Unafki ni...................?

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,228
1.Unajifanya unasuluhisha watu wanapigana kumbe kimoyo moyo unataka wadundane ila unasuluhisha tu ili uonekane unajali

2.Kujifanya unasuluhisha wapenzi waliogombana kumbe kimoyo moyo unataka waachane ili ufaidi.

3...................

4...............

5................



endelea
 
Kujifanya wampenda rafiki yako kumbe behind the scene unatamani kumtilia sumu kwenye chakula kwa sababu ya maendeleo yake..
 
Kujifanya wampenda rafiki yako kumbe behind the scene unatamani kumtilia sumu kwenye chakula kwa sababu ya maendeleo yake..

unatamani mtoto wa jirani yako afeli mtihani ili wako aonekane kichwa
 
Kushangilia kwa vigelegele na makofi mengi hotuba ndefu ikiisha,kumbe ulikuwa unataka amalize fasta!

Gee Cee

kujifanya unalia machozi kuonyesha unauchungu lakini hujivui gamba
 
Unajidai unapenda kwenda kanisani, lakini unasubiri 'amina' ya mwisho kwa hamu kubwa.
 
Unaenda kumsalimia mgonjwa na mijuisi ya maana, afu unamtangazia kachoka na ana miwaya wakati hujaona vyeti vyake.
 
Unamwita shemeji demu wa rafiki yako, afu ukibaki na shemeji unamponda rafiki yako, na unamtaka huyo demu wake.
 
Workmate akipandishwa cheo unampongeza kwa bashasha, kumbe unataka kumnyonga ili upate nafasi yake.
 
rafiki yako akipata hasara kwenye biashara unatamani kufungua shampeni kwa furaha.
 
Unaenda kumsalimia mgonjwa na mijuisi ya maana, afu unamtangazia kachoka na ana miwaya wakati hujaona vyeti vyake.

Hapa nimecheka hadi watu wameshangaa!

That is real Konnie...

My JF Best Entertainer of All Times..
 
Binti anavalishwa pete ya uchumba, anawaonesha mashoga zake, akiondoka wanaanza kusema pete yenyewe ya sh. 15m.
 
Back
Top Bottom