Unajua kwa kina sheria za ardhi

MAKOLA

Member
Jun 5, 2010
46
16
Una swali lolote linalohusu sheria ya ardhi, au jambo lolote unalotaka kuhusiana na mambo ya ardhi. NITAKUWA NAPATIKANA KWA EMAIL kwanzamen@yahoo.com. tafadhali uliza swali ambalo ni kweli linakusumbua mjumbe. OFA HII ITAANZA TAREHE "7/6/2010 MPAKA TAREHE 12/6/2010, KAMA SWALI LAKO LINAHITAJI MAELEZO MENGI ANDIKA SIMU YAKO NITAKUPIGIA NIKUELEKEZE."LENGO NI KUSAIDI JAMII KUHUSIANA NA TAALUMA YANGU"
 
Kwa nini usitoe makala ya vitu muhimu kuhusiana na sheria ya ardhi kuliko kutaka watu wakuulize wewe . Kwa nini wakuulize kwa mail na sio kupitia jukwaa hili ? Kama hii ni offer unapata nini in return. kama unasaidia jamii kwa nini offer hii iwe periodocal na isiwe ya kuendelea moja kwa moja?

This may border to touting which is prohibited in law.
 
ngambo ngali: unaweza kuniuliza kupitia jamii forum au kwa email; nimetoa muda huo kwa kuwa nipo na nafasi kwa wakati huo, baada ya hapo nitapata muda mchache sana wa kuaaccess internet. kwani majukumu ni mengi mtu wangu, ila kwa kuwa nafahamu kuna wanajamii kweli wenye shida na maswali ya ardhi ndo maana nikasema nitawacall endapo nitaona kuna umuhimu wa kufanya hivyo, hii yote ni kuokoa mda kakaangu,

" what an oldman see a youngman can not see even though he stands on top of a tree"
 
Ukifanya one to one unasaidia mtu mmoja lakini ukiweka jamvini unasaidia maelfu ambao ni memebers na guests wa hii forum, hebu jaribu kufikiria tena. Kama ulijua una muda mchache na wahitaji ni wengi si ni kudobosha watu wanaohitaji huduma hii kikwelikweli? Umejiunga wiki hii unatoa post na kusema hutakuwa na nafasi huoni yatia shaka?
 
ngambo ngali okey nitatoa makala mtu wangu "naheshimu hekima zako" nitairusha kesho jioni au jumatatu jioni'
 
SHERIA ZA ARDHI NA JINSIA TANZANIASHERIA ZINAZOHUSU MASUALA Sheria ya Ardhi namba 4 ya 1999. 2) Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya 1999.3) Sheria ya Mahakama za Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi namba 2 ya 2002.4) Marekebisho ya sheria ya Ardhi namba 2 ya 2004.5) Marekebisho ya sheria namba 11 ya 2005 sehemu ya nne. Sheria ya Ardhi namba 4 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 zilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1999 na kuanza kutumika rasmi mwezi Mei mwaka 2001. Sheria ya Mahakama za utatuzi wa migogoro ya ardhi ilipitishwa mwaka 2002 na kuanza kutumika rasmi mwezi Oktoba 2003. Misingi Mikuu ya Sheria Hizi ni:• Ardhi ni mali ya umma na imekabidhiwa kwa Rais kwa niaba ya Watanzania wote.• Raia wote wanawake na wanaume wana haki sawa ya kupata, kumiliki, kutumia na kugawa ardhi.• Milki za ardhi zilizopo ikiwa ni pamoja na milki za kimila zinatambuliwa na kulindwa kisheria.• Ardhi itumike kwa manufaa yanayozingatia maendeleo endelevu.• Fidia kamili na ya haki ilipwe kwa mmilika ji bila kuchelewa pale ardhi yake serikali ina poitwaa kwa manufaa ya umma.
3• Kuweka mfumo bora wa utawala na usimamizi wa ardhi ambao unawawezesha wananchi kushiriki katika kufanya maamuzi kuhusu masuala ya ardhi wanayokalia au kutumia.Sheria hizi zinatamka bayana kuwa mwanamke ana haki sawa na mwanaume katika kupata, kumiliki, kutumia na kugawa ardhi. (Kifungu 3(2) cha sheria ya ardhi na sheria ya ardhi ya vijiji za 1999).Usimamizi na Ugawaji Ardhi.• Kwa mujibu wa kifungu cha 29 cha Sheria ya Ardhi namba 4 ya 1999, mwenye mamlaka ya kugawa ardhi na kutoa hati ya umiliki wa ardhi ni Kamishna wa Ardhi.• Kwa mujibu wa kifungu 25 cha Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya 1999 mwenye mamlaka ya kugawa na kutoa hati ya umiliki wa ardhi kimila ni Halmashauri ya Kijiji.Hata hivyo cheti cha hakimiliki ya kimila • Kitatolewa katika fomu maalum. • Kitatiwa sahihi na Mwenyekiti pamoja na Katibu wa Halmashauri ya Kijiji. • Kitatiwa sahihi ama kuwekwa ala ma ya dole gumba na mwombaji. • Kitatiwa sahihi, kuwekwa lakiri na kusajiliwa na Afisa Ardhi wa Wilaya ambamo kijiji hicho kipo.Zingatia• Ni muhimu kila mmiliki wa ardhi awe na hati/ cheti halisi cha hakimiliki kuthibithisha haki yake ya kumiliki ardhi kisheria.
4
• Hati/ cheti cha hakimiliki ya kimila chini ya sheria ya ardhi ya vijiji namba 5 ya 1999 kina hadhi sawa na hati/cheti cha hakimiliki ya ardhi chini ya sheria ya ardhi namba 4 ya 1999.• Hati/ cheti cha hakimiliki ya kimila inaweza kumilikiwa kwa muda usio na kikomo na inaweza kurithiwa au kuhamishwa kwa wosia.Sifa za Kuomba Haki ya Kumiliki Ardhi.Chini ya kifungu 19 cha Sheria ya Ardhi namba 4 ya 1999 watu au mtu anayeweza kuomba haki ya kumiliki ardhi ni:-• Mwanamke au mwanaume Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea.• Kikundi cha watu wawili au zaidi ambao ni raia wa Tanzania na ambao wamejiunga pamoja chini ya sheria ya ardhi au sheria nyingine za Tanzania.• Mtu yeyote au kikundi cha watu ambao si raia wa Tanzania, wanaweza kuomba haki ya kumiliki ardhi, lakini watapewa haki miliki isiyo ya asili (derivative rights) kwa ajili ya uwekezaji.Chini ya kifungu cha 22 cha Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya 1999 wafuatao wanaweza kuomba hakimiliki ya Kimila katika ardhi ya kijiji:• Mwanamke au mwanaume yeyote ambaye ni mwanakijiji mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea.• Mtu yeyote au familia moja au kikundi cho chote cha watu kinachotambuliwa chini
5
ya sheria ya kimila au ambacho kimejiunga kama chama cha Ushirika.• Mtu yeyote ambaye alifunga ndoa na akaachika au ameondoka kijijni kwa kipindi kisichopungua miaka miwili, na mwanandoa mwenzake alikuwa mwanakijiji kabla ya kufunga ndoa na wote ni raia wa Tanzania.• Mtu au Kikundi chochote cha watu ambao kwa kawaida si wakazi wa kijiji, wanaweza kuomba hakimiliki ya kimila ila ni lazima wawe na wadhamini wasiopungua watano ambao ni wanakijiji, na pia ombi/maombi yao yaambatanishwe na tamko lililotiwa sahihi na kushuhudiwa kwamba mwombaji/waombaji wanakusudia kuanzisha makao ya kudumu ndani ya kijiji hicho katika kipindi cha miezi mitatu tangu wapate hakimiliki ya kimila.ZingatiaHalmashauri ya Kijiji itafanya uamuzi juu ya maombi hayo kabla ya kupita siku tisini tangu maombi yalipowasilishwa.Katika kutoa uamuzi kama itoe hakimiliki ya kimila au la, Halmashauri ya Kijiji inatakiwa kuzingatia usawa wa watu wote, kama vile kuyapa uamuzi sawa maombi toka kwa mwanamke au kikundi cha wanawake na yale yanayotoka kwa mwanaume au kikundi cha wanaume. YAANI kutokuwa na ubaguzi wowote dhidi ya mwanamke aliyeomba kupewa hakimiliki ya kimila. (Kifungu cha 23 cha sheria ya ardhi ya vijiji 1999).Uamuzi wowote wa Halmashauri ya Kijiji au chombo chochote kinachoshughulikia migogoro ya ardhi
6
utakuwa batili iwapo uamuzi huo utawanyima wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu haki yao ya kisheria ya kupata hakimiliki ya kimila.Sheria ya ardhi imeweka bayana kuwa ardhi tupu ina thamani na hivyo inaruhusu mmiliki wa ardhi kuuza ardhi ambayo haina maendelezo yoyote. Na pia imempa mamlaka Kamishina wa ardhi kupitisha mauzo ya ardhi isiyokuwa na maendelezo yoyote ilimradi tu mauzo hayo yatakuwa ni baina ya watanzania. Na kwamba mnunuzi anakubaliana na masharti ya umiliki kama inavyotakiwa kisheria. (Kifungu cha 5 cha sheria ya marekebisho ya sheria ya ardhi no. 2 ya 2004).KUHUSU WANANDOA(i) Hakimiliki ya Ardhi Baina ya WanandoaUmiliki wa ardhi wa pamoja unawezekana kabisa. Sheria ya Ardhi namba 4 ya 1999 inaeleza bayana kuwa wanandoa wanaweza kuomba hakimiliki ya ardhi kwa pamoja katika maslahi/mafungu yanayogawanyika au yasiyogawanyika. (Kifungu cha 161 cha sheria ya ardhi 1999).ZingatiaHakimiliki ya ardhi kwa maslahi/mafungu yasiyogawanyika inatolewa kwa wanandoa moja kwa moja. Ila kwa watu ambao sio wanandoa ni lazima kwanza wapate idhini au kibali cha mahakama.Katika umiliki wa pamoja wa aina yoyote ile ni lazima majina ya wamiliki wote yawepo kwenye hakimiliki na kila mmoja awe na nakala ya hakimiliki.(Kifungu 160 cha sheria ya ardhi namba 4, 1999).
