Unafiki wa wazi wa hawa watu...

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
925
Dr. Mwakyembe,awali alilieleza taifa kuwa amelishwa sumu, akatuhumu Serikali hasa vyombo vya usalama kuwa hawalichukulii suala lake kwa umakini, wanampuuza yeye japo ni Waziri wa Nchi hii, je raia wa Kawaida waingekuwaje?,.

Ikumbukwe kuwa hata alipopata ajali wakatu ule alitaka kuihusisha ajali hiyo na Jeshi la Polisi na alilituhumu na kusimama kidete kumtetea Dereva wake. Wengi tuliamini kuwa kweli Mhe. huyu anaandamwa na wanania ya kumwondoa kutokana na upiganaji wake kuping ufisadi. Hata hivyo, Kauli alizozitoa karibuni kuwa anaugua ugonjwa wa Ngozi ndio umetushtua wengi..nia yake ni nini?. Hajui madhara ambayo yanatokana na kauli zake za Kinyonga? ... Sasa Dr. anakana hata yale ambayo aliyatoa katika kinywa chake, yale yaliyoandikwa kutokana na warzaka ambao inadaiwa kuwa yeye aliandika, ule walaka ambao umebainisha mbinu za kijajusi ambazo zilitumikwa kumdhuru, ukamtaja mtumishi wa Umma aliyehusika na sasa yu marehemu (Je, ndugu za Marehemu yule wanajisikiaje sasa kwa yeye kuhusisha na makakati wa kumdhuru Waziri wake?? Je, nao hawana haki ya kuomba suala hili lichunguzwe ili ukweli ubainike?, wao hawataki kujua ndugu yao nini kimemuua?)

.Ikumbukwe kuwa Dr. Mwakyembe kwa histori sio mwanaharakati, yeye kwa nyakati tofauti amewahikuhusishwa na kazi za Mfumo (TISS).

Kuteuliwa kwake na Bunge kwenye Kamati ya Kufuatilia zabiuni ya Umeme wa Dharura iliyotolewa kwa kampuni ya Richmond LCC kamwe hakukumfanya yeye kuwa mpinga ufisadi..alikuwa anawasilisha tu yale ambayo Kamati ya Bunge ambayo alikuwa Mwenyekiti ilibaini na hjazikuwa fikra zake binafsi (Mama Kilango Malecela alilibvainsiha hilo vizuri wakati Bunge lilipojadili Ripoti ya Kamati ya Kuchunguza Sakata la Jairo)..Vinginevyo, tukimwingiza kwenye kundi la wapinga UFISADI tunaweza kuwa tunaafikiana na maneno ya Lowassa kuwa Kamati ya Mwakyembe ilikuwa "Bias" iliegemea upande mmoja. Kwani kwa kawaida, Kamati ya aina il, kama ilivyo kwa Jaji au Hakimu wa mahakama, inapaswa kuwa "huru" (Neutral). Hivyo, kwa mazingira haya, Mwakyembe AU Samwel Sitta ambae kwa wakati ule alikuwa Spika wa Bunge lililounda Kamati na kupokea Ripoti ya Kamati ya RICHMOND kamwe hawezi kuvaa gamba "wapinga Ufiosadi". Kwa kufanya hivi, inaonekana wazi kuwa walikuwa tayari wamefikia uamuzi (perceived decision) na kuwatia hatiani waliohusika (Lowassa, Rostam, Msabaha, Karamagi et al ) kabla hata kutolewa ripoti ya Uchunguzi..

Nasita kusema,
kwa wale aliowafundisha pale UDSM wanamjua vizuri..Dr. ni Mtu ambae amebeba sifa zote za baadhi ya makabila ya Nyanda za Juu kusini hasa ukanda ulee atokako..( sina maana ya kutusi) wengi wao ni wakarimu, wacheshi, ila baadhi yao ni watu wa kupenda "publicity" wanafiki, wasio na msimamo, wenye kujifagilia fagilia, wengi wanapenda kujionyesha wanajuana wa watu wengi, wanajua mengi nk nk).

Samwel Sitta nae kigeugeu, na ndie ambae alieachai Bunge kujadili kwa moto mkali sana sakata la Richmond na Dowans lakini cha Kusikitisha, aliafiki hoja za Chama na Serikali yake kuufunga Mjadala huo kabla mambo hayaja wekewa Mkakati wa Kuyashughulikia..Leo Sitta ambae anakipande cha Keki ya CCM mdomoni (akiwa ni Mbunge na Waziri wa CCM ) hawezi kutuambia kuwa anapingana na Mtu kama Lowassa au Rostam (watu wa Chama chake) toka moyoni mwake..huu ni unafiki wa wazi kabisa..
 
