Unaikumbuka hii?

Da Womanizer

JF-Expert Member
May 24, 2010
1,577
148
Nakumbuka kitaa kipindi hicho wakati redio ni dili kubwa.......
Tena tulikuwa tunaita redio kaseti halafu swali linalofuatia hapo ni "Redio yako ina bendi ngap?!!"......................
Mwingine utasikia anajisifu mi nimenunua kitu kina bendi 12 wakati vituo vyenyewe vya redio viwili RTD na bbc tu na vyote masafa ya kati(MW).
 
Kila zama na makali yake.
Siku hizi redio zina FM na AM tu,
kisha baada ya hapo ni DVD, HDMI, DVX..
yaani digital kuanzia box lake la nje hadi waya wa connection
 
Kila zama na makali yake.
Siku hizi redio zina FM na AM tu,
kisha baada ya hapo ni DVD, HDMI, DVX..
yaani digital kuanzia box lake la nje hadi waya wa connection

Kuna mredio upo home we acha tu..................nakumbuka nilikuwa nawekewa biti hata kuufungulia ni Panasonic kubwa spika mbili na lina vi disco light..............hiyo ilikuwa ni christmass kwa Pasaka!

Aaah ................tumetoka mbali jamani!:becky::becky::becky:
 
Nakumbuka kitaa kipindi hicho wakati redio ni dili kubwa.......
Tena tulikuwa tunaita redio kaseti halafu swali linalofuatia hapo ni "Redio yako ina bendi ngap?!!"......................
Mwingine utasikia anajisifu mi nimenunua kitu kina bendi 12 wakati vituo vyenyewe vya redio viwili RTD na bbc tu na vyote masafa ya kati(MW).
We kwani hujui, walikuwa na maana kuwa hizo bendi ni Maquiz,Matimila,OSS, n.k, n.k......!! Ndizo zilikuwa zinasikika sana redioni enzi hizo.
 
Nakumbuka kitaa kipindi hicho wakati redio ni dili kubwa.......
Tena tulikuwa tunaita redio kaseti halafu swali linalofuatia hapo ni "Redio yako ina bendi ngap?!!"......................
Mwingine utasikia anajisifu mi nimenunua kitu kina bendi 12 wakati vituo vyenyewe vya redio viwili RTD na bbc tu na vyote masafa ya kati(MW).
Hii mada kama siyo tungo tata basi siyo mahala pake :nono:
 
Umenikumbusha story fulani hivi....ashukum si matusi Jamaa fulani alinunua redio kaseti, siku moja akawa ame-import kimwana. Akafungulia redio yake kwa sauti kubwa halafu akaisogeza karibu ya dirisha ili majirani wasisikie kinachoendelea ndani, Wakati wanaendelea na shughuli akapita mwizi dirishani akaingiza mkono kuiba ile redio. Kufuatana na mkao wao katika shughuli kimwana akamuona yule mwizi, akaanza kusema rediiiio,,redi..rediii.. rediii..jamaa akafikiri ni mbinu ya kimwana ili amhonge redio yake, goli lilipoingia kimwana akamalizia kwa kusema redio inaibiwa...redio imeibiwa!!!, jamaa si alitoka mkuki kumfukuza mwizi akiwa amesahau kuvaa nguo....majirani wakafikiri amewehuka...!!!!
 
Bila shaka enzi hizo Chidumule, Remmy n.k ndio walikuwa wanakimbiza kunako ulingo wa dansi.
 
bila kuwasahau akina Hemedi Maneti, mzee Hamza kalala, Nico Zengela, Adam Bakari.......ya kale yana utamu wake it kind of music history if not funny
 
Back
Top Bottom