Unafiki wa Marekani na ukibaraka wa Kikwete vinavyoangamiza Watanzania

Massenberg

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
1,173
1,370
Siku wananchi watakapoamua kupigana dhidi ya udhalimu (kama itatokea wakawa na ujasiri huo) wanaofanyiwa na serikali iliyoko madarakani, Wamarekani hapa nchini wasiachiwe.

Hii ni kwa sababu Marekani inajipambanua kuwa mpigania haki za binadamu duniani kote, lakini cha ajabu mauaji ya raia na uvunjaji wa haki za binadamu unakithiri hapa nchini siku hadi siku bila wao kutamka neno lolote kama wanavyofanya kwa Zimbabwe, Myanmar na kwingineko.

Wanafahamu pia wizi wa kura na chaguzi zisizozingatia sheria na haki, lakini pia wako kimya, badala yake wanasifia uhusiano "mzuri" baina ya nchi hizi mbili huku wakitoa tuzo za Martin Luther King.

Lakini ukiangalia kwa karibu unakuta kuwa wamekaa kimya kwa sababu Kikwete (Muzungu worshipper) ni kibaraka wao mkubwa sana; hakuna analowabishi, kila kitu anawakubalia na kuwachekea tu, pengine haelewi Kiingereza chao kutokana na lafudhi ya Kimarekani inavyofunika maneno kwenye matamshi.

Hali ilivyo sasa hapa nchini ni sawa na nchi zingine nyingi, lakini kutokana na favours wanazozipata hawaikemei wala kuitisha serikali hii huku maisha ya raia wasio na hatia yakipukutishwa na risasi za polisi wapumbavu.

Serikali inajua kuwa haiwezi kubanwa na Wamarekani ndiyo maana uhuni na unyama unaongezeka siku hadi siku.
Itakapotokea msala unaanzishwa na wananchi wenye hasira, hebu Wamarekani wasisahaulike ili wajifunze ubaya wa unafiki.
 
Japo sikubaliani na ulilolisema kuhusu Rais wetu na unafiki wa Marekani, mimi nitakutetea hadi tone la misho wa jasho langu la uhuru wako wa kusema.
 
lahi yao kwanza kuna Rais dikteta kama Museveni lakini kwa sababu ni kibaraka wao wako kimya kumbuka kuhusu Charles Tayrol,Mobutu hata Savimbi ukweli rais wetu anapendwa sababu ni kibaraka wao
 
jk yuko potepote...mara kwa obama mara kwa cameron...sijui hawa wazungu wanampa nini au sijui jk anawapa nini? hatulii...!
 
Tanzania chini ya Kikwee ni sawa na Israel: it can do anything with impunity!
 
Marekani hawana permanent friends. Only permanent interests. Kikwete is the best president for American interests tangu tupate uhuru wetu. Go figure!
 
Marekani hawana permanent friends. Only permanent interests. Kikwete is the best president for American interests tangu tupate uhuru wetu. Go figure!

Hakuna namna kwa sasa hakuna kiongozi ambaye si best wa US..

Akiwemo kwa africa labda mugabe (almost done)..

After all asingekuwa kuwa rais na US chadema wangeshachukua nchi kwa kujipendekeza kwao..

Nawashauri chadema muwe rafiki na Russia na Iran...lol
 
Hakuna namna kwa sasa hakuna kiongozi ambaye si best wa US..

Akiwemo kwa africa labda mugabe (almost done)..

After all asingekuwa kuwa rais na US chadema wangeshachukua nchi kwa kujipendekeza kwao..

Nawashauri chadema muwe rafiki na Russia na Iran...lol
Soma ile ripoti ya Wikileaks jinsi alivyoliuza jeshi letu kwa Wamarekani akishirikiana na Kapuya. It is nothing to be proud of.
 
Marekani hawana permanent friends. Only permanent interests. Kikwete is the best president for American interests tangu tupate uhuru wetu. Go figure!


Usiwe na wasiwasi Mkulu. Tunajenga community hapa na baadaye tutaanza ku-lobby kwa maslahi ya watanzania.
 
Maisha yenu watanzania yataendelea kuwa kitendawili hadi mtakapoacha ushabiki wa Yanga na Simba katika siasa! Dhiki na mahangaiko mnayataka wenyewe! Hakuna sababu ya kuilaumu serikali bali wananchi mjilaumu wenyewe. Kumbukeni hiyo serikali haikuingia msituni na kutwaa madaraka!

Mlipiga kura kwa ushabiki wenu wenyewe! Ugumu wa maisha unaoendelea kwa sasa ni kwa ridhaa yenu wenyewe! Hayo ndiyo matokeo ya rushwa ya chumvi na vikofia vya kijani. Poleni sana!! Bila mang'amuzi, safari bado ni ndefu!
 
huu urafiki mkubwa wa taifa letu na marekani umeanzaje kuna nini baba mwanaacha.
 
Back
Top Bottom