Unafiki wa wanaJF inamaana hamumfeel mchizi kama anavyowafeel?

kama kufall in love na avatar ni zambi acha tu niandikiwe. khaaaa! hakyanani mapigo ya moyo yameongezeka kwa 5% baada ya kuangalia hii avatar

Taratibu please...abulance ziko mbali....zinaweza ziwe bado kule Gongolamboto...! Na sisi bado tunakuhitaji humu....
 
Ha Ha haaaa... I like you Dudes... napenda kuwaita The Funny Trios au The Three Amigos.. Yaani Akiwepo Hashy, Uporoto na Kloro... Lazima ucheke..

Hapa wakuu mgekuwa mnakusanya haya maandiko na kuweka kwenye kitabu mnaweza kutengeneza Comedy...:clap2:
Tunashukuru kwa kutukubali kicheko kinaondoa stress.

Hivi kweli...Nilham naye kadisapia lini??? sijamwona yule mrembo wa kiarabu....au baada ya watu kujua ile picha sio yake... kama yeye alivyosema???
Nilham ana matatizo ya moyo tumuombee.

kamanda tumeanza kukutilia wasi wasi na wewe sasa. hii chain kumbe ni kubwa acha niwasiliane na kamanda mwema.
Hommie hata mimi ? wahusika ni wanajeshi wenyewe isije kuwa wanamalalamiko kama polisi wa misri. Mwenzio siki hizi ni mtori na ndizi moshi kwa kwenda mbele vurugu na mabomu hapana.
 
nina hakika nikifa kwa ajili ya avatar yako nitakuwa nimekufa kifo cha five star. usibishe nitachukia

Hapana usikufe tafadhali...sasa nani atakuchekesha humu??? Mi hapa stress zote kwisha kabisa...nikilala usingizi mololuuu....:clap2::clap2:
 
nina hakika nikifa kwa ajili ya avatar yako nitakuwa nimekufa kifo cha five star. Usibishe nitachukia

umenikumbusha nilivo kuwa mdogo mi na braza tuligongwa na magari dingi alipokuja kutuona akanigombeza eti kwanini nimegongwa na bito wakati braza ye aligongwa na benzi......aiskrimu zote akapewa braza
 
Hapana usikufe tafadhali...sasa nani atakuchekesha humu??? Mi hapa stress zote kwisha kabisa...nikilala usingizi mololuuu....:clap2::clap2:
hehehe senks. jaluo_nyeupe anaweza akacover, kijijini kwao wanamuita kris rok, juzi wamempeleka shopping kigali
 
Hivi ina maana mliotajwa hapa mamumfeel huyu jamaa? kweli ubinadamu kazi sie ambao hatujatajwa tunaona unafiki wa waliotajwa Shosti kafungua thread https://www.jamiiforums.com/complaints-congrats-advice/111177-shossi-uko-wapi.html anamuomba jamaa arudi nyie mmeipotezea duh!


user-offline.png
Mohammed Shossi


29th January 2011 12:20 PM
#1
JF Senior Expert Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
im_msn.gif



Join Date : 17th January 2011
Location : Dar es Salaam
Posts : 1,621
Thanks 143 Thanked 542 Times in 314 Posts

Rep Power : 24




1 out of 1 members found this post helpful. Did you find this post helpful? |
icon1.png
Magreat Thinkers ninaowafeel...........


Nabofya kibodi yangu, salamu nazituma,
Kwenu marafiki zangu, natumai mu wazima,
Nawaombea kwa Mungu, mjaliwe yalo mema,

Nilham usiyechoka, asubuhi na jioni,
Nyumbani kuwajibika, halafu pia kazini,
Kisha huachi andika, kutujuza kulikoni,

Ni wewe ulieniteka moyo wangu
Nikaamua kukutokea kimizungu
Nikubalie mpenzi niachane na machangu

AfroDenzi
, nakuzimia tangu MWANZONI,
Fikra zake ni huru, pia zina burudani,
Nami ninamshukuru, hachoki tangu zamani,

Yupo dadetu
Festiledi, yeye hupenda MAISHA,
Kamwe hawezi kusita, mazuri kutuonesha,
Thanks tele azipata, maana huelimisha,

Michelle
yupo, hutaka TUJIELEWE,
Daima aandikapo, vichwa vyetu tusuguwe,
Sifa zake zipo, muhimu apewe,

Dr W. Slaa
nasaha tumepeyana, tena tukanufaika,
Mafumbo tukafumbana, kwa furaha na kucheka,
Na mara tukabishana, na wengine tukachoka
Kisha ukarudi tena, huku tumeshachamka.


Mzee Mwanakijij
i, MZEE WA CHANGAMOTO,
Haishi kutuambia, mambo yalo motomoto,
Habari hutupatia, yenye midundo mizito,

Hashycool
anza tangaza, ni kwako yamechimbuka
Watunzi waagiza, ushauri kuwataka
Yaseme kwenye baraza, hii ni mbiu ya mwaka.