7
Hakuna mmiliki anayeruhusiwa kuuza, kugawa, kuhamisha, kubadilisha umiliki au kuweka rehani ardhi ila ni LAZIMA kwanza awashirikishe wamiliki wote na wamiliki hao wote ridhaa zao kwa maandishi. (Kifungu cha 159 cha sheria ya ardhi namba 4 ya 1999). Sheria pia inaruhusu mwanandoa kumiliki ardhi binafsi au kumiliki kwa pamoja ila ni muhimu kuzingatia yafuatayo:• Mwanandoa mmoja anapoomba hakimiliki ya ardhi atatakiwa kueleza bayana kama anachukuwa hakimiliki hiyo kwa ajili yake binafsi au kwa ajili ya familia katika hakimi liki ya pamoja kwa maslahi/mafungu yasiyo gawanyika.• Endapo jambo hili halitawekwa bayana na hakimiliki imechukuliwa kwa umiliki wa pamoja baina ya wanandoa basi, kutakuwepo na dhana ya kuwa wanandoa wote wanamiliki ardhi hiyo kwa maslahi/mafungu yanayogawanyika, na msajili wa hati atatakiwa kuwaandikisha wanandoa hao wamiliki wa pamoja wa maslahi/mafungu yanayogawanyika.• Inapotokea kwamba mwanandoa anamiliki ardhi au nyumba kwa jina lake mwenyewe, na mwanandoa mwenzie amechangia nguvu zake katika kuitunza au kuiendeleza nyumba au ardhi hiyo, mwanandoa aliyechangia ana haki pia (ii) Rehani ya Ardhi au Nyumba ya Ndoa• Sheria ya Ardhi inampa haki mmiliki wa ardhi kwa kujaza fomu maalumu kuweka rehani ardhi au nyumba anayomiliki kwa
8
ajili ya kupata mkopo. Hata hivyo kuweka rehani ardhi au nyumba inayomilikiwa na wanandao NI LAZIMA kwanza ipatikane ridhaa ya mwanandoa/ wanandoa wote wanaoishi au kutumia ardhi hiyo. (Kifungu cha 114 cha sheria ya marekebisho ya ardhi namba 2 ya 2004). Hivyo maombi ya rehani yanatakiwa kujazwa katika fomu maalumu na kuwekwa sahihi na mwanandoa/wanandoa wa mkopaji wanaoishi katika nyumba hiyo.• Ni wajibu wa Mkopeshaji kabla ya kutoa mkopo kuchukua hatua za makusudi za kuthibitisha kwamba mkopaji ana ndoa na kwamba anayetoa ridhaa ni mwanandoa halali wa mkopaji. (Kifungu cha 114(2) cha sheria ya marekebisho ya sheria ya ardhi namba 2 ya 2004).• Rehani ya kimila itafuata taratibu za kimila zinazotumika katika eneo hilo. Hata hivyo kama kuna tatizo lolote juu ya rehani wahusika watatakiwa kutumia huduma ya Baraza la Ardhi la Kijiji. Pamoja na mambo mengine Baraza la Ardhi la Kijiji litatakiwa kuangalia kama rehani ilikuwa na masharti yanayozingatia haki na taratibu za rehani ya kimila katika eneo husika. (Kifungu cha 115 (1) (2) na (3) cha sheria ya marekebisho ya sheria ya ardhi namba 2 ya 2004).• Endapo Mkopeshwaji amekiuka masharti ya mkataba wa rehani Mkopeshaji anatakiwa ampe taarifa (notice) mkopeshwaji kumjulisha ukiukwaji huo na kumtaka arekebishe tatizo hilo. Endapo Mkopeshwaji atashindwa kurekebisha
9
tatizo hilo ndani ya muda wa siku thelathini tangu kutolewa kwa taarifa (notice) hiyo, basi Mkopeshaji anaweza kuuza ardhi au nyumba iliyowekwa rehani. (Kifungu cha 127 cha sheria ya marekebisho ya sheria ya ardhi namba 2 ya 2004).• Ieleweke wazi kwamba hata kama Mkopeshwaji atakuwa amekiuka masharti ya rehani Mkopeshaji haruhusiwi kuchukua na kumiliki ardhi inayotumiwa na Mkopeshwaji kwa ajili ya kilimo au ufugaji au kuingia na kuishi ndani ya nyumba iliyowekwa rehani endapo nyumba hiyo ndiyo makazi ya Mkopeshwaji au ndugu wa Mkopeshwaji. Mkopeshaji anaweza kufanya hivyo tu kwa kupata kibali cha mahakama. (Kifungu cha 130 (5) cha sheria ya marekebisho ya sheria ya ardhi namba 2 ya 2004).Je, ni utaratibu gani ufuatwe endapo mwanandoa
atagundua kwamba ardhi au nyumba ya ndoa imewekwa rehani bila yeye kutoa ridhaa?• Taarifa itolewe haraka iweze kanavyo kwenye Halmashauri ya Kijiji na kwa Afisa Ardhi wa Wilaya aliyeko katika eneo husika, ili taratibu zifanyike za kubatilisha rehani hiyo.• Mwanandoa husika pia anaweza kwenda mahakamani kuomba na kuweka pingamizi la rehani na pia rehani ibatilishwe.
10
Zingatia • Iwapo nyumba au ardhi ya wanandoa ndoa itawekwa rehani bila idhini ya mmoja wa wanandoa anayetumia au kuishi ndani ya nyumba hiyo, reheni hiyo inakuwa batili.• Pia iwapo mwanandoa atataka kuuza, kukodisha, kuweka rehani, au kuhamisha hakimiliki ya ardhi au nyumba ya ndoa kwa mtu mwingine, yule atakayehamishiwa, kuuziwa, kukodishwa au kupewa ana wajibu wa kuhakikisha kama ridhaa ya mwanandoa/wanandoa wengine imetolewa.Ukodishaji na UpangajiMmiliki wa ardhi anaweza kukodisha au kupangisha hakimiliki ya ardhi kwa muda maalum. Lakini ni vyema kujua kwamba muda unaoruhusiwa na sheria wa kukodisha au kupangisha una kikomo chake yaani unaishia siku kumi kabla hakimiliki ya ardhi haijaisha muda wake.Aina za UpangajiZipo aina kuu mbili za upangaji.1. Upangaji wa vipindi.2. Upangaji wa muda maalum. Upangaji wa vipindi ni upangaji ambao hauonyeshi muda maalum wa upangaji. Hivyo upangaji wa aina hii unaweza ukawa wa kipindi cha wiki hadi mwezi hadi mwaka, n.k. (Kifungu cha 79 cha sheria ya ardhi namba 4 ya 1999).
11
Upangaji wa muda maalum ni upangaji wa mwaka mmoja au pungufu. Katika upangaji wa aina hii mkataba wa upangaji waweza kufanyika kwa njia ya mdomo au maandishi. Mkataba huu huainisha masharti na majukumu ya Mpangaji na Mpangishwaji katika suala zima la upangaji. (Kifungu cha 80 cha sheria ya ardhi namba 4 ya 1999).Utaratibu wa kusitisha mkataba wa upangaji ni mpangaji au mpagishaji kutoa taarifa (notice) ya siku thelathini (30) kwa mwenzake kueleza nia hiyo ya kusitisha mkataba wa upangaji. (Kifungu cha 19 cha marekebisho ya sheria sehemu ya nne namba 11 ya 2005). Zingatia Iwapo Mpangaji amekiuka masharti ya mkataba wa upangaji, Mpangishaji anaweza kuchukua hatua zipasazo ili asitishe mkataba wa upangaji. Mahakama katika kujadili na kuamua itoe amri ya kusitisha mkataba wa upangaji au la, pamoja na mambo mengine itaangalia, umri wa mpangaji, hali yake ya kipato, afya, pamoja na idadi ya wanaomtegemea. Hii ina maana kuwa mahakama
itajiuliza maswali mbalimbali. Kwa mfano, je? Mpangaji ana mahali pa kuishi? Je? Mpangaji ana namna nyingine ya kujipatia kipato na mahali pengine
pa kuishi yeye na familia yake au wanaomtegemea?Urejeshaji wa Hakimiliki ya Ardhi• Mtu mwenye hakimiliki ya ardhi anaruhusiwa kurejesha haki hiyo kisheria pale anapoona kwamba haihitaji tena ardhi hiyo au hana uwezo wa kuiendeleza. Mrejeshaji anatakiwa kutuma maombi ya urejeshaji kwa Kamishna wa ardhi au kwa
12
Baraza la Ardhi la Kijiji.• Hata hivyo, sheria inakataza urejeshaji wa ardhi wenye nia ya kumnyima au kumdhulumu mwanandoa au mmiliki mwingine haki yake ya umiliki anayostahili au haki ya kupata maslahi katika ardhi husika. (Kifungu cha 42 na 43 cha sheria ya ardhi namba nne ya 1999).Ushiriki wa Wanawake Katika Masuala Yahusuyo Ardhi.Sheria za Ardhi za mwaka 1999 zimeweka mfumo bora wa utawala ambao unawawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika masuala ya ardhi nakuwakilishwa katika mipango na maamuzi yanayohusu ardhi. Kwenye usuluhishi na utatuzi wa migogoro ya ardhi wanawake pia wanapaswa kushiriki kwenye kamati za usuluhishi katika ngazi mbalimbali kama ifuatavyo:(i) Baraza la Kitaifa la Ushauri la ArdhiBaraza hili linaundwa chini ya kifungu 17 cha sheria ya ardhi namba 4 ya 1999. Baraza hili linatakiwa kuwa na wajumbe wasiopungua saba (7) na wasiozidi kumi na mmoja (11). Wajumbe hawa wanateuliwa na Waziri wa Ardhi. Jukumu kubwa la baraza hili ni kupitia na kuangalia upya masuala ya ardhi na kumshauri waziri juu ya sera ya taifa ya ardhi kwa nia ya kufanya marekebisho na mabadiliko inapobidi, ili kuboresha utekelezaji wa masuala ya ardhi nchini.ZingatiaSheria mmemtaka waziri katika kuteua wajumbe hao azingatie uwiano unaoridhisha baina ya wajumbe wanawake na wanaume.
13
(ii) Kamati ya Uamuzi ya Kijiji.Hii ni kamati ambayo inaweza kuundwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji chini ya kifungu cha 53 cha sheria ya ardhi ya vijiji namba 5 ya 1999, kwa ajili ya kusuluhisha migogoro inayohusiana na mipaka ya ardhi, haki ya njia na maslahi ya wanawake, walemavu, na watu wasiokuwepo kijijini. Kamati hii itaundwa na wajumbe wasiozidi tisa (9), ambapo wajumbe wasiopungua wane (4) wanatakiwa wawe wanawake. Wajumbe wa kamati hii watatumikia kwa kipindi cha miaka mitatu (3) na wataweza kuchaguliwa tena kwa kipindi kingine cha miaka mitatu (3).Kikao halali cha Kamati ya Uamuzi ya Kijiji kinatakiwa kuwa na wajumbe wasiopungua watano (5), ambao wawili (2) kati yao ni lazima wawe wanawake.Mtu yeyote ambaye hakuridhika na uamuzi wa Kamati ya Uamuzi ya Kijiji anaweza kukata rufani dhidi ya uamuzi huo kwenye Baraza la Ardhi la Kijiji ndani ya kipindi cha siku thelathini (30) baada ya kutolewa kwa ZingatiaIli kamati hii iweze kuendelea na mkutano wowote utakaoitishwa ni lazima wajumbe watano wawe wamehudhuria na kati yao wawemo wajumbe wanawake wasipungue wawil(2).(iii) Baraza la Ardhi la Kijiji.Kwa mujibu wa kifungu cha 60 cha Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya 1999 kila kijiji kinatakiwa
14
kuunda Baraza la Ardhi la Kijiji ambalo
litakuwa na kazi ya kusuluhisha na kutatua
migogoro yote ya ardhi kijijini. Baraza la Ardhi
la Kijiji linatakiwa kuwa na wajumbe saba (7)
ambapo watatu (3) kati yao ni lazima wawe
wanawake. Wajumbe wa Baraza la Ardhi la
Kijiji wanateuliwa na Halmashauri ya Kijiji na
kupitishwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji.
Kikao halali cha Baraza la Ardhi la Kijiji
kinatakiwa kiwe na wajumbe wane (4)
ambapo wawili (2) kati yao ni lazima wawe
wanawake.
Baraza la Ardhi la Kijiji linatakiwa kufanya
kazi zake kwa kuzingatia misingi ya kimila ya
usuluhishi pamoja na misingi ya haki.
Mtu yeyote ambaye hakuridhika na uamuzi wa
Baraza la Ardhi la Kijiji anaweza kukata rufani
dhidi ya uamuzi huo kwenye Baraza la Kata.
Mahakama za Utatuzi wa Migogoro ya
Ardhi Nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa sheria za ardhi za mwaka 1999
pamoja na sheria ya Mahakama ya utatuzi wa
migogoro ya Ardhi 2002, mahakama zifuatazo
zimepewa jukumu la kushughulikia migogoro ya
ardhi kuanzia ngazi ya kijiji hadi ngazi ya kitaifa.
15
WITO:
• Wanawake ni watumiaji wakuu wa ardhi hivyo vyombo vinavyohusika na masuala ya
usimamizi na utawala wa ardhi vihakikishe
kuwa wanawake na wanaume
wanashirikishwa ipasavyo katika masuala yahusuyo ardhi.
• Wanawake wahakikishe kuwa
wamezitumia nafasi watakazokuwa nazo kwa kushiriki na kutoa mawazo yao kwa lengo la kuboresha maslahi ya familia zao na taifa kwa ujumla.
MAHAKAMA
YA RUFAA
MAHAKAMA
KUU KITENGO
CHA ARDHI
BARAZA LA ARDHI NA
NYUMBA LA WILAYA
BARAZA LA KATA
BARAZA LA ARDHI LA
KIJIJI

:A S 8: "UKIMPENDA MKEO HAUTADHULUMU HAKI YAKE YA KISHERIA KATIKA ARDHI"
 
Misingi Mikuu ya Sheria Hizi ni:• Ardhi ni mali ya umma na imekabidhiwa kwa Rais kwa niaba ya Watanzania wote.• Raia wote wanawake na wanaume wana haki sawa ya kupata, kumiliki, kutumia na kugawa ardhi.• Milki za ardhi zilizopo ikiwa ni pamoja na milki za kimila zinatambuliwa na kulindwa kisheria.• Ardhi itumike kwa manufaa yanayozingatia maendeleo endelevu.•

Makola kama hiyo ndo misingi ya sheria ya ardhi najiuliza swali moja huwa sipati jibu, kwa nini ni wazawa wachache sana wanamiliki viwanja kwenye maeneo nyeti kama vile sea view, upanga, oysterbay ( ukiachia waliuziwa nyumba za serikali na mashirika). Huoni kuwa hapa ni kinyume cha misingi uliyoitaja? Je ugawaji huu unazingatia maendeleo endelevu kwa wazawa?

Kwa mtazamo wangu ni kuwa "HaKI SAWA YA KUMILIKI" haimaanishi kuathiri taratibu nyingine. Haki siku zote uenda na wajibu. Wajibu huo ni pamoja na kufuata taratibu husika ambazo ni pamoja na kuwa na uwezo wa kugharimia eneo na kuzingatia mipango ya kuhudumia/ kendeleza ardhi husika.

Kuwepo kwa watu wanaomiliki ardhi maeneo ambayo wengine hawawezi kumiliki unasababu nyingi na kubwa zaidi ni Kipato kwani ardhi kama mali ya Taifa, inamilikishwa kwa raia kwa muda maalumu kwa madhumuni ya kuiendeleza tu na sio vinginevyo. Pengine, taratibu zinaweza kuwashindwa wengine kuweza kumiliki ardhi katika maeneo fulani fulani. Hali kadhalika, taratibu hizo hizo zinaweza kupindishwa na watekelezaji wake ili kuwanyima haki wengine kupata umiliki wa ardhi ambayo wengine wanaonekana kuwa na haki juu yake.

Ili kupata ulinganifu, nadhani Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 (Namba 4) na Ile ya Ardhi ya Vijiji 1999 (Na.5) wakati wote zinapaswa kusomwa sambamba na sheria nyingine zinazohusu nazo kama zile zihusuzo ugawaji,usimamizi, na undelezaji wa ardhi kwa maana ya kuzingatia madhumuni. Kwa mfano sheria za Mipango Miji, Sheria za Kilimo, Sheria za Malili, Sheria za Majenzi, Sheria za Serikali za Mitaa (Local Government), Sheria za Maji, Barabara, Wanyamapori, Sheria za Kutwaa Ardhi (Land Acquisation) nk nk. Hizi zinaweza kuathiri pia haki ya mtu kumiliki ardhi kwa njia moja au nyingine.
 
Nimekupata Ngoshwe, lakini, Wananchi tunazidi kuwa wachovu kiuchumi, na hakuna mwelekeo kuwa tunaweza angalau kuinuka kiuchumi kwani hakuna mkakati madhubuti wa serikali wa kutuendeleza, hivyo maeneo hayo tutaendelea kuyasikia tu, sio kwamba misingi wa Ardhi uliotajwa juu utatuondoa wananchi ambao wengi ni walalahoi kwenye ardhi yetu na kutusukuma pembeni mwa miji. kwa nini basi sheria zingine ziweke mgawanyo unaondena na kipato wakati wanajua fika kuwa wazawa hatuwezi kufika huko.
 
Wajua pengine kaka shida ni kukosekana kwa mfumo wa kuwezesha watu wanaopata ardhi kuitumia kwa matumizi yaliyokusudiwa na endelevu. Tofauti na mfumo wa Sheria za Kikoloni ambazo zilikuwa na Mkazo wa kuahakikisha mtu anapewa ardhi kwa kuzingatia uwezo alionao kuiendeleza na sio kwa misingi ya kuhongana au rushwa, na pia ikiwa anashindwa kuitumia kwa madhumuni ananyang'anywa right ot, kwa sasa nakubalina nawe kkuwa hali inatisha kabisa. Kwa mfano, yapo maeneo mengi ambayo yanatolewa kwa madhumuni ambayo hayana maslahi ya Taifa.

Ukienda Wizara ya Ardi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, unaweza kukuta kuwa wao malengo yao zaidi yamejikita katika kugawa tu ardhi kupitia Sheria za Ardhi (Na. 4 & 5) pasipo kunagalia madhumuni na malengo mazima ya kichumi na kijamii. Kwa mfano, mpaka hivi leo, japo tunasema Tanania ni nchi inayotemea KILIMO, hakuna Sheria yeyote ambayo ina ainisha, kulinda na kuweka msisito wa wale wanaopewa ardhi kwa ajili ya kilimo kama ilivyo katika Sekta nyinginezo (Mistu, maliasili, madini, barabara, makazi, wanyama pori nk).
Ukienda kwenye Halmashauri za Wilaya mpaka huko vijijini, wanasisitiza watu walime pasipo hata kujua hiyo ardhi ya kilimo ipo wapi na inatosha kwa kisai gani na itatumika kwa miaka mingapi na italindwaje ili isiweze kutwaliwa kwa madhumuni mengine ikiwemo makazi na shughuli nyingine binafsi za kiuchumi ambazo sio lengo lake.

Kwa mfano ukipita maeneo mengi ya Morogoro au hata Arusha pale Arumeru ambapo watu sasa wanafumua majumba, unaweza kuona jinsi ardhi ilivyokuwa na dhamani kwa maana ya kuwa na uoto wa asili na rutuba ya kuwezesha kilimo. Lakini kwa kuwa anasa zimehamia kwenye kuporomosha majumba, sasa watu wanajitahidi kutwaa ameneo makubwa na kuuza ili waweze kujenga na baada ya muda unaona ardhi ambayo inafaa kwa kilimo inapotea. Sambamaba na hilo, kwa upande wa wanyama, misitu na maliasili nyingine, unaweza kuona pia jinsi sheria zao zilivyokuwa makini na mgfumo wa usimamizi ulivyomadhubuti. Maafisa husika wanaweza kukushuhulikia vilivyo ukikutwa kwenye mbuga ya wanyama aua ukiua mnyama wa porini kuliko ambavyo unaweza kusaidiwa kulipwa fidia iwapo mnyama wa porini akila mazao yako au kukuharibia shamba hivyo kukukoseha kipato.

Kwa mtazamo wangu, kila siku nimekuwa nikiona kuwa tunasheria kali za kulinda maeneo ambayo sio "priductive" na kusahau kujilinda wenyewe (kwa mfano unamlinda zadi mnyama wa porini kwa kumwekea mpaka na askari ili asiuwawe, kuliko kumlinda mkulima kwa kumpatia ardhi ya kutosha na yenye rutuba ya kilimo ambayo ina miundo mbinu yote inayofaa pamoja na wataalamu wa kutosha kumsaidia kuendeleza ardhi hiyo.
Sheria za Ardhi kwa upande mkubwa, zenyewe zimejikita zaidi kutoa na kutwaa ardhi pasipo kuwezesha jinsi ya kuitumia ardhi hiyo kwa malengo endelevu. Kwa mfano, kwa sheria za sasa unakuta kifungu kinasema mtu atakayepewa ardhi akishindwa kuitumia kwa madhumuni yaliyokusudiwa, mamlaka husika inaweza kumnyanganya mtu huyon ardhi. Hata hivyo, ingekuwa vyema kama Wizara au Idara husika ikaangalia pia jinsi gani ya kumwezesha mtu aliyepewa ardhi kwa madhumuni ya shughuli za kiuchumi anaweza kuiendeleza kwa kuweka chombo kitakachokuwa kikipima kila wakati vigezo vya maendeleo katika ardhi na sababu za kuweza kubaini kuwa mhusika ameshindwa. Kwani kwa
wakati wote, haijawahi kutokea kuwa ardhi inayotwaliwa kutokana na mhusika kushindwa kuiendeleza inabakia mikononi mwa Serikali, ikitwaliwa atapewa mtu mwingine ambaye nae anakuwa hata tofauti na yule wa awali na hali inaendelea kuwa mbaya tu.

Usimamizi huo mbovu wa ardhi inayogawiwa kwa wanachi kwa ajili ya madhumuni mbalimbali ndio umepelekea hata maeneo ambayo yangeweza kuwa mifano ya maendeleo kuonekana leo kuwa ni kama jalala la taka labda kutokana na watu kujiamulia matumizi, kugawana hovyo au kuuza na kujenga hovyo hivyo pasipo kuzingatia taratibu za mipango miji.

Kwa mfano, japo Kamisheni ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi ( The National Land Use Planning Commision) imekuwepo kisheria tokea mwaka 1984 na pia kurekebishwa upya kwa madhumuni ya kuijengea uwezo zaidi katika utendaji kupitia Sheria mpya ya mwaka 2007 ( The Land Use Planning Act No. 6 of 2007 ), inaonekana kuwa bado kumekuwa na masukumo mdogo sana kati ya Kamisheni hiyo, Wizara mama ya Ardhi na hata Wizara au Idara nyingine za Serikali hasa katika kuhakikisha uwepo wa mipango endelevu ya matumizi ya ardhi kwa madhumuni mbalimbali katika nagzi zote. Cha ajabu unaweza kukuta kuwa Kamisheni hii inajikita zaidi kwenye kuhamasisha uwekezaji toka nje kwa kushirikiana na TIC ili hali hakuna maeneo ambayo hakika tunaweza kusema kuwa hanafaa kutumia kwa uwekezajia wa muda mrefu ukiacha yale mabayo yamekuwa yakitumika kwa mazoea na wakulima wetu na ambayo akija mwelezaji wa nje wakulima wanaambiwa wapishe ili kuruhusu uwekezaji nao wanalipwa fidia kiduchu ili wahamie sehemu nyingine.

Kwa kuwa kizazi kinazidi kuongezeka, na mfumo tunaoenda nao sasa ni wa kuwahi na kugawiana kienyeji tu maeneo yaliyowazi pasipo hata kuweka utaratibu wa kuyaendeleza yale tuliyonayo na tuliyokwisha yatumia toka zamani ili yazidi kutunza hadhi yake, ikiwa pia tunahimiza wawekezaji toka nje kuja kuwekeza katika maeneo ambayo tayrai yanaonekana yanafaa kwa kilimo na shughuli nyingine za kiuchumi ili hali tukiwaondoa wazawa katika maeneo husika ili wakatafute pengine (bila kuwaandalia), itafika wakati tutapoteza kabisa ardhi inayofaa kwa shughuli za kiuchumi na pia makazi. Katika kipindi hicho sasa hata hii amani tunayojivunia haitakuwepo tena kama yale ya Zimbabwe, Afrika ya Kusini na kwingineko ambapo ardhi ilionekana kuwa kubwa siku za nyuma sasa ni kama imeisha na wazawa hawana kwa kwenda.
 
Ukitilia maanani kuwa viongozi na watendaji wetu wanafikiria kwa mwaka mmoja bila kujali mipango ya miaka 10 au 20 ijayo unadhani pamoja na sheria hizo nzuri tutakuwa wapi, tutalima wapi, tutafuga wapi ukiangalia sana post yako ya juu na kuitafakari ina maana tunatayarishwa kuwa watu wa supermarket na kuyafanya masoko yetu traditional kwisha. Zamani bagamoyo ilikuwa inaproduce mpunga na mihogo tosha sasa hivi maeneo hayo yote wametoa viwanja.

Fikiria Songwe, mbalizi ( mbeya ) mawiti (tabora), kigoma nyuma ya magereza kule, kimara na mbezi ( DSM ) Maili mbili, msalato, ntyuka ( dodoma) yote haya yalikuwa maeneo ya kilimo lakini sasa ndo kama ulivyosema wazawa wamenyang'anywa na halamashauri na kufanya viwanja . Nadhani baada ya miaka 10 situation itakua mbaya sana. Katikati ya miji tunafukuzwa pembeni ya mji tunaondolewa what next?

A disaster in the coming.
 
Balaa tupu mzee. Ila I always believe kuwa wapo watu ambao wana dhamana katika ofisi zao ambao hakika ndio wanaolitia mkenge taifa hili. Hao ni pamoja na wale wanaoitwa "Maafisa MIpango" (ARDHI, UCHUMI, MIJI, WATENDAJI,) nk. Hebu fikiria eno kama lile la pale Tebgeru ambapo zamani enzi za Mwalimu aliona panafaa kwa shughuli za kilimo na utafiti wa kilimo (upande wa kushoto kama unakwenda Arusha Mjini kuna chuo cha Kilimo na Utafiti vya muda Mrefu) eti leo pale wamejenda Chuo Kikuu na pana kuja hoteli za Kitalii, kuna magereji na shughuli hivyo hovyo nje ya Kilimo.
Huko Badamoyo mzee, sasa watu wanachukua maeneo makubwa ili wajenge shule, mahoteli nk. Kule Mbalizi, Kapunga-huko Mbalali, Kule Songea, RUkwa, Iringa na maeneo mengine mazuri tuliyoona yanafaa kwa kilimo sasa yanakwisha. Mbali ya kupoteza rutuba kutokana na matumizi ya muda mrefu ikiwemo mbolea za viwandani, hayo maeneo sasa watu wanayabadili kuwa ya makazi kama si kuuza kwa shughuli nje ya Kilimo. Kauli Mbiu zetu kama hayo ma KILIMO KWANZA haziendani na hali halisi kabisa.

Kwa wenzetu Ulaya kwa mfano, wamekuwa na akili ya kulinda ardhi kutokana na matumizi kwa kuwa waliamini toka zamani kuwa ardhi ni uoto wa asili ambao unapotea. Maeneo ya Kilimo, Makazi, Viwanda, na mengine ya Hifadhi tayari yametengwa. Mtu huwezi kuingilia huo utaratibu uliowekwa. Ukitaka kufanya jambo la maendeleo suala la "Planning Consent/Approval" ni nyeti. Huwezi kurusha au kutoa rushwa. Ukitaka kumiliki ardhi binafsi asa utaratibu uliopo ni vigumu sana kuupindisha kabla haijabainika (kwa kesi chache sana).

Kwetu hali imebadilika kabisa. Wapo watu wanamiliki maeneo makubwa sana sasa sehemu mbalimbali ambapo hawajaendeleza kabisa lakini hawashughulikiwi na mamlaka husika. Kampeni zinakuwa kuhamisha toka kwa wazawa ardhi waliyoendeeza kuliko kutafuta ile iliyowazi na kuiwekea misingi ya kuiendeleza ikiwemo miundo mbinu. Viongozi wetu pengine utafikiri hawajifunzi kutoka kwa wenzao katika nchi zile wanazotembelea...
 
watu wengi wanalaumu " usawa katika kugawana viwanja" AMINI NAWAAMBIENI watanzania hawajui thamani ya "Surveyed land" utakumbuka wakati wa mradi wa viwanja 20000 katika jijiji la dar, viwanja bunju ilikuwa mpaka miliono moja. lakini watu kwa kuwa manzese, kimara,makongo juu, kulikuwa na viwanja mpaka vya laki mbili kwa wakati huo. kutokana na watu kutojua thamani ya ardhi iliyopimwa wataaalamu wa wizara Walikopa fedha benki wengine waliweka rehani nyumba zao . na kumudu kununua viwanja mpaka 20 kwa mtu mmoja. wakati huo viwanja hivyo vilikuwa vinauzwa kama nguo sokoni au nyanya sokoni. "unafedha unalipia unapewa kiwanja. lakini watu wakapuuza mpaka baadae vinaishi na wanashtuka, baada ya kuona wengine walionunua kiwanja milioni moja wanauza milioni ishirini. kwa hiyo NGOSWE AMINI NAKWAMBIA WATANZANIA WANAJUA KULALAMIKA LAKINI, HUWA WANAKUMBUKA SHUKA ASUBUHI.
 
Kwa mtazamo wangu ni kuwa "HaKI SAWA YA KUMILIKI" haimaanishi kuathiri taratibu nyingine. Haki siku zote uenda na wajibu. Wajibu huo ni pamoja na kufuata taratibu husika ambazo ni pamoja na kuwa na uwezo wa kugharimia eneo na kuzingatia mipango ya kuhudumia/ kendeleza ardhi husika.

Kuwepo kwa watu wanaomiliki ardhi maeneo ambayo wengine hawawezi kumiliki unasababu nyingi na kubwa zaidi ni Kipato kwani ardhi kama mali ya Taifa, inamilikishwa kwa raia kwa muda maalumu kwa madhumuni ya kuiendeleza tu na sio vinginevyo. Pengine, taratibu zinaweza kuwashindwa wengine kuweza kumiliki ardhi katika maeneo fulani fulani. Hali kadhalika, taratibu hizo hizo zinaweza kupindishwa na watekelezaji wake ili kuwanyima haki wengine kupata umiliki wa ardhi ambayo wengine wanaonekana kuwa na haki juu yake.

Ili kupata ulinganifu, nadhani Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 (Namba 4) na Ile ya Ardhi ya Vijiji 1999 (Na.5) wakati wote zinapaswa kusomwa sambamba na sheria nyingine zinazohusu nazo kama zile zihusuzo ugawaji,usimamizi, na undelezaji wa ardhi kwa maana ya kuzingatia madhumuni. Kwa mfano sheria za Mipango Miji, Sheria za Kilimo, Sheria za Malili, Sheria za Majenzi, Sheria za Serikali za Mitaa (Local Government), Sheria za Maji, Barabara, Wanyamapori, Sheria za Kutwaa Ardhi (Land Acquisation) nk nk. Hizi zinaweza kuathiri pia haki ya mtu kumiliki ardhi kwa njia moja au nyingine.

Ngoshwe, naomba ushauri na kuelimishwa . Mtu aliyenunua ardhi/kiwanja toka kwa mtu binafsi ambacho hakijapimwa na kiko mjini (for that matter nje ya mji sehemu ambayo haijapimwa) analindwa vipi umiliki wa eneo lake na sheria ulizozxitaja hapo juu
 
Kulingana na Sheria ya Ardhi Na.5 ya mwaka 1999, ardhi ya Tanzania ipo katika makundi matatu • Ardhi ya Kijiji (Village Land) • Ardhi ya Hifadhi (Reserved Land) na • Ardhi ya Jumla (General Land) 2.Aina za miliki za ardhi Kuna aina mbili za kumiliki ardhi zina- zotambulika kisheria:
•Miliki ya kupewa na Serikali (Granted Right of Occupancy)
•Miliki ya Kimila (Customary Right of Occupancy)

Kwenye Sheria ya Ardhi Na. 4. kuna Makundi mawili ya Ardhi ya jumla ambayo ni Ardhi iliyopimwa na Ardhi isiyopimwa.
Ardhi iliyopimwa ndio inayoweza kutolewa Hatmiliki na kisheria usimamiwa na Kamishna wa Ardhi. Ardhi isiyopimwa inatambulika lakini kwa maana ya umiliki. kwenye Ardhi hiyo ana haki sawa Kabisa na Yule anayemiliki Ardhi iliyopimwa. kinachotakiwa ni kuthibitisha tu umiliki labda kimila au kutokana na Mkataba wa Mauziano ya Ardhi na mtu aliyemiliki Ardhi hiyo kimila au vinginevyo. Elewa kuwa ili kupata Hatimiliki yaani kumiliki Ardhi iliyopimwa, kwa Kawaida maombi ufanyika na mmiliki wa Ardhi isiyopimwa.
Hivyo, kisheria inatambulika hiyo Ardhi isiyopimwa. Kwenye sheria ya Mipango Miji ya Mwaka 2007, Halmashauri za Wilaya zinawajibu wa kuandaa Mipango ya maendeleo ya Ardhi hata kwenye Ardhi isiyopimwa.
 
Nakushukuru sana Ngoswe. Nimepata mwanga mkubwa sana. Swali la mwisho (ikiwezekana): Mipango miji ikiweka mipango ya maendeleo katika ardhi yangu kama nilivyoainisha hapo kwenye swali la kwanza, haki zangu ni zipi. Kwa mfano wanataka kuichukua kuweka wanavyovijua wao. Haki zangu zinalindwaje katika kutwaa eneo langu. Kumekuwa na mgogoro wa Tibaijuka na wakazi wa kigamboni kuwa sheria ya mipango miji, 2007 haikufuatwa katika dhana nzima ya ujenzi wa mji wa kigamboni (unaotarajiwa) kutwaa ardhi yao.
 
Kwa kujibu wa sheria za Ardhi tajwa, Ardhi yote ni Mali ya umma chini ya dhamana ya Rais. ila mwananchi hupewa Ardhi kutumia tu kwa muda Maalumu kwa shughuli za maendeleo ikiwemo makazi nk. Iwapo Ardhi yako imetwaliwa kwa shughuli yeyote na mamlaka ya Serikali, kwa Kawaida wewe kama mmiliki wa Ardhi hiyo unachoweza kudai ni staili yako ya fidia.

Kwa ufupi "fidia ya ardhi" ni gharama ambazo mmiliki halali wa ardhi hulipwa kwa kuzingatia haki zake juu ya ardhi husika, yaani; thamani ya ardhi, maendelezo katika ardhi husika na maslahi mengine juu ya ardhi kwa mmiliki.Endapo mwananchi ambaye eneo lake linachukuliwa kwa ajili ya upanuzi wa barabara, ni haki yake ya msingi kushiriki katika hatua zote ikiwa ni pamoja na kupewa fidia kwa mujibu wa kifungu cha 3(g) cha sheria za ardhi na.4 na na.5, 1999.
Utaratibu unaofanyika ni serikali kushirikisha wananchi katika eneo husika juu ya maeneo yao pamoja na hatua au taratibu mbalimbali zitakazofanyika au kutekelezwa na wamiliki au watendaji wa serikali. Ukaguzi wa maeneo ya wamiliki na tathmini ni moja wapo ya taratibu za awali katika utambuzi na utoaji wa fidia ya ardhi.

Masuala ya utoaji wa fidia nchini Tanzania yamekuwa hayazingatii katiba ya nchi,sera,sheria, kanuni za ardhi na maslahi ya wamiliki. Hii ni kutokana na manung'uniko ya wananchi wanaohamishwa katika maeneo yao kulipwa viwango vidogo vya fedha kama fidia. Vilio vya wananchi vimekuwa vikisikika katika vyombo mbalimbali vya habari na hata kesi mbalimbali kufunguliwa katika Mahakama za ardhi nchini kuashiria wananchi kutoridhika na michakato ya fidia inayofanyika katika maeneo yao.
Ardhi tupu
Msingi wa kukadiria thamani ya ardhi yoyote na uboreshaji kwa ajili ya ulipaji wa fidia ni thamani ya ardhi hiyo katika soko
Maendelezo katika ardhi na gharama za kuliendeleza eneo
Maendelezo yanayofanyika katika ardhi kama vile majengo na mazao yanatakiwa kulipwa kwa mmiliki wa ardhi kama gharama halali na halisi alizotumia kufanya maendelezo katika ardhi husika. Kwa kawaida kila mwaka serikali imekuwa ikitoa viwango vya majengo na mazao mbalimbali ambayo kiuhalisia wahanga wengi wamekuwa wakilalamikia kuwa sio stahili za gharama ambazo wametumia katika kuendeleza ardhi zao

Ardhi mbadala
Ni dhahiri kwamba milki ya mtu inapoingiliwa , mabadiliko ya kimaisha lazma yatatokea. Mathalani wahanga wengi ambao wamekuwa wakiishi katika maeneo yao kwa muda mrefu. Kwa sehemu kubwa wanapohamishwa pasipo kupatiwa ardhi mbadala, matokeo yake ni kuwafanya waishi maisha ya kutanganga katika nchi yao. Ni haki yao kupatiwa ardhi maeneo mengine na ardhi hiyo iwe imepimwa ili kuongeza uhakika wa ardhi husika na pasipo kufikwa na bomoabomoa nyingine au kuhamishwa.
Posho ya usumbufu
Itakadiriwa kwa kuzidisha thamani ya ardhi mara wastani wa asilimia ya riba inayotolewa na benki za kibiashara kwa akiba ya muda maalum ya miezi kumi na miwili wakati wa upoteza ardhi
Posho ya usafiri
Itakuwa gharama halisi ya kusafirisha tani kumi na mbili za mizigo kwa reli au barabara(kutegemea njia ipi ya gharama nafuu) hadi umbali usiozidi kilometa 20 kutoka mahali pa kuondoshwa
 Riba

Riba kwenye fidia yoyote italipwa na serikali kuu au mamlaka ya serikali ya mtaa pale tu ambapo malipo ya fidia hayakulipwa kwa wakati. "kulipwa kwa wakati" maana yake ni kulipa fidia katika kipindi cha miezi 6 baada ya ardhi inayuhusika kutwaliwa au hakimiliki kubatilishwa.Endapo kiwango cha fidia hakilipwi miezi 6 baada ya ardhi kutwaliwa au hakimiliki kubatilishwa riba italipwa kwa wastani wa asilimia ya riba inayolipwa na benki za kibiashara kwenye akiba za muda maalum hadi fidia itakapolipwa
Kupoteza faida
Faida halisi kwa mwezi kwa biashara inayoendeshwa kwenye ardhi itakadiriwa na kuzidishwa mara miezi 36 ili kufikia kiwango cha malipo ya faida inayopotea.
 
Watanzania si walalamishi ila maisha yao ndio malalamishi, ni mtanzania yupi anaeweza kupata milioni moja keshi? kazi za jungu jiko hazina hata mdhamana benki!
 
Back
Top Bottom