Unadhani ingekuwaje kama ingekuwa ni unapata stahili yako on the spot.

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
12,037
24,595
......kama tukitenda dhambi tungekuwa tunapata adhabu hapo hapo, kwa mfano ile unamaliza kuwaza uovu wako tu, unastukia unanyukwa makofi, makonzi na mitama mfululizo huku akupigae humuoni.
Unadhani status ya uovu ingekuwa vp?
 
hahaha nahisi watu wangekuwa na makovu ya kunyukwa lol uovu ungekuwa mchache.
 
Ha ha ha ha haaah!!! Nimecheka sana baada ya kusoma hapa.....
Nadhani wengine wangekufa kabisa...
 
unarudi nyumani una manundu na vumbi mwilini, nguo zimechafuka, watoto wanakwambia "mama/baba ulikuwa unawaza mambo mabaya eeh!"
mume/mke naye anaku tight "yaani wewe kila siku kuadhibiwa tu, sasa leo utanieleza hayo uyawazayo kila siku."
 
Ha ha ha ha haaah!!! Nimecheka sana baada ya kusoma hapa.....
Nadhani wengine wangekufa kabisa...
umesimama kwenye public na upo serious na watu wanakuona mtu wa maana...ghafla wanasikia mtu ananyukwa makofi, wanageuka waangalie wanakuona mtu mzima tayari umepigwa mtama na upo kimo cha ndama ukiwa safarini kwenda ardhini, unafika kama gunia...watu wote wanakuangalia, mzee unainuka huku unaona ona noma, unajifuta vumbi huku vimachozi vinakulengalenga kwa mbaali...then unaongea kwa kuona soo "....naonewa tu"
mwisho watu wakiondoka unalia kwa sauti ili kupunguza machungu ...
 
hahaha nahisi watu wangekuwa na makovu ya kunyukwa lol uovu ungekuwa mchache.
Au tungekuwa tuna vaa helmet na manguo kama wale wanaanga. Sijui na mitamama tungeikwepaje? Au binaadam tungegundua lami/barabara zenye magodoro
 
umesimama kwenye public na upo serious na watu wanakuona mtu wa maana...ghafla wanasikia mtu ananyukwa makofi, wanageuka waangalie wanakuona mtu mzima tayari umepigwa mtama na upo kimo cha ndama ukiwa safarini kwenda ardhini, unafika kama gunia...watu wote wanakuangalia, mzee unainuka huku unaona ona noma, unajifuta vumbi huku vimachozi vinakulengalenga kwa mbaali...then unaongea kwa kuona soo "....naonewa tu"
mwisho watu wakiondoka unalia kwa sauti ili kupunguza machungu ...

Nimecheka hadi machozi yamenitoka...lol !
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom