Unajua historia ya bendera ya taifa lako tangu 1885?

Mmm mbona tofauti kubwa sana, sio tu kwenye rangi nyeusi bali pia hicho kijani sasa kimefanana zaidi na kile cha ccm, wakati bendera ya zamani haiko hivyo. Haya ni makosa kweli ya mtengenezaji au kuna maagizo maalum kutoka lumumba???
 
Halafu kila mlingoti walioweka bendera wameweka na antena wakijifanya ni kwa ajili ya bendera nyingine....
 
Kiuhalisia kuna mwonekano tofauti kiasi fulani. Hivi ukubwa wa nguo iliyotumika kutenengena bendera hauwezi kuathiri vipimo vya muonekano wa hizo rangi? kuna sheria inaitwa 'National Flag and Coat of Arms Act' kwa ajili ya kulinda hizo nembo au vitambulisho vya taifa.
 
kwani bendera nayo inahusika kwenye 'uandikaji upya' wa historia ya uhuru na taifa!?
Nadhani historia itakuwa imeandikwa upya kuwa Rais Obama alipotembelea Tanzania; Tanzania imebadilisha Bendera na kufanya muonekano wa bendera ya Taifa ya sasa kuwa tofauti na ya zamani ili kuingia kwenye kumbukumbu kuwa ndilo Taifa pekee lililo wahi kubadilisha Bendera yake kwa ajili ya Ugeni wa rais wa nchi nyingine!
 
Ujio wa Rais wa Marekani unaweza kubaki kuwa ni kumbukumbu kubwa kwetu kama nilichokiona jana, yaani kubadilika kwa muonekano wa Bendera ya Taifa; kutakuwa kumesababishwa na ujio wa Rais Barack Obama!!

Barabara ya Julius Nyerere inayotoka Uwanja wa Ndege atakapopita Rais huyo kumepambwa bendera zinazofanana fanana na Baendera yetu ya Taifa la Tanzania niliyoizoea.

Naomba Watalaam wa mambo ya uraia na wazalendo wa nchi hii, mnijulishe kilichotokea mpaka bendera ikibadilishwa au ni kitu gani kinacho sababisha bendera ibadilishwe!

Naomba mnijuze ni chombo gani chenye mamlaka ya kubadilisha bendera ya taifa na hatua zipi zinazofuatwa mpaka Bendera ikabadilishwa!

Nilicho kiona kwenye bendera ya sasa ni kuufanya mchirizi mweusi unaokatiza kutoka ncha moja kwenda nyingine kufanywa mkubwa sana na kuifanya rangi hiyo kuwa dorminant kwenye bendera yetu, kinyume na Bendera ya zamani.

Siku zote huwa naamini kuwa Bendera ya Taifa ni tunu na Alama yetu ambayo ina vipimo halisi na haiwezi kuwa inachezewa chezewa!

Kama kuna mtu alipewa tenda ya kutengeneza bendera za Taifa kwa ajili ya ujio wa Obama na badala yake akatuletea bendera iliyobadilishwa bila kufuata utaratibu wa kubadilisha Bendera ya Taifa; Naomba asilipwe na achukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu.

Maskauti wa Nchi wa sasa, mnaona kama mambo yako sawa na bendera yetu?

Hilo nalo neno, kwani umeleta kitu "so unique if not peculiar". naamini serikali yetu ni tulivuu na sikivu, italifanyia kazi jambo hili.
 
Tatizo hapa kwetu kila jambo linafanyika mradi liende.
Inaelekea mtu kajipa tenda ya kushona bendera za Taifa nyingi kwa ajili ya ugeni huu, bila kuzingatia vigezo kadhaa.
Upatikanaji wa vitambaa sahihi (authentic) vyenye rangi inayokubalika (shade). Kwa kuwa rangi zina 'shades' tofauti, mfano kijani, bluu, hata njano zina shades tofauti. Pia upana wa rangi ya njano haukutiliwa maanani, na pia alitakiwa atafutwe mtu ambaye ataleta vitambaa visivyochuja rangi pindi mvua ikinyesha ama bendera hizo zikifuliwa (sijui kama huwa zinafuliwa). Lakini kwenye Tanzania yetu ambayo serikali imejaa mafisadi, tunaingia aibu na wao wamekaa kwenye viyoyozi wakisema 'who cares?'
 
