Unakumbuka ma-dj wakali enzi hizo?

MT255

JF-Expert Member
May 3, 2012
3,346
4,605
Unakumbuka ma -dj wakali enzi hizo.... 1.dj jerry koto 2.dj young millionea 3.dj chriss fabi (the lover) 4.dj deo zullu 5.dj kali kali 6.dj mangapiii 7.dj ali koko endelea tupia hapa ma-dj wa zamani.....
 
dj chalz....dj venture.....bonny luv....na wengine wengi.....
 
hao ulio wataja ni wa juzi 2 mi nazungumzia enzi hizo mfano...enzi za mboe leo hii club bilicanas.
 
....Wote tisa 10 alikuwa ni DJ Kalikali pale Mbowe huyu alikuwa akiamua kupanga mawe halafu kishapata safari mbili au tatu kichwani basi utasuuzika na roho yako. RIP Kalikali
 
mkubwa BAK nimekukubali...huyo ulie mtaja alikuwa moto wa kuotea mbali....dah...wakati umeenda sana enzi hizo ulikuwa unaomba usiku usiishe!
 
Mie namkumbuka Kim&Boyz kwenye Yo Rap Bonanza,pia nakumbuka Tulipokua tunaenda kuchukua watoto magoti.
 
Mie namkumbuka Kim&Boyz kwenye Yo Rap Bonanza,pia nakumbuka Tulipokua tunaenda kuchukua watoto magoti.

Da aisee umenikumbusha mbali King Kong III, huyu jamaa ndo alianzishaga yale mashindano ya Disco ambapo walipatikana washindi kama kina Maneno Ngedere, MC diga Diga, Super Nyamwela, mashindano yalikuwa yanafanyika pale Lang'ata na Vijana Kinondoni!

RIP waliotangulia mbele za haki.
 
Kwa Morogoro alikuwepo jamaa alikuwa anaitwa Dj sweet coffee Banana akiwa anapiga Disco pale ukumbi wa shimoni Morogoro Hotel huku John Dillinga, wakati huo akiwa anajulikana kama John Mkimbizi akiwa anasaidia kupanga tape na kuzungusha kwa pen 'cueing'. Dj Peter Mo ambaye kwa sasa huwa namsikiliza kwenye Groove back kila Jumamosi kupitia clouds FM alikuwa akikaa mita 2 mbali kabisa na walipo ma-dj yaani akina sweet coffee banana na msaidizi wake John Mkimbizi!
Those were the days jmn acheni tu!
 
Hivi Dj john delinga makloo kapotelea wapi! Yaani alikuwa akijitaja tu hilo jina lake mi nasuuzika kabla ya mziki wenyewe!
 
BAK best wangu, hebu jitaje enzi zako ulikuwa unaitwa dj nani! Manake hujambo baba!
....Wote tisa 10 alikuwa ni DJ Kalikali pale Mbowe huyu alikuwa akiamua kupanga mawe halafu kishapata safari mbili au tatu kichwani basi utasuuzika na roho yako. RIP Kalikali
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Hivi Dj john delinga makloo kapotelea wapi! Yaani alikuwa akijitaja tu hilo jina lake mi nasuuzika kabla ya mziki wenyewe!

Kiukweli John Dillinga Matilou aka John Mkimbizi yaani DJ JD aka Ever lasting DJ alikuwa mkali kuanzia kwenye Radio shows hadi Club. Kuna wakati walibamba sana wakiwa na ka-group kao ka Ma-Dj wanne akiwemo Jd mwenyewe na Rico walibamba sana jiji la dsm.

Kwa sasa nasikia jamaa anafanya biashara zake ikiwa ni pamoja na kuagiza magari japan na kuuza bongo!
Nam-respect sana John Dillinga maana anao uwezo wa kweli kwenye art ya u-dj.
 
BAK best wangu, hebu jitaje enzi zako ulikuwa unaitwa dj nani! Manake hujambo baba!

Best King'asti hahahahah lol! mie nyimbo nyingi kwanza kabisa nimezijulia kupitia wazazi maana nao ni wapenzi wakubwa wa muziki na katika kujirusha rusha katika viwanja mbali mbali vya starehe, lakini ukweli ni kwamba BAK hajawahi kuwa DJ ila Best ukiwa na kashughuli kanahitaji DJ :):) basi usipate shida wala sikuchaji kitu :)...mie na weye dam dam
 
Last edited by a moderator:
enzi hizo Ma-Dj walikuwa wanaheshimika sana.zamani ulikuwa huwezi kumkaribia dj kirahisi disco....
 
mkubwa BAK nimekukubali...huyo ulie mtaja alikuwa moto wa kuotea mbali....dah...wakati umeenda sana enzi hizo ulikuwa unaomba usiku usiishe!

Pale Mbowe kulikuwa pia na DJ Gerald, wapenzi wa Mbowe walikuwa wakishuka pale na kukuta DJ Kalikali hayupo, yupo Gerald basi walikuwa wanapatwa na simanzi :):) hakuwa mbaya kihivyo lakini DJ Kalikali alikuwa ni moto wa kuotea mbali. Kama umeenda kucheza muziki basi utasuuzika na roho yako ukitoka pale 10 au 11 za asubuhi roho yako nyeupeeee.
 
Lol! Kumbe mtoto wa nyoka weye manake unajua miziki kama mzazio!
Tatizo la dj wa bure koo linakuwa kama lina turbo, unameza vimiminika tu! Ntakufikiria lakini best, besdei yangu basi.
Best King'asti hahahahah lol! mie nyimbo nyingi kwanza kabisa nimezijulia kupitia wazazi maana nao ni wapenzi wakubwa wa muziki na katika kujirusha rusha katika viwanja mbali mbali vya starehe, lakini ukweli ni kwamba BAK hajawahi kuwa DJ ila Best ukiwa na kashughuli kanahitaji DJ :):) basi usipate shida wala sikuchaji kitu :)...mie na weye dam dam
 
Last edited by a moderator:
yaah ni kweli kipindi hicho unaweza ukawa unaenda disco fulani kwa sababu ya dj tu.mimi nakumbuka CHRISS FABI(THE LOVER)alikuwa ananivutia sana jamaa alikuwa anajua sana.(R.I.P)
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom