uko juu sana.nakupa zoezi la kukokoto iq ya nape mnauye!Mental age/Umri wa Akili hupimwa kwa uwezo wa kiutendaji wa ubongo wa mtu. Kama mtu wa miaka 15 anaweza kufikiri, kutatua tatizo na kutenda kazi ambayo ingefanywa na mtu wa miaka 20 basi Umri wake wa akili/ Mental age ni miaka 20 na Umri wake wa kuzaliwa/ Chronological age ni miaka 15. Kiurahisi zaidi mtoto wa darasa la kwanza mwenye umri wa miaka 7 (chronological age) akipewa hesabu za mtoto wa darasa la tatu mwenye miaka 9 na akaziweza vizuri basi mtoto huyu wa miaka 7 atapewa daraja la Umri wa akili/mental age ya miaka 9. Hivyo Ukichukua Mental age (Umri wa akili) ukagawa kwa Umri wa Kuzaliwa (Chronological age) kisha ukazidisha kwa 100 jibu lako litakuwa kati ya makundi haya hapa chini: Jipime
Grade Range Percent
Genius/Kipaji maalumu/Uwezo usio wa kawaida:144 >.
Gifted/Uwezo wa juu sana:130-144.
Above average/Uwezo wa juu: 115-129.
Higher average/Wastani: 100-114.
Lower average/Wastani wa chini: 85-99.
Below average/uwezo duni: 70-84
Borderline low/Taahira kiasi: 55-69.
Low/mtindio wa ubongo <55