Labda huu mjadala ungenoga kama tungelikuwa na vielelezo vyenye kuonesha kipimo sahihi cha uwiano wa upana au ujazo wa kila rangi.
La sivyo itakuwa ngumu kudhania tu kuwa hiyo bendera ina makosa.
 
Hii ni kwasababu ya kukosa umakini kwa aliyepewa tenda.

Mkuu aliyempa tenda ndiye ana matatizo makubwa zaidi!

Alitakiwa aweke proper specifications kwenye tenda pamoja na sampuli kama kungekuwa na ulazima.

Pia wakati wa kuzipokea alitakiwa akague na kujiridhisha kuwa ziko sawa.

Inaelekea haya hayakufanyika, vinginevyo hawangepokea bendera ambazo haziwiani na bendera halisi.
 
Inaelekea wengi tunaochangia maada hii tunakubaliana kuwa kuna mabadiliko ya/kwenye Bendera ya Taifa!!! Lakini hatujajadili iwapo mabadiliko haya yameshababishwa na ujio wa Obama au yalifanyika kwa kufuata taratibu zilizoko za kubadili bendera ya Taifa au ilikuwa ni makosa ya bahati mbaya au ni uzembe tu, uliofanywa na ofisi ya Waziri Mkuu ambao ndio wanao wajibika na uhifadhi wa Bendera ya Taifa!
Kama mabadiliko haya yamefanyika kwa makosa, ni vema Ofisi hii iombe radhi Watanzania kwa makosa yaliyofanyika, halafu maofisa waliohusika moja kwa moja na upatikanaji wa bendera hiyo wawajibishwe, pia mtu aliyepata tenda hiyo asilipwe fedhe zozote mpaka atakapo leta bendera sahihi.
 
Inaelekea wengi tunaochangia maada hii tunakubaliana kuwa kuna mabadiliko ya/kwenye Bendera ya Taifa!!! Lakini hatujajadili iwapo mabadiliko haya yameshababishwa na ujio wa Obama au yalifanyika kwa kufuata taratibu zilizoko za kubadili bendera ya Taifa au ilikuwa ni makosa ya bahati mbaya au ni uzembe tu, uliofanywa na ofisi ya Waziri Mkuu ambao ndio wanao wajibika na uhifadhi wa Bendera ya Taifa!
Kama mabadiliko haya yamefanyika kwa makosa, ni vema Ofisi hii iombe radhi Watanzania kwa makosa yaliyofanyika, halafu maofisa waliohusika moja kwa moja na upatikanaji wa bendera hiyo wawajibishwe, pia mtu aliyepata tenda hiyo asilipwe fedhe zozote mpaka atakapo leta bendera sahihi.

Nitafutieni ka-sheria kalikovunjwa.... ili muhusika (ofisi ya Mpigaji Mkuu)..... ACHAPWE NA APIGWE TU.... Maana tumechoka na watu kujipa tenda ni kufanya fanya vitu vya ovyo ovyo....
 
mkuu upo sahhi tofauti ni kubwa sana hii ndo tanzania bana tuna ujuzi finyu less serious wajuaji tunabebana
 
mmmhhhh! mbona kama wamechanganya na ya nyinyiem?

unajua watanzania kwa kupiga dill aliyepewa tenda ameomba zilizobaki SA akaongezea blue basi akawa amenaliza kazi rais wetu wanakuibia hata ww lakini sishangai kwa wat
 
Back
Top Bottom