananchi waielewe maana wengi walikuwa wakiikataa na pia ilifanywa kwa kuwa malaria ni disease of national interest na sio tatizo 'dogo' kitaifa kama impotence
pili hapo umefanya makosa mawili kwanza kutangaza tadalafil lakini mbaya zaidi unaitangaza LEVITRA kwamba ndio tadalafil lakini levitra ni VARDENAFIL, mimi ningekuwa ni mods ningeiondoa hii thread kwa sababu umefanya pharmaceutical advertising kinyemela kwa kuitangaza specifically LEVITRA, je wewe ndo agent wake hapa bongo? lakini pia umechanganya watu kwa kuwaambia levitra ndio tadalafil wakati levitra ni vardenafil
jamani tusipende kutumia madawa hovyo kwa kusoma kwenye internet, kusoma kutoka kwa watu laymen kama hawa bila kwenda hospitalini, ni hatari sana, especially hizi dawa za mitindo ya maisha, life style diseases sio nzuri kujinywea hovyo hovyo, na mwisho dawa za kuongeza nguvu za kiume ni HATARI sana kama una matatizo katika mfumo wako wa damu( cardiovascular system).
thanks ndo raha ya jf