Tuweke wimbo wa kigeugeu jamani hapa. Hivi lakini cheo huwa kinatafutwa kwa nguvu hivi? Kama ni hivyo basi mimi siwezi. Kura kwa Dovutwa tujue moja!!!!!!
 
Wangekuwa kweli wanapinga maovu yanayoendelea ndani ya serikali wanayoitumikia walau wangejiuzulu. Na mimi sintashangaa siku Sita atakaposhikana mkono na Lowasa kuwa anaomba yaishe maana wananchi wanazidi kujua ukweli juu ya Richmond na tofauti za kimtandao.
 
Dr. Mwakyembe,awali alilieleza taifa kuwa amelishwa sumu, akatuhumu Serikali hasa vyombo vya usalama kuwa hawalichukulii suala lake kwa umakini, wanampuuza yeye japo ni Waziri wa Nchi hii, je raia wa Kawaida waingekuwaje?,.

Ikumbukwe kuwa hata alipopata ajali wakatu ule alitaka kuihusisha ajali hiyo na Jeshi la Polisi na alilituhumu na kusimama kidete kumtetea Dereva wake. Wengi tuliamini kuwa kweli Mhe. huyu anaandamwa na wanania ya kumwondoa kutokana na upiganaji wake kuping ufisadi. Hata hivyo, Kauli alizozitoa karibuni kuwa anaugua ugonjwa wa Ngozi ndio umetushtua wengi..nia yake ni nini?. Hajui madhara ambayo yanatokana na kauli zake za Kinyonga? ... Sasa Dr. anakana hata yale ambayo aliyatoa katika kinywa chake, yale yaliyoandikwa kutokana na warzaka ambao inadaiwa kuwa yeye aliandika, ule walaka ambao umebainisha mbinu za kijajusi ambazo zilitumikwa kumdhuru, ukamtaja mtumishi wa Umma aliyehusika na sasa yu marehemu (Je, ndugu zama
 
Wangekuwa kweli wanapinga maovu yanayoendelea ndani ya serikali wanayoitumikia walau wangejiuzulu. Na mimi sintashangaa siku Sita atakaposhikana mkono na Lowasa kuwa anaomba yaishe maana wananchi wanazidi kujua ukweli juu ya Richmond na tofauti za kimtandao.

Mnafiki siku zote haishi kujifikicha!!
 
Kwa bahati, sikupata kuamini hata chembe simulizi za Mwakyembe...kama ulimwamini au unaendelea kumwamini basi pole yako!
 
Kwa bahati, sikupata kuamini hata chembe simulizi za Mwakyembe...kama ulimwamini au unaendelea kumwamini basi pole yako!

SIkupata hata siku kumwamini ....yawezekana hata yale aliyoandika katika Ripoti ya Bunge ya Richmond yalijaa upotoshaji?
 
hawa jamaa ni hatari sana na wanaendelea kuaminiwa na nwtanzania wasiojua ni nini wanafanya...bado najiuliza ofisi ya spika ya urambo iliyogharaim takribani milion 300 inafanya kazi gani sasa....:thinking:
 
Mwakyembe tumtendee haki, ni kweli labda amekuwa mnafiki kwa kiasi fulani lakini pia tuangalie mazingira aliyokuwa nayo kabla wakati na baada.

Je kweli tunamlinganishaje na wanakamati wenzake wa Richard munduli? Ole sendeka, Kilango aliyechota mpaka sifa ya kimataifa, si na injinia stela manyanaya ni moja wao, wote wamenunuliwa na mafisadi kwa dau ndogo tu?

Mpendazoe tu ni shujaa aliyebaki, hakuwa mnafiki.

Ushauri wa Bure kwa Makembe, kaa mbali na maadui zako, it is too late to compromise. Umeponea chupu chupu sasa utakuwa mishikaki usipoangalia. Undumakuwili ni art ambayo wewe huwezi

 
Mwakiyembe ni mwalimu wangu pale UDSM hivyo namfahamu fika!. Ameomba tuyaache ya kuumwa kwake tusonge mbele!.
 
Ukiwa mnafki ujanani unakua mchawi uzeeni.kwa umri wa 6 yule si mnafi tena,ni mchawi ten mshirikina,mzandiki.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom