Unafiki tulio nao kuhusu kaluzi za ushoga toka Uingereza!

kuti kavu

Member
Feb 25, 2009
68
21
...Nimekua nikifuatilia kisemwacho na waTanzania wenzangu pamoja na viongozi wetu kuhusu kauli ya Uingereza kuwa ni sharti kukubali kuwatambua mashoga ama sivyo misaada wanayotupa wataiondoa. Asilimia kubwa ya waTanzania wameonesha jazba juuu ya hili wakiwemo viongozi wetu LAKINI:

WOte tunajua kuwa vitendo vya kishoga vimekuwa vikifanyika hapa nnchini na mara kadhaa wazi wazi. Mara ngapi magazeti ya UDAKU yameweka ukurasa wa mbele watu wakifanya vitendo vya kishoga?. Wiki chache zilizopita CLOUDS FM waliita shoga na kumuhoji mchana kweupe na alikiri kufanya ushoga na kuwa anasomesha watoto wa kazi hiyo. Viongozi wetu wanalijua hili, waTanzania tunalijua hili lakini hata mara moja sikusikia vyombo husika kulipigia kelele hili kwa uzito unaotakiwa.

LEO hii mara baada ya Uingereza kutaka kutuburuta kuwa tuukubali utamaduni huu wa kifedhuli ndo KIONGOZI ANASEMA USHOGA HAUKUBALIKI NA TUKIMKAMATA ATAFUNGWA MIAKA 30 KAMA SHERIA INAVYOSEMA.

HEBU TUJIULIZE SHOGA WA MWISHO KUFUNGWA MIAKA 30 ALIKUWA NANI? HUYO ALIYEHOJIWA REDIONI NA KUKIRI USHOGA ALICHUKULIWA HATUA GANI? HAO WANOTOLEWA MAGEZETINI WAKIFANYA VITENDO HIVI WALICHUKULIWA HATUA GANI?

Nionavyo mimi asilimia kubwa ya kauli zinazotolewa ni UNAFIKI TU!!! na kutafuta umaarufu wa kisiasa.... Ni sawa na kuwa na mtoto wako mwizi halafu huchukui hatua lakini akitokea jirani na kukuambia uitambue na kuikubali tabia ya wizi aliyonayo mwanao unaanza KUHAMAKI!!!
 
Nani asietambua kuwa Tz kama zilivyo nchi nyingine za Afrika vitendo vya ushoga vipo? Na ni dhahiri kabisa ni ushenzi, uchafu na kinyume kabisa na maadili ya Mungu, na utamaduni wetu.
Daudi kameruni anataka tuhalalishe ufedhuli huu na uandikwe kwenye vitabu vyetu kuwa ni haki ya binadamu.. Watu tunapopingana nae, wewe unadai eti umekuwa ukifuatilia hoja za hizi na kuuita unafiki! Mi nadhani huu si unafiki ni sawa kabisa kukataa na kuendelea kukataa. Shida ni kwamba hapa bongo sheria hazifuatwi na ndio maana hao mashoga unaona wanaranda mitaani na kufanya takataka zao bila kuchukuliwa hatua za kisheria.
Ungana na wazalendo kupinga hiyo kadhia usiite unafiki ipo siku kitaeleweka tu..
 
Jaribu kufika magomeni mtaa wa chidya. huko kuna mashoga kama wanawake.
 
Hapa tunapiga kelele tu. Kama Dav na wenzake wakikomalia kauli yao, sheria ya kuhalalisha upuuzi huu hapa Bongo itawekwa tu. Na hii ndiyo gharama ya kuwa ombaomba. Kumbuka yaliyotokea Uganda, Malawi n.k.
 
Cha msingi tukatae kwanza kwa nguvu zote kisha tuangalie namna ya kufanyia kazi sheria husika tusitumie mapungufu yetu kuharalisha huu uozo
 
Tumsikilize Mungu tu, na siyo binadamu tusije tukapata laana isiyo na ulazima wa kupata!

Mungu pekee ndo solution kamili na siyo binadamu!
 
Back
Top Bottom