Unajithamanishaje? ...Unathaminiwa?

Ni kweli kujithamini au kuthamini wengine kunatokana na kujitambua wewe binafsi. Na hili kujitambua wewe binafsi inabidi ujue tamaduni za jamii inayokuzunguka iwe kazini, familia au hata Pub. Kwa kujua hilo ndio utaweza kushusha au kupandisha vigezo kutokana na maisha ya jamii hiyo.

Mara nyingi ukijishusha kwa kiasi fulani utakuwa na uwezo mzuri wa kujitambua na kujichaganya na kukubalika na jamii sehemu yeyote hile..hata pale nyumbani kwako jaribu kujishusha na kuthamini kazi za House girl au Houseboy wako..jaribu kumfanya kama mdogo wako na uone matokeo yake.... Pia tukumbuke hakuna kipimo cha thamani..sio cheo, wala hela, wala mavazi, wala mikogo..wala kutoa misaada..vyote hivyo havisaidii kupandisha thamani yako ..Thamani ni kukubalika..na kuheshimika kwa kujishusha kwako albeit ilibidi uwe juu... Hata walevi wanathamani na kuthaminiwa wakikutana kwenye jamii za walevi wenzao..ni utamaduni na vigezo vyao. Hapo utaona thamani inakuja yenyewe na wala sio wewe unayeiweka au kuilazimisha... kikubwa.. Jitambue..jishushe ili wale wanaokuzunguka ndio wakupandishe..
kweli kabisa, mtu yupoyupo tu, analoliongea kila siku watu hawamwelewi, pumbapumba tu, na bado anataka watu wamthamini fo who she/he is haoni kama inabidi atumie nguvu ya ziada ili apate thaminiwa na jamii?
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Kweli kabisa Tulizo, ila sie waafrica hapo bold huwa ngumu sana, wengi wetu kujishusha ili tupate faida fulani hatuwezi, natokeo yake kila mtu kichwa juu hata kwenye jambo anaona kabisa anatakiwa aje chini lakini hakuna

Shantel labda hutaniamini nikikwambia sisi wafrika ni wazuri kwa hilo..ila kama tukilinganishwa na wazungu.. Mara nyingi ukifanya kazi kwa kujichanganya na hawa watani zetu weupe.. waafrika huwa tunakubakika sana na wazawa..kwani mara nyingi tunajishusha nakuthamini tamaduni za wazawa na wao.. Matokeo yake kazi zinaenda barabara na wazungu wanashangaa mfupa uliowashinda sisi waswahili tumeuweza..Siri kubwa ni kumthamini mtu hata kama ni wewe ndiye unampa msaada..
 
Kwa nini najithamini? ni hivi, dunia nzima kuna watu zaidi ya bn. ngapi? and who will give a damn about me other than myself??!..nobody!

Vyovyote ulivyo lazima mtu ujithamini, ukisubiri kuthaminiwa itakula kwako. yes, kuna muda mwingine mtu ukikutana na matatizo unaweza kujiona huna thamani lakini maisha ni pande zote na ukifahamu hili unatakiwa kutatua matatizo kwa kadiri ya uwezo wako.

Sijui aisee, najithamini na kujijali sana katika haya maisha!!..

...Spot on BJ!...maswahiba ya uthaminishwaji thamani ya moyo hayo,...lol,
fragile_handle_with_care_package_shipping_label_sticker-p217906670256084704tdcj_125.jpg

 

Dah, hapo penye wekundu, mbona sie wengine ni wepesi kung'amua nimechemsha?
Kumbe kuna wenzangu hutumia muda mrefu kugundua 'wana bore?'....well well well!

...kuna wengine wanawatishia wenzao nyau hata hapa JF na u Snr/Premium Member.
Yale yale, ha ha ha...Nimekusoma kituo kwa kituo.
Ashadii, asante kwa mchango wako.




Hivi mbu kwa post unazotoa hivi nani in his/her right mind would think kua hujithamini...
Kwanza kabisa kama you know you are hungry with a tired brain haitakiwi hata kugusa thread yako!
Amini usiamini kuna watu wanachukua mda mrefu kutambua (na hao ni wenye bahati...)
for others it is for ever... esp kama wahusika hufanya kwa kuuma na kupuliza... kuku
degrade in a way you think it is ok (and that what was suggested was your idea...)

Na hilo la JF kua kuna Premium Members wengine wana mikwara it is so true..
and if you let them.... tunarudi hapa hapa katika huu uzi na the way it applies...
 

Shantel umeandika jambo la maana sana. Kujithaminisha mwenyewe ni jambo la busara sana. Bahati mbaya, ni wachache mno wenye uwezo wa kulitambua hilo. Tatizo linaanzia kwenye maamuzi ya mtu na mtu. Ukishajikubalisha Mwanadamu mwingine akuamulie maamuzi yako, naamini taratibu utaanza kupoteza uwezo na thamani ya maamuzi yako. Hilo litapelekea kuanza kupoteza uwezo was kujiamini (Confidence & Self esteem)

Mfano;
Ni rahisi sana kwenye mapenzi mtu akakujengea hisia hakuna mwingine kuliko wewe. Hakuna ubaya katika kulitambua hilo, ubaya ni pale nawe utaposhindwa kujithaminisha kiukweli uwe mbora kuliko mwingine.
Kimtazamo wangu, kila mmoja wetu amejaaliwa mazuri fulani ambayo yanamtofautisha na mwingine. Mtu atapokupendea kwa mazuri yako, wapaswa nawe kuyajenga na yale ulokuwa na upungufu nayo ili uweze kujikamilisha japo kwa asilimia kubwa zaidi.

Lakini vile vile, ...kuna watu ambao ni mahodari kuwakatisha tamaa wenzao. Watakuja na hadithi za, 'hujapendeza!' 'hujaelimika!' 'huna hoja!' 'hujui hili na lile' nk nk nk.... Ikiwa nawe ni mdhaifu, uka ya accomodate mawazo ya nje yakutawale maamuzi yako, jijue unajichimbia kaburi la kutaka kum- please mtu, ilhali unajipotezea Values zako.

Negative comments ni Challenges za kukupima uwezo wako, "thamani yako!"




Spot on ndugu yangu!...kujikweza kunatuharibia sana ndugu yangu. Tatizo la kujikweza hapafu watu wakaja kubaini mapungufu yako, kunawapelekea wengi kupatwa na msongo mkubwa wa mawazo, na hata wengine kujionea bora wakatishe maisha kuliko aibu watayoipata.
Mbu, pia ukiona watu wanakuzongazonga kwa kukukashifu sana pasipo na tija ,na kukutaja kwa sana ujue tu thamani yako iko juu mbele yao ila wao tu hawajijui kama wanakuthaminisha ki namna fulani
 
Mwe mambo mengine yanaweza kutufanya thamani zetu kwa wenzi wewtu zikashuka.... Kama JF LoL maana twawezapewa talaka ati! Mbu umeoa?
 
Mwe mambo mengine yanaweza kutufanya thamani zetu kwa wenzi wewtu zikashuka.... Kama JF LoL maana twawezapewa talaka ati! Mbu umeoa?

mnnhh, nini tena? LOL...mbu is engaged to 'Liberian Girl.'
 
Likwanda HB yoyote hajiamini ana wasi wasi na hajiamini kuwa amekamilika. So kila mara ana wasi wasi kuwa kuna tatizo au hana uhakika akitoa ushauri utasikika
HB ni mtu wa namna gani?ufafanuz plse...!
 
mnnhh, nini tena? LOL...mbu is engaged to 'Liberian Girl.'
Mwenzangu nlikuwa namaanisha angalia saa sita usiku wakati mwenzio anategemea uwe pembeni yake mwapeana joto, mie ninapost JF si najishushia thamani kwake LOL! Nahata kama kaniomba nisiingie JF kwa kuwa na usiku sana, mwanamke mimi sijatii! Si najiandikia talaka kabisa hapa?Hongera mwaya, msalimie Liberian gal
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Garmi swali zuri sana
Hb ni mwanaume ambaye anajiona ni mzuri wa sura twaweza sema kwa kifupi ni kati ya wale watu wanajiona au wanaosifiwa wana sura nzuri. Haijalishi kuwa ni kweli wana sura nzuri ila washaamishwa hivyo kuwa wana sura nzuri na huwezi wapinga kwa hilo. So muda wote wao wanahakikisha kuwa wanaziweka sura zao zioekane the same so hawajiamini hawana uhakika kuwa muonekano wao ni kweli unawafanya wawe hivyo au wakiwa kwenye mazingira halisi kama kweli wanaonekana hivyo.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Aksante Mr. Rocky kwa ufafanuzi makini! Umenikumbusha kuna dada mmoja alikuwa kapendwa na HB mmoja yeye akamtolea nje akisema hawezikuwa na mwanaume mzuri kuliko yeye!!! .... Huyu dada hakuwa anaijua thamani yake!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Mwanajamiione ni noma sana unakuta mwanaume mzuri kukiko mwanamke wake na anajipodoa kuloko mwanamke wake hapo sasa nani atakuwa mwanamke. Na hb huwa hawajiamini. Wana kasumba moja ya kutaka waonekane hata kama wanafanya upumbavu au kitu cha kijinga. Wanataka jamii iwatambue kuwa ni wazuri wa sura. Sasa kwenye kutaka waonekane wanajikuta wanafanya mambo ya kijinga au show off za kijinga. Ila sio hb wote wako hivyo. Kuna waliokwishajitambua na wanafanya mambo kulingana na hali halisi na wanafanya mambo kwa hali halisi sio kwa sura zao. Washajitambua kuwa wana sura nzuri na kujithamini na wanajichanganya na kufanya kile jamii inachomtaka afanye.
 
Wanasema wewe una thamani gani bila title yako?????

Mfano kuna watu ukiondoa title wanazoshikilia mfano dokta fulani,
au professa fulani.....
Au manager fulani
au mmiliki wa kitu fulani.......

Wako sooo empty ,ni kama hawawezi ku exist bila titles hizo......
Duh! kaka umepiga ngumi ya jicho...mule mule pamoja na misifa yoote hiyo..nyumaya pazia ni mizigooo..tena magunia ya misumari
 
  • Thanks
Reactions: Mbu

...ila, tusiendekeze sana uzuri wa sura aka 'Reception' jamani...nadhani tabia ndio thamani ya uzuri wa mwanadamu, au?
Unless mwataka kunambia 'anauza sura' kwenye matangazo ya biashara nk,...
 
mbu na the boss mmefunika' kwa kweli sisi wtz wa leo tumekuwa tukidhani kuvaa sura zisizo zetu kuna tija..,hii kitu imekuwa ikitugharimu sana check na fainali uzeeni baadaye tunakuja kuwa sisi lakini tumeisha chelewa. Hebu tazama jinsi waheshimiwa wanvyoishi, ongea yao, mipango yao,wanavyomtazama mtz-heee! eti nao wamekuwa wafanya biashara wa kiasia..loo wameshuka toka usa cijui ni wawekezaji? KUMBE-nyuma ya pazia ni kina juma maganga,chausiku,mapambano,akilimali,munguatosha,songambele nk wakiwa wamelelewa ktk nyumba za miti tanzania vijijini-tena wamesoma bureee..wanamsaidiaje mtz leo, Mungu anjua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom