Unakumbuka Simba ya Azim Dewj na Yanga ya Abass Gulamali?

Miaka hiyo watu tunabet team yangu ikifungwa nakupa mke wangu alale kwako siku mbili nami nikishinda unanipa mkeo.

Au unakuta mwenye nyumba anasema simba au yanga ikifungwa kodi miezi sita hulipi. Hapo mpangaji anaombea ile mbaya timu husika ifungwe ....

Miaka hiyo mtu anahama mji week nzima. Na refa akichezesha vibaya anaondoka chini ya ulinzi mkal wa FFU NA HAPELEKW KWAKE MPAKA WEEK 2 ZIPITE
 
It was 1991 Uwanja wa Aman Zanzibar Kombe la Africa Mashariki imefika wakat wa Mikwaju ya Penalt Pambano limechezwa Usiku Penalt ya Mwisho anaenda kupiga Beki wa Yanga David Mwakalebela anapaisha na Simba inatwaa Ubingwa! Aiseee tulijikuta Washabiki wa Simba damu tumefurika Msimbazi kuanzia saa 6 usku mpaka Alfajiri bila ya kutarajia
 
Tusimsahau Alfred Kategile, Damian Mrisho Kimti hahah
Sijui nini kilimkuta kategile nadhani ulabu ila huyu alikuwa winga khatari sana ya kushoto product ya biashara shinyanga hiyo yeye na mwinyimvua komba (masolwa )Ahmed abbas Michael Paul (nylon )abdalah magubika (zagada )edibily lunyamila dhikiri mchumila aly ngaoneka Paul John Masanja hizi zote products za biashara shinyanga.
 
Mie nikiwakumbuka kina Mahadhi bin Jabeer na Kina Sunday Manara naishia kusema Al hamdulillah Kama hatukufanikiwa kipindi kile kimpira basi Mafanikio yatashuhudiwa na Kizazi kingine sio chetu
 
Mie nikiwakumbuka kina Mahadhi bin Jabeer na Kina Sunday Manara naishia kusema Al hamdulillah Kama hatukufanikiwa kipindi kile kimpira basi Mafanikio yatashuhudiwa na Kizazi kingine sio chetu
Wale sio wa kuwa kumbuka kabisa chozi linaweza kukutoka umahiri wao leo nani mpaka mahadhi na dilunga timu ya afrika haikuwa mchezo.Leo kizazi cha kina mohamed salim yahya tostao mwinyimkuu njohole thuweni kiswabi mwinda ramadhani (maajabu )elius Michael George kulagwa huwezi kuwafananisha uwezo wao na hawa wetu wa leo.
 
Huyu mwinyimkuu njohole alikuwa na uhusiano na deo njohole?

Wale sio wa kuwa kumbuka kabisa chozi linaweza kukutoka umahiri wao leo nani mpaka mahadhi na dilunga timu ya afrika haikuwa mchezo.Leo kizazi cha kina mohamed salim yahya tostao mwinyimkuu njohole thuweni kiswabi mwinda ramadhani (maajabu )elius Michael George kulagwa huwezi kuwafananisha uwezo wao na hawa wetu wa leo.
 
Ha ha ha..umenikumbusha mechi moja ya kombe la a. Mash na kati anaingia kocha mchezaji Hassan Hafif kubadilisha matokeo kipindi cha pili simba wanawapiga Waganda Bao 3. Sijui yule jamaa alienda wapi. Hassan Hafif sikuwah msikia tena kwenye soka.

It was 1991 Uwanja wa Aman Zanzibar Kombe la Africa Mashariki imefika wakat wa Mikwaju ya Penalt Pambano limechezwa Usiku Penalt ya Mwisho anaenda kupiga Beki wa Yanga David Mwakalebela anapaisha na Simba inatwaa Ubingwa! Aiseee tulijikuta Washabiki wa Simba damu tumefurika Msimbazi kuanzia saa 6 usku mpaka Alfajiri bila ya kutarajia
 
Sanif lazaro tingisha namkumbuka sana kwa mabao yake. Na abeid mziba alikuwa mzuri sana kwa mabao ya vichwa. Yanga walikuwa na kipa wao mwenye mbwembwe halaf mtemi juma pondamali.

Alikuwa kivutio sana miaka ile.

Marehemu selestini sikinde mbunga, Deo Njohole, makumbi Juma, sanifu Lazaro Tingisha, zamoyoni Mogera, Abeid Mziba, Abubakari Salumu (sure boy)

Hawa kina Lunyamila walikuja baada ya kina Sanifu kuondoka
 
Aisee mnanikumbusha wachezaji kma justine mtekele, na waganda walikuwa na majid musis alikuwa balaa sana huyu jamaa. Alikuwa na nguvu. Simba walikuwa na mpiga penalty mahiri hussein marsha alikuwa akienda kupiga penalty watu wanaanza kushangilia. Pia alikuwa bishoo hapendi kuchafuka uwanjan wala hachezi rafu
 
Marehemu selestini sikinde mbunga, Deo Njohole, makumbi Juma, sanifu Lazaro Tingisha, zamoyoni Mogera, Abeid Mziba, Abubakari Salumu (sure boy)

Hawa kina Lunyamila walikuja baada ya kina Sanifu kuondoka

Sio Sahihi!!! Ingawa Umri Ulikwisha Songa Lakini Sanif Lazaro Kuanzia Katikati Ya Miaka Ya 90s Alicheza Pamoja Na Lunyamila hasa Pale Lunyamila Aliporejea Kutoka Malindi SC ya Mjini Unguja Unguja.
 
Natamani Nimtaje Mfalme Abdallah King Kibaden Lakini Nahofia Reaction Za Mashabiki Wa Yanga manake Huyu Jamaa Hat trik Aliyochomoka Nayo Si mchezo..
 
It was 1991 Uwanja wa Aman Zanzibar Kombe la Africa Mashariki imefika wakat wa Mikwaju ya Penalt Pambano limechezwa Usiku Penalt ya Mwisho anaenda kupiga Beki wa Yanga David Mwakalebela anapaisha na Simba inatwaa Ubingwa! Aiseee tulijikuta Washabiki wa Simba damu tumefurika Msimbazi kuanzia saa 6 usku mpaka Alfajiri bila ya kutarajia
Hii ilikuwa 1992, 1991 walicheza Fainali Simba na SC Villa, Simba akatoka kifua mbele 3-0.
 
Sc villa walikuwa wazuri sana.una kumbukumbu nzuri. Villa sijui kama wapo. Nakumbuka na zanz ilikuwepo miaka hiyo small simba ,malindi na mandege kama sikosei kombe la a.mash na kati mech zinachezwa usiku ilikuwa raha sana ushindan wa miaka ile.

Kulikuwa na nyota nyekundu hawa walikuwa wanaogopwa sabab ya kuchapa buti. Huko tanga kulikuwa na coastal union, mbeya kuna Tukuyu Stars, morogoro kuna reli ,mwanza kuna wana TP lindanda Pamba. Hizi team zilikuwa zinachangamoto kwa simba na yanga sana.
 
Mimi ni miongoni mwa walioshuhudia mpira ukichezwa kipindi hicho. Ni kweli mpira ulikuwa unapigwa, lakini hakuna tofauti sana na unavyopigwa sasa, ndio maana hata timu yetu ya taifa haikuweza kufanya lolote la maana. Tofauti tu ni kwamba wakati ule watu waliokuwa na vipaji vya asili walikuwa wengi ukilinganisha na sasa. Kinachosababisha tuone mpira ulikuwa mwingi kuliko sasa ni ile asili ya binadamu kupenda vya zamani kuliko vya sasa. Hata kina Gerd Muller, Paul Gaza, John Barnes, Abedi Pele, George Weah na wengine wa nyakati zilizopita wanasifiwa kuliko kina Robert Lewandowski, Yaya Toure.
Kombe la challenge lilichukuliwa kipindi gani?
Soka ilikuwepo kuliko sasa Ndugu! Be fair
 
Kiukweli miaka hiyo kulikuwa na ushindani mkubwa sana kati ya Matajiri hawa wawil na Simba na Yanga. Sijui ni nini kiliwatoa kwenye Ule Ushindani.

Mechi zao zilikuwa zikitabiria na watabiri akina Majura na mtabiri mwingine nmemsahau katika magazeti ya Mfanyakazi.

Nawakumbuka wachezaji kama akina abedi mziba,fred minziro,hussein marsha, george masatu, mtwa kihwelu,itutu kigi,nonda shaban,said mwamba kizota,fumo felician,danny mhoja,twaha hamidu,zamoyoni na method mogella,salum kabunda ninja, athuman china,idd paz n.k

Miaka hiyo wachezaji walikuwa wanajituma sana. Wanacheza kwa nguvu na akili. Mpira ulikuwa unasakatwa hasa.

Huku azim dewj na abbas gulamali wakitambiana ile mbaya.
hawa Wahindi wa Yanga si Yanga asilani - wote ni Simba na historia inathibitisha hilo. wapo Yanga kwa maslahi ya kibiashara tu.

hicho cha Wahindi hakinishangazi sana kwani kwao ni biashara. kinachonishangaza ni kwa Waswahili kapuku kuishabikia Simba!
 
Enzi zakina sanif lazaro 'tingisha' salum kabunda 'ninja'. Watangazaji wa mpira redio Tanzania walikuwa wanajua Sana kunogesha matangazo. Unasikia 'wao bila sisi moja'
Burudani hizi zilikuwa zinaletwa na RTD, kupitia kwa watangazaji wake mahiri akina omary jongo na ahmed jongo.
 
Bila kuwasahau

John makelele
Ndege john
Dowa said
Raphael paul
Steven nemes
Said John
Deo mkuki
Hamis gaga
Malota soma
George masatu
Hussein masha
Mohamed mwameja
Kimti
 
Back
Top Bottom