Unakubali wanandoa waaminifu wenza wao huwa opposite

The Hunter

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
1,049
305
Wana JF mara nyingi katika jamii tunamoishi tumeshuhudia ama kuhadithiwa na wakati mwingine kuona Mwanandoa fulani anaisaliti ndoa yake, unapochunguza upande wa pili unamkuta mtu huyohuyo ana mke au mume mwaminifu kabisa;

Na binamu yangu mmoja yeye ameoa kama miaka minne nyuma lakini jamaa ni malaya mbwa, nyumbani ana mke mzuri mwenye staha, na mwenye kujiheshimu sana, lakini mumewe ndo ivo tena, jamaa mtaani ana watoto zaidi ya nane sasa,
Mdogo wake alimuiga kaka mtu matokeo yake akapita kusipo, katembea na vibinti karibu vyote mtaani, hapo alipo afya imeshaanza kudhoofu na mbaya zaidi kaka yake nae katembea na baadhi ya hao mabinti.

Tuamini kuwa hakuna aliyezaliwa akijua, hivyo kila mtu hufunzwa, kama unahisi mwenzako hakuridhishi mfunze, mwelekeze, tuache uzinzi kwani mwisho wake ni kuugua na hata kuwaambukiza wasio na hatia
Kumbuka ukishaupata ndo niwako tena hutapona, utakuwa ni maiti inayotembea, hutakuwa na furaha na hata hao unaoshiriki nao watakukimbia
.
 
Nakubaliana na wewe, ila pia tambua kuwa uzinzi ni tabia regardless unaishi na mwenza mwaminifu kiasi gani!! Nawashauri wenye tabia hizi waache jamani
 
Ukiskiliza stori za waathirika wengi wanadai wenza wao ndo wamewaletea maambukizo.
angalia kwenye familia ama ukoo wako kama hutakutana na kesi za namna hii, hii nikumaanisha mmoja anakuwa mwaminifu huku mwingine ni malaya wa kisirisiri.
 
Wazinzi wajanja sana, huchagua wenza wenye tabia ya kufaa ili familia iweze kuwa na hata mmoja wa kuijali.
 
mkubwa unenalo ni kweli kabisa... na nafikiri ni mpango wa mungu katika kuweka balance!! hebu fikiria mkikutana wote vicheche aina ya ndoa mtayokuwa nayo itakuwaje? so to balance mungu amefanya opposite charges ( mwaminifu na asiye mwaminifu) ndo wacop vizuri...
 
Songíto;2919470 said:
na nafikiri ni mpango wa mungu katika kuweka balance!!

mawazo ya kibinadamu siku zote huwa hayana hitimisho la kueleweka juu ya mipango ya Mungu kwa sisi binadamu. Yaani Mungu anapanga john na Janeth mmoja awe mzinzi mwingine mwaminifu..........duuuuuuuuuu, ni mawazo ya aina yake juu ya mipango ya Mungu kwa binadamu!
 
Wana JF mara nyingi katika jamii tunamoishi tumeshuhudia ama kuhadithiwa na wakati mwingine kuona Mwanandoa fulani anaisaliti ndoa yake, unapochunguza upande wa pili unamkuta mtu huyohuyo ana mke au mume mwaminifu kabisa;

Na binamu yangu mmoja yeye ameoa kama miaka minne nyuma lakini jamaa ni malaya mbwa, nyumbani ana mke mzuri mwenye staha, na mwenye kujiheshimu sana, lakini mumewe ndo ivo tena, jamaa mtaani ana watoto zaidi ya nane sasa,
Mdogo wake alimuiga kaka mtu matokeo yake akapita kusipo, katembea na vibinti karibu vyote mtaani, hapo alipo afya imeshaanza kudhoofu na mbaya zaidi kaka yake nae katembea na baadhi ya hao mabinti.

Tuamini kuwa hakuna aliyezaliwa akijua, hivyo kila mtu hufunzwa, kama unahisi mwenzako hakuridhishi mfunze, mwelekeze, tuache uzinzi kwani mwisho wake ni kuugua na hata kuwaambukiza wasio na hatia
Kumbuka ukishaupata ndo niwako tena hutapona, utakuwa ni maiti inayotembea, hutakuwa na furaha na hata hao unaoshiriki nao watakukimbia
.
#
binamu ako umesha mshauri? usitoe punje kwa majicho ya wenzio, ilihali banzi bado kwa jicho lako
 
Back
Top Bottom