Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unakumbuka nini wakati wa JKT

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Facts1, Jan 8, 2010.

 1. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani ni vizuri kujikumbusha mambo yaliyopita na ni kujifunza vilevile.

  Nilipomaliza Form six nilichaguliwa kwenda Bulombora JKT Kigoma, tulifika Kigoma stasheni saa 12 jioni tulikuwa kama 30 hivi, gari la jeshi lilikuja saa 4 usiku ilituchukua mwendo wa karibu masaa 3 kwenda kambini. Tulipofika tukakuta chakula kipo tayari tulipouliza maji ya kunawa namkumbuka afande aliyekuwepo anaitwa Nusu Mungu akatujibu unaulisa maji yakunawa jeshini akatuambia tunawe kwenye umande sikuamini.

  Baada ya chakula ilikuwa mida ya saa 9 usiku tukapelekwa kwenye hanga kulala, kabla ya kuingia afande akatuambia kwenye hili hanga kuna vitanda vitano tu kwa hiyo atakayewahi ndiye atakayelalia kitanda, kwa vile mimi niambiwa ukifika jeshini lazima uwe shapu shapu sikujivunga, ukachorwa mstari umbali wa kama hatua hamsini kutoka kwenye hanga filimbi ilipopulizwa nikawa mtu wa tatu kuingia tulipotimia watano afande akafunga mlango nikawa na uhakika nimepata kitanda, cha ajabu akasema sasa nyie ndio mnajifanya ki-fowadi fowadi yaani kimbelembele inabidi mlifagie hili hanga na ku-lideki, kweli tuli deki hadi kukapambazuka wakati wenzentu wakiimba tu mapambio pale nje. Hii ni experience yangu tu kama unayo ya kwako tuletee.
   
 2. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,616
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  kaka pole, ila hongera hanga lenu lilikuwa hata na sakafu sementi ya kudeki? vipi madekio mlipata wapi? ndo za kudekia na maji jee mlichotea kwenye nini?

  hilo ndiyo JKT mzee.
   
 3. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yule afande alichofanya ni kutuonyesha maji yanapopatikana basi ndoo madekio fagio ilibidi tuhangaike wenyewe, najua kuna wengi hawataamini lakini ndivyo ilivokuwa.
   
 4. Gelange Vidunda

  Gelange Vidunda JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 311
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  "Disco", mchakamchaka saa 11:45 asubuhi (na 841 KJ, JKT Mafinga muda huo sio mchezo!! Kiwinter sio cha kawaida!), miraba Idetero, mboga za majani ya kombania Dubliganga......

  Ngono......
   
 5. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vipi watu Ruvu mpo mnayakumbuka mayai, kuna siku tulienda Ruvu kwa michezo sisi wageni tukapendelewa kulinda mabanda ya kuku usiku, nilijaza trey kama mbili za mayai kwenye mifuko ya kombati ili nitoke nayo, sasa kumbe asubuhi yake kabla ya kukabidhi lindo kuna ka gwalide na mazoezi kidogo pushapu, uvingike mayai yote yalipasuka ilikuwa soo ndugu yangu.
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 25,512
  Likes Received: 1,596
  Trophy Points: 280
  Uzinzi mtupu
  mtu akikupenda;kamnda akimpenda si wako maisha gani kuumizana ni hilo tu sito nasema sitolisahau
   
 7. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2010
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 888
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  842 KJ, hapo ni Mlale JKT, Kuna shamba linaitwa embakassy, na kitu inaitwa bigula, hupigwa saa nyingine mpo kwenye foleni ya msosi inabidi muache, hapo ni afande Mtono (RIP) Kaanzisha kamoto makusudi ili mkazime
   
 8. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #8
  Jan 8, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,796
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Facts1 hii topic ni moto sana na iliongelewa sana hapa:

  http://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/21863-je-unakumbuka-nini-enzi-zako-za-jkt.html

  May be Mods anaweza kuziunganisha.
   
 9. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 10. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,709
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nimesikia kwamba JKT inarudi tena kwa Vijana wanaomaliza F 6, sijui iatakuwaje na huu Ukimwi, Mungu ajua.
   
 11. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  nilikuwa bulombora pia!afande ngoma etc!ilikuwa ngumu kwanza,baadae tulizoea!more than a decade !but wanawake walidhalilishwa na maafande!walitoa miili yao bila kupenda
   
 12. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli wasichana walikuwa wanadhalilishwa, unakumbuka kulechini michikichini na matofari kazi kwelikweli na kule serengeti karibu na michungwa?
   
Loading...