Unadhani Filiku-Njombe anastahili wadhifa gani?

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,145
13,216
Huyu jamaa ameonesha ujasiri sana na ukomavu wa KISI-HASA, mimi nisingePenda apewe wadhifa wowote maana nitamkosa sana katika kuikosoa serikali ya chama chake, nakumbuka jinsi Mwanri, Pinda, Mwakyembe, Manyanya, Kasaka, na wengineo walivyokuwa wanaichachafya serikali lakini ONA SASA baada ya kupewa kisu na umma nao WAIKATE KEKI........
 
sasa kwa nini tumpe cheo wakati kazi aliyonayo ni inamfaa zaidi? watz bwana vyeo vya nini sasa namna hii, tunahitaji filikunjombe zaidi bungeni pale, bunge ni mhimili muhimu sana, uwaziri hautamfanya mtu awe makini ukichukulia kanuni ya kuwajibika kwa pamoja huyu ataonekana popote pale. he is effective where he is.

kama tukiwa tunafikiria kuwazawadia wakuu wa mikoa, wa wilaya, wabunge nk doketi za uwaziri basi tunataka kuitukuza executive branch katika balance of power ya demokrasia yetu. na hiki ni kitu kibaya kwani hata hawa wanasiasa watakua ni povu la bia tu kila siku, kujifanya wanachachafya serikali ili wapewe wizara..sana sana apewe kamati fulani ya bunge na si zaidi
 
Mi naona abaki mwakirishi wa wananchi hiyo ndo inamfaa, labda awepo kwenye kamati watchdogs,
 
Kumbe kelele zote hizo anatafuta cheo!
sidhani ni kutafuta cheo bali kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili watanzania kwa kusababishwa na kundi fulani dogo tu la watu.......
 
au mnataka kumuenzi baada ya kupata Brain Concussion?
 
hivi kwa wakati huu na serikali hii kuna nafasi nzuri na ya uhuru zaidi kama ubunge.? Kama mnaona uwaziri mzuri muulizeni mwakyembe.
 
Hata kama anatafuta cheo, tunampa maana kaonesha anaweza kusimamia maslahi ya nchi. sasa hao tuliowapa vyeo muda wote huo wanaonesha uwezo gani? kuiba?? ehhh wizi wa mali zetu, heri apewe Fili atatusaidia kwa kiasi fulani hata kama sio 100%
 
Mtoa hoja nadhani katumwa na Filikunjombe,hivi kweli uongozi leo ni zawadi.nadhani umepotea.filikunjombe hapo amejaribu kutimiza majukumu yake na si zaidi tuwe na mawazo chanya
 
Back
Top Bottom