Unakumbuka porojo za makamba;lukuvi aamua ku paste

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
Lukuvi: Kiama cha wamachinga Okt 30

Na Hilary Komba

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. William Lukuvi ametangaza kuwa ifikapo Oktoba 30 mwaka huu wamachinga wawe wameondoka katika maeneo yasiyo rasmi vinginevyo timuatimua itaanza upya.

Bw. Lukuvi alisema hayo Dar es Salaam katika mazungumzoa yake na watendaji wa Manispaa ya Ilala wakiwamo wenyeviti wa serikali za mitaa, watendaji na madiwani juzi.

Alisema biashara zote ambazo zinafanywa katika maeneo yasiyo rasmi yakiwemo maeneo ya barabara zinatakiwa kuondoshwa kabla ya tarehe hiyo ambayo imetangazwa kwa lengo la kufanya jiji kuwa tofauti na lilivyo hivi sasa.

"Jiji la Dar es Salaam limekuwa chafu sana kutokana na uzembe wa kusimamia sheria, sasa wakati umefika kwa wakazi kubadirika na nitahakikisha jiji hili linakuwa safi na kufanana na halmashauri ya Moshi ambayo imetumia sheria zake kuyaweka mazingira katika hali ya usafi.

Alisema timuatimua hiyo itaziondosha biashara zote zinazofanywa katika maeneo yasiyorasmi zikiwemo biashara za maji ya kunywa ya chupa, nguo, miwa, machungwa na aina ya zote za vyakula.

Kwa mujibu wa Bw. Lukuvi shughuli hiyo ya timuatimua itafanywa na askari wa Jeshi la Polisi na wale wa jiji ambao watawakamata watakaokaidi kuondoka.

Alisema timuatimu hiyo pia itawakumba wenye gereji katika maeneo yasiyo rasmi, baa zinazopia muziki wa juu katika makazi ya watu, vyoo vinavyotiririsha maji ya vyooni, wanaocha magiari barabarani, kutupa taka ovyo, wanaojisaidia maeneo yasiyo rasmi.

Naye Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Bw.Suileman Kova alisema jeshi lake limejipanga vizuri kwa kuwakamata na kuwafikisha watu wanaovunja sheria kwa kufanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi.

Alisema shughuli hiyo haitakuwa nguvu ya soda, kwani yeye hapendi kushindwa jambo, hivyo machinga watakaokaidi amri yake hatawaonea huruma kwa sababu mpango huo ni wa kuliweka jiji katika mazingira ya usafi.

USHAURI

USI COPY KAMA HUJUI KU PASTE
 
Lukuvi mh
mh makamba alikuja na yote hayo wacha la kuhamisha omba omba na kutumia pesa za jiji kuwarudisha makwao waliishia kuwaona njiani baada ya wiki mbili akurudia tena...alichofanikiwa ni kumuhamisha mzee wetu tuliempenda mzee matonya........kariakoo ilikuwa safi kabisa hakuna alieamini unapishana na mtu kama unapishana na gari....leo hii kariakoo machinga wamejaa mpaka kwenye mlango wa mkuu wa kituo cha polisi msimbazi...we unakuja na lipi jipya...unakumbuka ulianza na la kuapa kamatakamata ya magari mjini biashara inayoendeshwa na wakuu wenzako wakiongozwa na rto.....leo hii magari yanakamatwa hata umepaki sehemu yako na askari wa jiji...kumbe hii ilikuwa nguvu ya soda baada ya maaskari wa jiji kumkamata mamaa lukuvi ...sasa haya mambo utafanikiwa ....???mtangulize mungu usionyeshe watu
 
Back
Top Bottom