Unahisi umebambikiwa mtoto?........... Mtazame usoni!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Imebainika sasa kwamba, kuweka kwetu ndita, kukunja uso kwa hasira na kutoridhishwa, hakutokani na kuiga kwetu kwa wazazi au walezi, bali zaidi hutembea katika kizalia (Genes). Watu wa familia moja au ambao tunasema ni damu moja, wanaonekana kuwa huwa wanatumia mtindo wa aina moja wa kuonesha kukereka katika nyuso zao.

Watafiti ambao wamekuwa wakichunguza kuona kama nyuso zetu hubadilika tunapokereka kwa kujifunza au kwa kufuata kizalia, wamebaini jambo hilo, baada ya kuwafanyia walemavu wasiiona utafiti. Pamoja na kwamba, huwa tunaiga kuweka ndita, kukunja midomo au kionesho kingine cha kutoridhika kihisia kwa kuwaiga wazazi au walezi wetu, imeonekana kwa sehemu kubwa kwamba, kuna suala la kurithi tabia hizo. Kwa mfano, kwenye tafiti zilizofanywa ambapo walemavu wasiiona wapatao 21, walifanyiwa utafiti. Walemavu hawa walizaliwa wakiwa hawana uwezo wa kuona. Baada ya kuulizwa maswali yasiyoeleweka, au kusimuliwa habari za vurugu na umwagaji wa damu, wagtu hao walionesha ishara za uso, ambazo zilifanana na zile zilizooneshwa na ndugu zao.

Watafiti walichunguza uinuaji wa nyusi za uso, utapanyaji wa midomo na ishara nyingine za uso na kugundua kwamba, za ndugu wa wale walemavu zilikuwa karibu sawa na walemavu kuliko mza watu wengine waliohisishwa kwenye utafiti huo.
Kwa sehemu kubwa, ishara za uso zenye kuonesha kukerwa au hasira na kutoridhika, ndizo ambazo hufanana kati ya ndugu. Hii ikiwa na maana kwamba, ndizo zilizorithishwa, kuliko zile zinazoonesha furaha. Mmoja kati ya watu waliohisishwa kwenye utafiti, alikuwa hajaonana na mama yake kwa miaka 18, kwani alipozaliwa tu alipewa familia nyingine kumlea. Huyu naye, alionesha ishara za uso ambazo zilikuwa ni sawa kabisa na mama yake. Hii ilizidi kuthibitisha kwamba, ishara hizi huwa zinarithiwa zaidi kuliko kuigwa.

Kwa mfano familia ambayo wakiudhika au kutoridhishwa na jambo hubinua midomo, wengi katika familia hiyo, watakuwa na mtindo huo, hata kama hawakukulia nyumba moja. David Matsumoto kutoka chuo kiku cha Francisco, marekani, anasema, huenda hii ni juhudi ya maumbile ya kutaka uwabainisha ndugu kutoka wale ambao siyo ndugu. Hii ina maan pia, mtu anaweza kujua kama mtoto siyo wake bali wa fulani kwa kuangalia namna mtoto huyo anavyoonesha ishara ya kutoridhishwa kupitia uso. Kama mtoto wa familia fulani, ana mtindo tofauti kabisa wa kuonesha kwa uso kutoridhika, inaweza kuwa na maana kwamba, mtoto huyo siyo wa familia hiyo. Je hii inaweza kuwa njia nyingine ya kubaini kama mtu amebambikiwa mtoto? Ndivyo tafsiri ya wataalamu ilivyo.

Hata hivyo, naomba usitumie njia hiyo kupima kama mtoto ni wako au siyo, kwani haijathibitishwa kama ilivyo kwa DNA.
 
Kwa sisi Watanzania kuangalia usoni haitoshi, labda kwa wenzetu wazungu! Mi nafikiri DNA ndiyo mpango mzima! :poa
 
Haya kwa wale wenye ndoa za mashaka,kutoaminiana na wanaotafuta sababu za kuachana,kazi kwenu sasa!
 
Mkuu, nakubaliana kabisa na hizo ishara hasa hizo za uso unavyo'react kwenye hasira, huzuni, mshtuko n.k iko mpaka ndugu wa familia moja kwa nyakati tofauti nimewaona wakitaka kuanza kula wanakohoa kakihozi flani hivi kaaina kama pozi hivi, ndio waanze kula.
Tena hata wenyewe mtu na kaka yake hua hawajijui, mimi ndiyo nilikua nawastukia.
 
Kwa sisi Watanzania kuangalia usoni haitoshi, labda kwa wenzetu wazungu! Mi nafikiri DNA ndiyo mpango mzima! :poa

Maumbile hayana uzungu bana, Mbona hata madaktari wetu walio wengi wamesomea huko kwa wazungu na sasa wanatutibu.
Hebu chunguza, kuna facial expression ambazo tunarithi kutoka kwa wazazi.
 
kweliiiii,, sisi kwetu mtu akikereka kuna aina flani ya utazamaji.. Mi mwenyewe nimeishuhudia kwangu na kwa ndugu zangu kibao.
 
kweliiiii,, sisi kwetu mtu akikereka kuna aina flani ya utazamaji.. Mi mwenyewe nimeishuhudia kwangu na kwa ndugu zangu kibao.

Kumbe tunaweza kujua kama huyu ni ndugu yetu au mama aliibilizia nje kwa kuchunguzana namna tunavyobenua midomo kwa dhereu au tunapochukizwa na akina Rejao au Bujibuji..............LOL
 
shikamoo baba,
Hii kwangu ni mpya keshokutwa naenda moshi,
Nitafanya karisechi ka mda kwa ndugu zangu nione na sie tuna stail gani lol!
 
shikamoo baba,
Hii kwangu ni mpya keshokutwa naenda moshi,
Nitafanya karisechi ka mda kwa ndugu zangu nione na sie tuna stail gani lol!

Unajua kuna kastaili fulani ka kubenuan mdomo wa chini upande wa kushoto pale unapomtazama mtu kwa dharau, niliwahi kumuona baba yako akibenua mdomo kwa staili hiyo, kwa hiyo sina wasiwasi, wewe ni mtoto wa mzee naniliu kabisaaaa.........
 
mguno!

DAh......hii junior anayo sana; nikidhania ananiimitate na hasa nikiwa serious kwenye tafakari ya jambo fulani ama kutaka kuanza kufanya kazi fulani; hali ambayo nami huwa naipata bila kutarajia!

Thanks!
 
Kuna jamaa humu jf anasema eti ni ndugu yangu wa damu, Ngoja nimwangalie usoni kwanza. ntarudi. ova
 
Unajua kuna kastaili fulani ka kubenuan mdomo wa chini upande wa kushoto pale unapomtazama mtu kwa dharau, niliwahi kumuona baba yako akibenua mdomo kwa staili hiyo, kwa hiyo sina wasiwasi, wewe ni mtoto wa mzee naniliu kabisaaaa.........
Hahahahaha!
Mie simo unajua kbs mama anamiliki passwedi ya id yako,
Mie mtoto tu hayanihusu kbs,
Nitamwambia wala sikujua kmaunaniongelea mie!
 
Hahahahaha!
Mie simo unajua kbs mama anamiliki passwedi ya id yako,
Mie mtoto tu hayanihusu kbs,
Nitamwambia wala sikujua kmaunaniongelea mie!

Naona sasa mwanangu unataka kuleta shari kwa mama yako........................ Haya nenda kafanye homework, usibishane na baba yako............
 
Back
Top Bottom