Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,919
- 31,161
Kutokana na hali ngumu ya kiuchumi imenilazimu kuanza kibarua kingine ku "supplement" ajira yangu kuu. Gharama ya nyuma, makadi kibao, na vitu vingine ninavyolipia ambavyo hata sivihitaji imenifanya nijikute nabadilisha sana mtindo wa maisha.
a. Hakuna kwenda sinema kila weekend;
b. Hakuna kula out (imebidi nijifunze kupika kitu kingine zaidi ya wali na maharage ya makopo)
c. Hakuna kwenda mjini kwa gari (naendesha hadi Mall, napaki nakuchukua UDA - SmartBus) siku nikiwa na mizunguko mingi
Sasa tatizo kubwa lililopo nikilinganisha na nilipokuwa nyumbani ni kuwa hapa kwenye kibarua kikuu na hata hicho cha pili "hakuna mitkasi" ya kuweza kusupplement kipato changu na hasa shughuli nyingi nizifanyazo. Wakati mwingine hali inakuwa ngumu na ninatamani kungekuwa na "njia" ya mkato ya "kibongo bongo" kuweza kujipatia "kipato cha ziada" bila kuhenyeka sana.
Sasa hili limenifanya nijiulize mtumishi wa umma au hata sekta binafsi (ambaye si mmiliki) anatumia njia gani kusupplement kipato chake na kuafford lifestyle yake? Hivi kwa kipato chako peke yake unaweza kumudu maisha yako au itabidi ufanye mabadiliko makubwa ya jinsi unavyoishi? Je yawezekana kumbe wengi wetu tukipewa nafasi ya kula, tutatafuna bila kukaribishwa na kumegua bila hata kunawa mikono? Je yawezekana baadhi yetu ambao tunatamani kushika nafasi fulani ya kiuongozi tuna upotential fisadism wa aina fulani?
Endapo mianya yote ya ulaji ikifungwa (no per diems, posho nyingine kama za vikao, za safari, za hali ngumu n.k) utafanya nini? Itakuwaje kama bosi wako anataka uwepo kazini kweli kwa masaa nane na usiende kushughulikia "miradi" yako wakati wa kazi? Vipi kama yule mtu wa supply akiamu kuzingatia sheria na kuhakikisha kitu hakitoki isipokuwa kwa saini na kwa idadi kamili; yaani njia zote za ujanja za kujipatia kipato zikibanwa utaweza kuishi kwa kipato chako au kutafuta shughuli nyingine halali katika muda wako wa ziada?
Je yawezekana tunaishi katika utamaduni wa kijanja janja kiasi kwamba ufisadi siyo suala la wenye nguvu tu bali pia watu wa chini ambao maisha yao yote wamejifunza "kuula" na hivyo kila mtu anapopata nafasi ya kutumikia kitu cha kwanza anachofikiria ni jinsi gani nafasi hiyo itampa kipato zaidi ya kile kilichoko kwenye mkataba?
Bila njia za ujanja ujanja tunaweza kweli kuishi kwa kipato chetu cha kawaida.
Heshima mbele mkuu MMJ.
Tunaweza kuishi maisha mazuri kwa pato halali kama tutazingatia yafuatayo.
{1}Kupanga matumizi kutokana na pato lako halali.
Pengine hili linaweza kuwa tatizo kubwa kwa watanzania wengi,mara nyingi tunapenda kutumia fedha zetu bila kuangalia pato letu halisi.Ninaposema kupanga matumizi kutokana na pato halali,maana yake ni kuanzia nyumba tunazopanga,vyakula tunavyokula,usafiri tunaotumia na nk.
{2}Kuwa mbunifu kuongeza pato kwa njia halali.hii itategemea zaidi na utaalamu wa mtu kwa mfano mimi nilikuwa mhasibu GTEA ingawa kampuni imeshindwa kufanyakazi sijawahi kutetereka kwasababu nililikuwa natumia ujuzi wangu kufunga mahesabu kwa kampuni zaidi ya tatu.
{3}Kusave fedha hata kama ni kidogo kwaajili ya kuwekeza.Hili nalo ni tatizo kubwa kwa watanzania wengi.Hatuna utamaduni wa kusave tunapenda kutumia hata kama pato tunazopata litaongezeka ndivyo matumizi yetu yanavyoongezeka.