Unafiki wa balozi wa Kenya Tanzania

Ndugu TX,
Kufuta ulichobandika hapa, ambacho ndicho kinachofanyiwa rejea na wachangiaji siyo ustaarabu maana wachangiaji wanaonekana wazushi!
Rudisha, au omba Mods wafunge mjadala huu.

Mtoa Hoja hapo juu "yako" kaiweka hio article.....au kuna mengine....? Next time mtoa Mada bado akiweka bandiko unachotakiwa ni kumquote..hata kama akifuta qoutation yako itabakia reference...!!!
 
Ndugu yangu,
Nadhani tunachanganya mambo hapa.
1. Kichwa cha habari kinasema "Unafiki wa balozi wa KEnya tz"...Ukisoma mada unashangaa, badala ya kuona unafiki, unaona mtu anatoa ushauri wake kuwa, mkitaka kuanzisha mfanye homework yenu vizuri kwa maana wao ambao tayari wanazo, wanaona changamoto zinazowakabili.
2. Ulishawahi kusikia " best/good practices" that needs to be replicated? Kama jibu ni ndio, basi utakubaliana nami kuwa hakuna haja ya kufanya makosa pale mwenzio alishayafanya.Unachotakiwa ni kuchunguza alikosea nini na wapi na wewe uanzishe chako kwa kurekebisha yale makosa na siyo kuyarudia vilevile.
3. Inashangaza unaingiza udini hata mahali ambapo sio pake.Waraka - ambao ni mawazo ya kundi fulani katika jamii kuhusu suala fulani ambalo hata kikatiba watu wana uhuru kutoa mawazo yao, haifanani na kuanzisha taasis ndani ya mfumo wa serikali ambao watu wa imani zote watawajibika kugharamia kwa njia ya kodi zao.jARIBU KUTOFAUTISHA NDUGU.
4. Usihukumu watu kwa misingi ya dini kwa maana utashangaa utawabandika watu dini ambazo siyo zao!

Shangazi, nimekuelewa. Lakini naomba kukuuliza, kama hili la mahakama ya kadhi kinachosumbua ni kodi. Vipi mkataba wa Serikali na Makanisa ambapo Serikali itatoa fedha na upendeleo kwa kusomesha Wakristo, pia itatoa fedha ama kukopa kwa niaba ya Wakristo kwa ajili waendeshe shule na hospitali. Jee hapo ni sawa?.

Pili, mimi nazungumza ama naandika kile ninachosoma. Kama wewe unaniona mdini, haiwezekani wewe usiwe mdini. Manake unatumia kipimo gani kuniona mdini, wewe usiwe na chembe ya udini katika moyo wako. Kuhukumu nitahukumu, hili suala limehusu dini, unataka niseme kuwa hapa kuna ukabila wakati ni udini.
 
Hivi akitokea Balozi wa Msumbiji ama Rwanda, akatoa ushauri wa ubaya wa Waraka wa Kanisa Katoliki kutakalika. Hayo hayatokuwa mawazo yake bali itaonekana ni kuingilia masuala ya nchi. Lakini huyu kwa kuwa yuko upande wa Wakristo, ahh anaonekana kasema.

Kwani kasema mahakama ya kadhi isiwepo au kasema swala liangaliwe kwa undani zaidi?
 
Hivi jamani humu JF haina mambo mengine ya kuchangia ya kutuletea maendeleo kwa kasi ni mambo ya Udini tuuuu yanachangamkiwa badala ya kuhamasisha maendeleo ya shule, barabara, Umaskini uliokithiri ukitawala???? Tuache udini
 
hakuna pesa yoyote ile ambayo selikali inawapa shule. na shule zenyewe hata selikali ingetoa wanasoma watu wa dini zote including waislam. pia hata kama ingekuwa hivyo, waislam pia wangekuwa na uhuru wa kujenga mashule yao ili wapate nao. zaidi ya yote, hata kama waliingia, wana haki kwasababu mashule yao yalinyang'anywa ili tuchukuliane na watu waliokuwa illiterate kwa kiwango kikubwa. nina maana, tuligawana umasikini au ujinga ili tusome wote. isingekuwa hivyo, basi, wakristo tu ndo wangekuwa wamesoma hadi leo. wengine wangekuwa wafanyabiashara za samaki wa feri wakikaa mbagala, manzese na magomeni. tulifanya hivyo kuwasaidia tu.shukrani hamna?
 
Huyu Mfumwa kweli mfu--------we ulitaka aseme anzisheni mahakama ya kadhi ndo ufurahi? aaahahahahaah! haitatokea hiyo mahakama hata iweje kamanda, we endelea kuchapa kazi badala ya kupoteza muda wako kwa vitu visivo na msingi wowote.

Eti mahakama ya kadhi!!!-----------what is that??????

Rom
 
mahakama kama hizi zimeshashindwa huko kenya, zinawaletea kichefuchefu na usumbufu, wanajuta kwanini walianzisha. ni bora ametoa ushauri ili watu waelewe, tusiingie kichwa kichwa.

Wakishindwa waKenya sisi kwanini tusiweze? hii ndo misimamo fubavu
 
hakuna pesa yoyote ile ambayo selikali inawapa shule. na shule zenyewe hata selikali ingetoa wanasoma watu wa dini zote including waislam. pia hata kama ingekuwa hivyo, waislam pia wangekuwa na uhuru wa kujenga mashule yao ili wapate nao. zaidi ya yote, hata kama waliingia, wana haki kwasababu mashule yao yalinyang'anywa ili tuchukuliane na watu waliokuwa illiterate kwa kiwango kikubwa. nina maana, tuligawana umasikini au ujinga ili tusome wote. isingekuwa hivyo, basi, wakristo tu ndo wangekuwa wamesoma hadi leo. wengine wangekuwa wafanyabiashara za samaki wa feri wakikaa mbagala, manzese na magomeni. tulifanya hivyo kuwasaidia tu.shukrani hamna?
Kwa akili zako unafikiria kuwa hakukuwa na shule za Kiislam zilizo taifishwa!? Hivi mpala leo bado upo na ile ile propaganda ya "hawakusoma hao"
Nyie mlio soma mmelifikisha wapi Taifa hili, kila kukicha linanuka umaskini wa kutupwa? Unataka kunambia kuwa nyie wasomi (!?) Ndipo mlipoifikisha Tanzania hapa tulipo, yaani mnajivunia ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.
 
mahakama kama hizi zimeshashindwa huko kenya, zinawaletea kichefuchefu na usumbufu, wanajuta kwanini walianzisha. ni bora ametoa ushauri ili watu waelewe, tusiingie kichwa kichwa.

Wakishindwa waKenya sisi kwanini tusiweze? hii ndo misimamo fubavu

Haja sema Tanzania itashindwa. Yeye kasema kutokana na experience ya Kenya ni bora na Tanzania tuka liangalia vizuri jambo hili. Kwa hiyo usiweke maneno mdomoni mwake mkuu.
 
Kazi kweli kweli, mtu katoa ushauri unachotakiwa kufanya ni kuusikiliza na kuupima kama unafaa au haufai kumuita mnafiki hakutobadilisha chochote sana sana kunaonyesha jinsi uelewa wako wa mambo ulivyo mdogo. SMH!
 
Hivi akitokea Balozi wa Msumbiji ama Rwanda, akatoa ushauri wa ubaya wa Waraka wa Kanisa Katoliki kutakalika. Hayo hayatokuwa mawazo yake bali itaonekana ni kuingilia masuala ya nchi. Lakini huyu kwa kuwa yuko upande wa Wakristo, ahh anaonekana kasema.

,....TUACHE USHABIKI,TUONGEE UKWELI.
KWA MUJIBU MAGAZETI NILIYOSOMA NI KWAMBA BALOZI HUYO ALISEMA MAHAKAMA HIZO ZINALETA KERO HUKO KWAO NA AKASHAURI UMAKINI UWEPO KTK KUJADILI NA KUAMUA KAMA IWEPO AU LA.
Waraka wa MADHEHEBU YA KIKRISTO MBONA UNAJADILIWA NA KILA MTU ANATOA MAONI YAKE NA BADO PANAKALIKA?
Cha msingi kwakuwa wanaotaka mahakama hiyo wapo,waitetee hoja yao na wanaopinga waraka wa wakrito watoe hoja na WAUMINI WAELIMISHWE KUSUDIO NA NAMNA YA KUTEKELEZA MAAZIMIO YATAKAYO FIKIWA.
Ahsante sana
 
Back
Top Bottom