Unajua maana ya jina Msasani?

Yoso

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
340
239
Je unaijua maana ya neno Msasani ambalo ni jina la eneo maarufu jijini ambalo alipata kuishi mwasisi wa taifa hili Mwl JK Nyerere?

Jina hili linatokana Mzee maarufu aliyeishi maeneo hayo aliyejulikana kwa jina la MUSA HASANI miaka ya 1930's.

Wwahamiaji wengi wa jamii ya kimakonde waliofika maeneo hayo walitamka jina la mzee huyo kwa lafudhi ya kikwao walimwita MUCHA CHANI ,hivyo ndiyo ikawa chimbuko la jina MSASANI.

Je wewe unafahamu chimbuko la jina gani? Lete hapa jukwaani!
 
KARIAKOO
Pale ambapo pamejengwa soko, wakati wa vita ya pili ilikuwa kambi ya wapagazi [wabeba vifaa na mizigo ya jeshi] ambao waliitwa 'Carrier Corps'
lakini wenyeji walitohoa jina hilo na kuita kariakoo.

KAWE
Enzi hizo za mkoloni ng'ombe walioletwa toka mikoani walikuwa wakipita njia maalum zilizotayarishwa kwa ajili hiyo njia hiyo iliishia kiwandani tanganyika packers. Wenyeji katika matamshi badala ya kuita COW WAY wao waliita kawe
 
newala =Wajerumani au waingereza walizindua kisima kipya

wakakiita New Well......ndo ikaenda hadi Newala lol
 
Lakini kuna rafiki yangu mmoja kutoka Swaziland, yeye alikuwa anaogopa sana kuitamka Msasani kwa sababu ati kwao ni tusi kubwa. Aliniambia hawezi kutamka neno hilo mbele ya mama yake, maana kufanya hivyo ni kuitamka njia ambayo alitokea kuja duniani kupitia kwa mama yake. Hakuwa straight lakini nadhani nilimuelewa. Yeye mwenyewe majina yake kwa hapa kwetu ni matusi kutamka, lakini alisema ukienda kwao lazima utamke majina hayo kwa sababu ni ya ukoo wao maarufu. Wengi walipenda kumuita jina la kwanza kwa sababu hiyo.

Ni sawa na hapa Tanzania, wewe kama unaitwa NGUMA ukienda Mbeya tafuta jina lingine la kuitwa ukiwa kule, vinginevyo watakutenga wakidhani wewe ni mhuni na huna adabu. Ukienda Moshi naambiwa usiseme KINU kwa maana hiyohiyo. Kuna eneo linaitwa GONJA NDUNGU, ukienda mbeya usiseme hadharani. Ni kama MCHAMBAWIMA ukilitamka Tanzania bara sipati picha palipo na wazee. Kuna watu wanaitwa MBORO kutoka moshi tena ni maarufu hata redioni nawasikia wakitajwa, nadhani wachaga nao wana mambo mwe! Hata bus limeandikwa jina hilo. Nasemaje napanda bus gani kwenda mjini?

Yote haya ni somo kwamba tamaduni zetu zimekaa kama pilau. Inabidi kuheshimu utamaduni wa mwenzio ili naye aheshimu wa kwako. PERIOD!
 
je unaijua maana ya neno msasani ambalo ni jina la eneo maarufu jijini ambalo alipata kuishi mwasisi wa taifa hili mwl JK nyerere, ni kwamba jina hili linatokana mzee maarufu aliyeishi maeneo hayo aliyejulikana kwa jina la MUSA HASANI miaka ya 1930's wahamiaji wengi wa jamii ya kimakonde waliofika maeneo hayo walitamka jina la mzee huyo kwa lafudhi ya kikwao walimwita MUCHA CHANI ,hivyo ndiyo ikawa chimbuko la jina MSASANI je wewe unafahamu chimbuko la jina gani? lete hapa jukwaani.

Alikuwako mwarabu mmoja kati ya wamakonde akiwa na duka. Jina lake MUSSA HASSAN
 
jangwani pale kulikuwapo na mzee akiitwa hivohivo mzee jangwani, kwa mama zakaria vilevile hapo mwananyamala
 
Kwanini majina yote yanatokana na kuja kwa wageni? inaamaana kabla wageni hawakuja maeneo hayo hayakuwa na majina?
 
At least jina la kwetu limebaki kama mababu walivyoliacha...Songagwegwe
 
Temeke WAILES= tEMEKE WALES...

Ensi hizo pale national stadium na jeshini[ukivuka mandela lilikuwa ni eneo la airport ya dar na upande wa wailesi {ambao uko kwenye muinuko kulikuwa na minara ya mawasiliano ya kampuni iitwayo cable & wireless. wenyeji walilishorten jina hilo na kuita wireless [wailesi] upo broo Dar ina very rich history na zile enzi za utoto wetu tulikuwa tunapenda kukaa pembeni kusiliza na ndiyo maana nasi tunaelewa baadhi ya mambo.
 
Wamarekani wawili walikuwa wanapita maeneo ya Manzese na mmoja awao akashangaa warembo wa kizaramo akasema '' Man....these?''........:baby::baby::baby:
 
Kule kusini kuna jina linaitwa CHILIPUWELI. Lilitokana na maneno SLEEP WELL. Wazungu walipokuwa wanaagana kabla ya kwenda kulala walikuwa wakiambiana hivi, sasa wamakonde wakalidaka hivyo. Kuna staff mwenzetu anaitwa Seif CHILIPUWELI, anatokea Newala
 
Kuna kamtaa kamoja utapoelekea sinza au ubungo Kinaitwa Sheklango.
Hii imetokana na mzee mmoja alikuwa SheKhe na jina lake akiitwa Kilango
Basi walitamka Shekhe Kilango.

Vilevile Mikocheni imetokana na Miti fulani inaitwa Mikochi. Sasa kwa kiswahili kwenye mikochi una sema Mikochini
Basi watu wakamodifai tu ikawa Mikocheni.
 
Back
Top Bottom