Kaa la moto
Chochote unachoweza,hima weka mchangoni
Hilo ndilo unalowaza,tukakawa hatulioni
Ila sala memaliza,ndio ukatia udhu

Madela wa Madilu
keri hazi ghasi, nyimbounawaimbia
Mwenye kukerwa huhisi, hujali humuingia
Hawi zimwi asikisi, ikawa bure tabia.

Pakajimmy amejieneza,sifa zakejamvini,
Jambo analoliwaza, taarifa kuwapeni,
Si vizuri kunyamaza, bora awajulisheni,

Kaiza
kaka yetu sote, jitu liloshiba,
Mengi hutaka tuyapate, yale yaliyoshiba,
Asichoke asisite, ajaze hata kibaba,

Gsana
Naingia jamvini, hapana tena ajizi
Nazikubali shukrani, kwa juhudi zangu hizi
Kushajiisha jamvini, watunzi wa zama hizi
Kheri ipo kwa manani, Mpaji kanijaalia.


Katavi
na LazyDog ipambeni JF wananeti mwasikia
Tenzi na mashairi nyeti, wengi watafurahia
Uridhi ndani ya beti mmfiche mmesikia?

Shishi na
Mpevu hoja za kweli toeni, faida kutupatia
Aso ubavu wavuni, shimoni atakimbia
Mtenza mwenye nguvu makini, hadharani nawambia
M_bongotz
acha woga, wananeti yetu hiba.

Kuwa fundi si ajabu, hilo kwanza eleweni,
Kuwa fundi ni thawabu, aliyanena Manani,
Msijempa adhabu, kwa maswali ya kwa nini?
Drphone ameshasilimu, sasa naitwa FUNDI.


Rose
naye ni rafiki, hutumia DARUBINI,
Kazi yake haichoki, popote ulimwenguni,
Kwenye siasa na urafiki, hutujuza kulikoni,

Mwanajamvi
Aspirin, hutuonesha MWANGAZA,
Makala zenye hekima, na mambo kuyachunguza,
Kwa ushairi ni vema, post zake zapendeza,

Zion Daughter
Si wakuamsha daku,walo macho wameona
Hashindani na kuku,kula wanacho kiona
Wala havai kikuku,kuwaiga walonona


Miss Judith
huyo, ana UPANDE MWINGINE,
Yale ayaandikayo, hupendwa nao wengine,
Kwa mawazo si mchoyo, hufanya tushikamane,

Gbolin
umesibu, umenena ya hakika
Tena nimetaajabu, posti zako za haraka,
Wajibu tena wajibu, wanajamvi kukusanyika
Jamvini bila tabu, sote twaburudika.

Wa ndima
Mgosi vipi unadhani, nasaha zipi azizi?
Nianze upande gani, kuepusha jinamizi?
Ni ipi ile ya ugoni, kutanguliza malezi?

MwanajamiiOne
pia, hutuambia AMKENI,
Hachoki kutuletea, yatokeayo nchini,
Daima hukumbushia, tutoke usingizini,

October
mwenzetu, utujuzaye maisha,
Wewe ni darasa kwetu, maarifa yaso kwisha,
Wafunza juu ya utu, mengi watuelimisha.

Teamo
bado kuchoka, upo kwenye msafara,
Ungali kwenye pilika, kwa zako huru fikra,
Nakuombea baraka, uzidi kuwa imara,

Mwenzetu
ni mwanaharakati, daima usiyechoka,
Wautumia wakati, pasipo yoyote shaka,
Maisha kuwa na chati, daraja la uhakika,

Inkoskaz
Upo kwenye mapambano, ujenzi walo taifa,
Hujalala kama pono, wastahili nyingi sifa,
Washika yetu mikono, ili tuzizibe nyufa,

Kiraka
mwendo ukaze, usiache harakati,
Mawazo uyaeleze, tena kwa kila wakati,
Ili nasi tujifunze, nawe uwe katikati,

Voiceofreason
, mapenzi umeandika,
tangu siku za zamani,
Yale yaliyokufika, na yale ya majirani,
Na kwako alozimika,umesema ya moyoni,

Ndugu yetu
Preta, kabobea kwa MAVAZI,
Vitu vyake ni vizuri, hilo mbona lipo wazi,
Yupo kwenye mstari, hachoki kufanya kazi,

Fidel80
nayakumbuka, manenoyo jamvini,
Hakika niliridhika, nami nikakuamini,
Kwako hayakufichika, hata yale ya moyoni,
Hashima siku hizi hakuna labda zamani

Invisible
tunamjua, mkuu wetu KIJIWENI,
Sheria apambanua, ili asitupige ban,
Sote tukajitambua, tujijue kina nani,


Mkuu
Klorokwini, posti zake ni KITAMU,
Hatosahau daima, kutupa yote muhimu,
Ujuzi wake kisima, haisaliti elimu,


Mkuu
Kashaijabutenge,nakuheshim zamani na sasa,
Yeye wala hajalala, mengi ameshayaasa,
Kabobea mijadala, ya jamii na siasa,

Kimokole
moyoni nafarijika, malenga tukikutanika,
Ya haki kuyatamka, batili kuzifunika,
Kheri ikaminika jamvini tukanufaika.
Bwana Kimokole, nakushukuru hakika


Magulumangu
mshairi, USHAIRI MAMBOLEO,
Mashairiye mazuri, tena yale ya kileo,
Huukuza ushairi, na kuupa mwelekeo,


Na
Wiselady, siachi kumsifia,
Elimu kutugawia, na picha kutuwekea,
Mazuri hutuambia, ndani ya hii dunia,

Maria Roza

Posti zako laiti ni tarumbeta, kuvuma wakasikia
Lakini wapi ni nta, sikioni wametia
Lije kubwa la kivita, barugumu likalia

Ndugu yangu
Rutashunyuma, sitokuwacha nyuma
Posti zako nii ghali sio kama uji
Zinawakuna wa mbali mbaka Tabora na Ujiji

Mjomba
Bujibuji, mwingi wa burudani
Posti zako adhimu, zinatupa burudani
Sina wakufanisha hata na mmoja humu ndani.

Nakumiss
mzee wa malivdavi ulie kaburini
Baada ya posti mbili wadau wakakupa bani
Kifo chako historia ndo mana nakutilia ubani

Ewe nawe
The Finest usinung'unike,
Tena uingie ndani nawe ufarijike,
Utuambie amkeni, wanajamvi tubadilike
Tushikane kwa imani wanajamvi tunusurike.

Wozawoza
wewe mshari jahili,
Kama huoni dalili, kebehi si jambo kupigania,
Twatetea kwa ukali, siambe tunatania
Kiwa sio zetu sisi, dini hizi ni za nani?

JF Moderator1
huyu wa ajabu, wala hataki mchezo
Kuwatia watu adabu, bila kuleta mizozo
Katoa watu ububu kukumbatia kuozo
Lazima tumpe thanks, Wanajamvi tumfurahie.

JF Moderator2
huyu ni hodari, Mtauni humkani
SIHABA baba jasiri, wala hataki utani
Hakuna kutafakari, mwanajamvi si muhuni
Pongezi tumpe na jamvi kulifurahia.

Mwenzetu huyu si mgeni,
Samora10 mwamjua
Mwenzetu si limbukeni, kusema anayoyajua
Samora10 hana utani, kwenye uovu hufichua,
Ni kijana muadilifu si kijana wakuchakachua.

Jaluo Nyeupe
mwamjua, bilashaka mwamuona
Ni yeye tunaemjua, hakika yupo bayana
Haki huitetea, bila kubaguana
Jaluo Nyeupe
ni rafiki hana kubaguana.

Na
Lizzy na Husniyo msisite, ikawa tusionane
Wala tusijikokote, mlonayo muyanene
Mllipo mji wowote, mambo tuelimishane
Abebwae hujikaza, ukumbi tuuchangie

Nyani Ngabu
, Babaubaya, michango nileteeni
Ninyi ndugu pia, shime tujitokezeni
Muhimu ni zetu nia, na wala sio thamani

Lizzy
fanya kuniandikia, wapi yako maskani
Ndipo nitapokwambia, mchango umpe nani
Na mimi tafatilia, nizitie kibwetani

Hongera niwatumie,
Kibunango na Babu Atakasema sirisiri
Na duwa tuwaombee, Rabi awape kivuli
Mungu awazidishie, duniani na peponi

Masikini_Jeurina
na Gurudumu hawa harambee, wapiga debe jamvini
Hawana ila ushee, imekuwa hamkani
Wamejifanya wazee, wao ndio makarani
Posti nyingi wanaandika hapa jamvini,

Muhogo mchungu
kwa siri au dhahiri , atoae yujamvini
Uziitazo ghururi , mwenyewe amezibuni
Unenayo yafikiri, usijeitwa fatani

Mwaminifu
thread ulozitunga,zitawafika wahunzi
Wale wasije kulonga,uloanza mwanafunzi
Wapita ukiwachonga,kwa vile una kurunzi

Ki Mey
hutenda mengi ya dini, habanduki kanisani
na posti nyingi jamvini, hukaribisha na wageni
na ibada za nyumbani, hatutaki hata wageni.

WomanOfSubstance
Na kama wapendelea, usitajwe hadharani

Kwa kuwa unahofia, mambo fulani fulani
Ninakuhakikishia, taweka siri moyoni


Maxishimba
uchunge mwenendo wako , wende mwendo wa kupima
Utunze twabiya zako , ujuwe baya na jema
Kama hujali wenzako , kutenda ya kuwauma
Ngoja nawe siku yako , utendwe bila huruma

Kakajambazi
, yeye huyu si mwizi, na tena ye si jambazi
Kanilaghai kiujuzi, kwa jinale jamvini
Huyu yeye si jinamizi, akatuchuna na ngozi
Kakajambazi ni mwema mwenzetu jamvini.

Tatiana
Kashika kuwasafisha, jamvini harufu waridi
Kutwa atuhamakisha, kuwa yeye ni shahidi
Posti zake zisokwisha, za tamu tena jadidi

Sulphadoxine
Unasi ghamu ghalati, siugenini jamvini
Siraji ng'aza sirati, uongoze Furusani
Chifunaga
kapaza sauti, Mwamuska si mwoga jamvini
MANYANZA
taabani, hali hana hamu.


Mawazo1109
ni wetu sote, hima tusaidiane
Wa mbele tuwafuate, haya tusioneane
Kwa hili natusitete, bali tusikilizane
Abebwae hujikaza, ukumbi tuuchangie.

GT
wake mdogodogo mwendo, wajulikana zamani
Mwendo usio vishindo, haufeli abadani
Asoweza huwa kando, awezae huwa ndani

Mbongopopo

Chunga heshima na cheo, na maovu usifikwe
Fidhuli umjuapo, usimtoze neno lake,
Takuudhi na wenzio, ushikapo pasishikwe
Umjuaye kunyakwe, simnyishe penye watu....

Godfrey Tajiri
Kweli wewe si wasongi, malenga mashuhuri
Umejikita kama kigingi, mwingi wa sururi
Usia nakupa tena uukariri
Usije oa shangingi maisha ukayaona shubiri
Cheusimangala,
Kadhalika nawe pia,usihi uko peke yako

Ukadhani umesahaulika ukawaonea wivu wenzako
Unaujuzi wakujitetea,kwa hoja zenye mashiko
Basi iweze duniya,kwani ya kale hayako
Upatapo tungo yako ,utaingiya jamvini



BLUE BALAA acha makeke, ushairi si mapene.
Kalamu yake Nsiande, kali kaka ujuani
Wapaswa kukaa chonjo, Rais msije mtaniani
Watajakutoa mkojo, Segerea wala si uraiani




Nguli Jabali wewe mbora, amekupamba Rabana,
Tena umetia fora, posti hufana,
Basi usiwe mkora, akiba uweke sana,
Sihadawe na unyange na unyange una mwisho


Vuvuzela
Nakuambia wazi wazi,sitaacha kusema neno.
Kwani jana sio juzi,ulimi si sawa na meno.
Umalenga si kuna nazi,hili ukumbuke mno.
Utunga hata kwa hirizi,uyawache majivuno.


Mimi ningali mwanafunzi katika hii tansia
Bado singuli kutunga nje ya tanzania
Baraza watu mahiri Kimensera acha kutania
Ila umetoa wazo zuri kazi talifanyia
Sivibaya kuijenga lugha yetu sawia
Nawe pia umo njoo tupige kasia
Usijitoe kundini kusema utenzi ni kadhia

Tungo huleta faraja penye dhiki na ghasia
Malenga hutoa hoja za msingi na wosia
Namaliza kukuomba tunga japo kwa kukisia.
Wajuzi walo jamvini watakufunda kiintelejensia.

DaMie nimeona na wewe nikutaje
Mtoto uliye na hiba nikushau iweje
Posti zako ni dawa zimeshinda mvuje
Zina toa wosiwa dar mpak kivinje
Usirudi nyuma jamvi usilikunje

Mdondoaji hupo nyuma kuchangia jamvini
Sasa noa panga na jembe tia mpini
Nani asojua mchango wako jamvini?

Superfisadi sasa amka, tenzi kutupatia
Uzipange kwa ubeti sio za kutupia
Utujuze hali yako na aila yako pia
Usinisahau kwa dua pamoja na nabia
Mungu akupe ya kheri na wanajamvi pia.

X-PASTER upo wapi mbona umetulia
Nini kimekusibu hoja hujachangia
Najua upo buze dini kulingania
Mungu akupe baraka na dhawabu pia.

Nami MWAJAMVI MIMI, Mohammed Shossi
Tungo zangu siwanyimi, nawapenda kiukweli,
Tena mara kumi kumi, tena na kwa kila hali,


Ambao sijawataja
, lipo shairi jingine,
Sote tungali pamoja, kwa mema tuombeane,
Tusichoke zetu hoja, hivyo na tushikamane,


Duh mkuu kamaliza kila kitu..............
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom