Una ufahamu gani juu ya Shamba 17 (Farm 17) la Wilaya ya Nachingwea?

atirbac

New Member
Jul 18, 2014
3
0
Hamjambo? Mimi ni raia wa Msumbiji na ninafanya utafiti kuhusu asili ya Shamba 17 la Wilaya ya Nachingwea.

Ninaelewa kuwa baada ya Vita vya Pili vya Dunia, Uingereza ilitenga Shamba 17, ikiwa moja ya mashamba 21 (au, 20 kulingana na vyanzo vingine), kwa wapiganaji wastaafu wa vita hivyo ambao wangependelea kushiriki miradi ya kilimo.

Ningependa kujua:

a) Maagizo kamili ya kikoloni kuhusu kuanzishwa kwa mashamba 21 (au 20) Wilaya ya Nachingwea.

b) Idadi ya askari waliokuwa kwenye mashamba hayo.

c) Kila shamba lilikuwa na ukubwa gani.

d) Aina ya kilimo, kanuni na masharti.

e) Ikichukuliwa maanani kwamba Shamba 17 lilipewa Frelimo na vikundi vingine vya ukombozi kutoka kusini mwa Afrika 1965, lilifungwa lini kama mradi wa kilimo?

f) Ilitokea nini kwa mashamba hayo?

Asanteni sana kwa msaada wenu katika jambo hili.

========

Baadhi ya Michango ya WanaJamiiForums..

jengo_samora.jpg
Jengo ambalo alikuwa anaishi Samora Machel.

KILOMETA zipatazo 34 kutoka makao makuu ya wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi, lipo eneo maarufu linalojulika kama Farm 17.

Katika eneo hili hivi sasa kuna shule ya Sekondari iliyoazishwa na wananchi kama hatua ya kuyaokoa majengo ambayo yametelekezwa kwa muda mrefu, hivyo kugeuka kuwa makazi ya wanyama wadogowadogo na kuzongwa na vichaka.

Ni makazi ya waliokuwa wapigania uhuru katika nchi za Kusini mwa Afrika, zikiwamo Msumbiji, Angola na Afrika ya Kusini ambazo kwa miaka kadhaa zilihenyeshwa na Makaburu waliokuwa wakiendesha siasa za ubaguzi wa rangi, pia Zimbabwe ambayo olikuwa chini ya utawala wa Waingereza hadi 1980 ilipopata uhuru wake.

Hapa ni mahali walipowahi kuishi wapiganaji wa vita ya ukombozi wakiwamo Rais wa sasa wa Zimbabwe, Robert Mugabe na viongozi wawili wa Msumbiji ambao wote ni marehemu kwa sasa, Edward Modline na mrithi wake, Samora Machel.

Kwa maana hiyo, unapozungumzia harakati za uhuru au ukombozi Kusini mwa Afrika ambazo kwa kiasi kikubwa ziliongozwa na Tanzania chini ya Hayati Mwalimu Nyerere, huwezi kukosa kutaja wilaya ya Nachingwea, hususan eneo la Farm 17.

Hali ilivyo

Hata hivyo eneo hili licha ya kuwa sehemu ya historia hii muhimu ya Bara la Afrika, ni kama limetelekezwa na laity kama siyo busara ya wakazi wa Nachingwea kuligeuza kuwa kitovu cha elimu kwa kuanzisha shule ya Sekondari, basi lingeweza kufutika.

"Naamini kama Samora na Nyerere wangekuwa hai eneo hili lisingeachwa hivi kwani wangelithamini na kulienzi," anasema mmoja wa wananchi wanaoioshi pembezoni mwa Farm 17.

Kauli hiyo ni kati ya kauli nyingi zinazotolewa na watu ambao wanaonekana kukatishwa tama na hali ilivyo katika eneo la Farm 17, kutokana na kutoeziwa ipasavyo.

Wakazi hawa wa Lindi na hasa wale wa wilayani Nachingwea baadhi yao wanakumbuka walivyoishi kwa wasiwasi wa kushambuliwa na Makaburu, ambao wakati wote walikuwa wakiwasaka wapiganaji wa vita ya ukombozi.

Hivyo kutelelezwa kwa majengo yaliyokuwa makazi ya viongozi wakuu wa nchi, kuliwafanya wapate mawazo ya kuyatumia kwa ajili ya kuanzisha shule ya Sekondari kupitia uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea.

Viogozi wanena

Mkuu wa shule ya Sekondari hiyo ya ya Farm 17, Longinus Nambole anasema eneo hilo kwa sasa linapata uhai kwa kuwa kuna shule.

Hata anasema baadhi ya viongozi wa nchi ambazo wakuu wake waliwahi kuishi hapo, wamekuwa wakifika na kutoa ahadi mbalimbali za kulifanyia marekebisho lakini ahadi hizo hazijatekelezwa hadi sasa.

"Hata Serikali yetu ya Tanzania haionyeshi kama hili ni eneo muhimu maana hakuna jitihada zozote zinazofanyika kutunza majengo haya,"alisema Nambole.

Nambole anasema Wizara ya Maliasili na Utalii, pia iliwahi kuaihidi kwamba ingeliendeleza eno hilo ili kulinda historia yake lakini ahadi hiyo haijatekelezwa hadi sasa.

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo yeye anasema hali ya majengo hasa lile alimokuwa akiishi Marehemu Machel ni mbaya kwani yemeanza kubomoka hasa barabara ya chini ya ardhi ambayo inahitaji kufanyiwa ukarabati mkubwa.

Chonjo anasema katika njia hiyo ya chini kwa chini, ukarabati unaopaswa kufanyika ni kuweka umeme na taa kuanzia kwenye nyumba hadi lilipo handaki ambako alikuwa akijificha Machel.

"Tunakiomba kitengo cha mambo ya kale kukarabati lile jengo na kusafisha pango na kuweka taa ili kuvuta watalii, kama tukipaendeleza tunaweza kupata watalii wengi ambao naamini wanapenda kuona sehemu hii,"anasema Chonjo.

Aidha mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa kupitia halmashauri ameigiza kutenga kiasi cha fedha kwenye bajeti yake ili kutengeneza eneo hilo wakati wakisubiri wizara husika kuliendeleza.

Mkazi wa kijiji cha Farm 17 Judith Bathromeo alisema kuwa iwapo eneo hilo litaboreshwa, litazalisha ajira kwa wananchi wa kijiji hicho kwani lingevuta watalii kutoka maeneo mbalimbali Duniani na pia kuchangia pato la taifa.

"Tunashangaa watu kila siku tunalia ajira hakuna, ajira hakuna, maisha magumu kama hapa wangepatengeneza ingekuwa nafasi ya wengi wetu kujipatia ajira, lakini ndiyo hivyo kama unavyoona hakuna jitihada yeyote ya kulienzi eneo hili,"alisema Balthoromoe.

Alidai kuwa mabalozi na viongozi ambao waliwahi kutembelea eneo hilo na kuahidi kusaidia ukarabati wake ni Balozi wa Msumbiji nchini, Jose Rui Amaral wa Msumbiji, aliyekuwa Balozi wa Zimbabwe nchini, Chipo Zindoga, Waziri Mkuu wa Msumbiji Carlos Cassa na Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo, Josenio Henriques.

Hata hivyo Balthoromeo anasema ahadi hizo hazijawahi kutekelezwa.

Afisa mtendaji wa kijiji cha Farm 17 Juma Alli alisema kuwa serikali ya kijiji hicho imejiwekea mikakati ya kulinda na kuheshimu mipaka ya maeneo kwa kutofanya shughuli za zozote za kibinadamu.

Historia ya Farm 17

Eneo la Farm 17 lipo umbali kilometa zipatazo 34 nje kidogo ya makao makuu ya wilaya ya Nachingwea, barabara inayoelekea Kilimarondo, ikipakana na wilaya ya Masasi.

Wapigania uhuru wa nchi za Msumbiji, Zimbabwe, Angola na Afrika ya Kusini walipata mafunzo na mbinu za kupambana na wakoloni na makaburu hadi nchi zao zilipofanikiwa kupata uhuru.

Waliacha majengo mbalimbali ya kihistoria likiwemo jengo alilokuwa anaishi Rais wa Msumbiji Marehemu Machael ambalo lilikuwa na njia ya chini ya ardhi yenye urefu wa kilometa zipatazo kumi.

Njia hii inaazia kwenye jengo hilo hadi kwenye handaki ambalo linasemekana ndipo alipokuwa anaishi, kisha kuendelea hadi kwenye uwanja mdogo wa ndege ambao alikuwa anautumia pale alipokuwa akisafiri.

Historia ya Farm 17 inaanzia miaka ya 1947 baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, wakati Serikali ya wakoloni wa Uingereza iliamua kufuta baadhi ya ajira kwa waliokuwa askari wa vita hyo na kuamua kuwatafutia ajira mbadala.

Serikali hiyo ya wakoloni iliamua kuwatafutia ajira kwa kuwakopesha wapiganaji hao fedha na kuanzisha mashamba ya karanga katika maeneo ya Nachingwea kupitia kampuni ya John Molem.

Kupitia mpango huo mashamba 18 yalianzishwa yakipewa majina kuanzia mashamba kuanzia Farm one hadi Farm 18. Hata hivyo kutokana na sababu mbalimbali mashamba hayo hayakuendelea na Waingereza hao kuamua kuondoka na kwenda kuishi Afrika ya Kusini.

Baada ya Tanganyika kupata uhuru Desemba 9, 1961 Serikali iliamua kutumia eneo la Farm 17 kuwa kituo cha kufundishia wapigania uhuru wa nchi zilizo Kusini mwa Afrika.

Viongozi mbalimbali wapigania uhuru katika nchi hizo wakiwamo Komredi Mondlane, Komredi Machel na Komred Mugabe waliishi kwa kujificha na kupewa mbinu mbalimbali, hivyo walichana kumbukumbu ambazo ni muhimu kwa historia ya ukombozi wa Afrika.

Baada ya nchi hizo kufanikiwa kujipatia uhuru eneo hilo lilikabidhiwa kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kikosi cha 41, baadaye wanajeshi hao waliondoka.

Hatua ya JWTZ kuondoka ilitoa mwanya wa majengo hayo kuhujumiwa kwani watu wasiofahamika walianza kuiba baadhi ya vifaa ikiwa ni pamoja na kung'oa mabati, huku eneo hilo likizungukwa na msitu mnene.

=======

FARM 17: AN IMPORTANT ICON OF LIBERATION STRUGGLE IN SOUTHERN AFRICA

Kennedy Kisula

THIRTY kilometres from Nachingwea Township in Lindi region lies an important icon for the liberation struggle in Southern African countries. The place is called Farm 17.

The buildings at the estate which are now housing Farm 17 Secondary School were once occupied by freedom fighters from Southern African countries. Notable among prominent leaders who used to stay at Farm 17 include founding President of Mozambique, Mr Samora Machel as well as the first President of Zimbabwe, Mr Robert Mugabe.

The farm remains one of important features for freedom fighters who were hosted by Tanzania under the leadership of the founding President of Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere. Samora Machel is said to be among leaders who stayed at Farm 17 for a very long as he mobilized fellow freedom fighters until Mozambique gained her independence from Portugal in 1975.

The founding Headmaster of Farm 17 Secondary School who is now the head of Nachingwea Secondary School complains, Mr Longinus Nambole, however that buildings at they are falling into ruin despite its great legacy in liberation struggle for southern African countries. Originally, Farm 17 was groundnut growing scheme by British colonialists in the failed Tanganyika groundnut scheme in late 1940’s.

Farm 17 was later used as a camp by FRELIMO during Mozambique national liberation struggles and later as a training base for freedom fighters from Zimbabwe, Angola and South Africa. With abandoned two-kilometre long dugout used by Samora Machel and his crew, the dilapidated house is currently serving as quarters for Farm 17 Secondary School members of staff.

The Headmaster of Farm 17 Secondary School, Zakaria Budimu said the school tries to take care of the building but had no budget for its renovation. “As a school we have no plans for renovation as we don’t budget for that.

That (renovation) requires a lot of money. What we do is to take care of it,” he explained during an interview with journalists from the Tanzania Standard (Newspapers) Limited (TSN). The educator urged the government to renovate the building and develop the area so as to attract tourists. “The government should do something to renovate the house and the dugout. It should make arrangements to develop this place,” he said.

The Chairman of Nachingwea District Council, Ahmed Mr Salum Makoroganya, earlier said every year the Mozambique Ambassador in Tanzania, embassy officials and some Mozambique nationals visit the area.

He said they were planning to promote the place and receive a significant number of Mozambique people who resided in Nachingwea during their independence struggles. He said they were expecting students from Nachingwea University opened in Mozambique to visit the place to learn about independence struggle by FRELIMO freedom fighters.

The University takes its Farm 17: An important icon of liberation struggle in Southern Africa name from the main political-military centre in Nachingwea where FRELIMO trained its guerrilla army during the war for Mozambique’s independence from Portuguese colonial rule. Given its history, residents explained that some of freedom fighters sired children with sired Tanzanian women.

As such there are children who are now adults whose fathers came from Mozambique, Angola, Botswana, South Africa and South Africa.
72ab14cf543c481b042101d30af77321.PNG

President Julius Nyerere of Tanzania (right) is flanked by his counterparts Samora Machel of Mozambique (centre) and Kenneth Kaunda of Zambia (left) at FRELIMO training camp, Farm 17, in Nachingwea, Lindi Region of Tanzania in 1972
 
jengo_samora.jpg

Jengo ambalo alikuwa anaishi Samora Machel.

KILOMETA zipatazo 34 kutoka makao makuu ya wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi, lipo eneo maarufu linalojulika kama Farm 17.

Katika eneo hili hivi sasa kuna shule ya Sekondari iliyoazishwa na wananchi kama hatua ya kuyaokoa majengo ambayo yametelekezwa kwa muda mrefu, hivyo kugeuka kuwa makazi ya wanyama wadogowadogo na kuzongwa na vichaka.

Ni makazi ya waliokuwa wapigania uhuru katika nchi za Kusini mwa Afrika, zikiwamo Msumbiji, Angola na Afrika ya Kusini ambazo kwa miaka kadhaa zilihenyeshwa na Makaburu waliokuwa wakiendesha siasa za ubaguzi wa rangi, pia Zimbabwe ambayo olikuwa chini ya utawala wa Waingereza hadi 1980 ilipopata uhuru wake.

Hapa ni mahali walipowahi kuishi wapiganaji wa vita ya ukombozi wakiwamo Rais wa sasa wa Zimbabwe, Robert Mugabe na viongozi wawili wa Msumbiji ambao wote ni marehemu kwa sasa, Edward Modline na mrithi wake, Samora Machel.

Kwa maana hiyo, unapozungumzia harakati za uhuru au ukombozi Kusini mwa Afrika ambazo kwa kiasi kikubwa ziliongozwa na Tanzania chini ya Hayati Mwalimu Nyerere, huwezi kukosa kutaja wilaya ya Nachingwea, hususan eneo la Farm 17.

Hali ilivyo

Hata hivyo eneo hili licha ya kuwa sehemu ya historia hii muhimu ya Bara la Afrika, ni kama limetelekezwa na laity kama siyo busara ya wakazi wa Nachingwea kuligeuza kuwa kitovu cha elimu kwa kuanzisha shule ya Sekondari, basi lingeweza kufutika.

"Naamini kama Samora na Nyerere wangekuwa hai eneo hili lisingeachwa hivi kwani wangelithamini na kulienzi," anasema mmoja wa wananchi wanaoioshi pembezoni mwa Farm 17.

Kauli hiyo ni kati ya kauli nyingi zinazotolewa na watu ambao wanaonekana kukatishwa tama na hali ilivyo katika eneo la Farm 17, kutokana na kutoeziwa ipasavyo.

Wakazi hawa wa Lindi na hasa wale wa wilayani Nachingwea baadhi yao wanakumbuka walivyoishi kwa wasiwasi wa kushambuliwa na Makaburu, ambao wakati wote walikuwa wakiwasaka wapiganaji wa vita ya ukombozi.

Hivyo kutelelezwa kwa majengo yaliyokuwa makazi ya viongozi wakuu wa nchi, kuliwafanya wapate mawazo ya kuyatumia kwa ajili ya kuanzisha shule ya Sekondari kupitia uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea.

Viogozi wanena

Mkuu wa shule ya Sekondari hiyo ya ya Farm 17, Longinus Nambole anasema eneo hilo kwa sasa linapata uhai kwa kuwa kuna shule.

Hata anasema baadhi ya viongozi wa nchi ambazo wakuu wake waliwahi kuishi hapo, wamekuwa wakifika na kutoa ahadi mbalimbali za kulifanyia marekebisho lakini ahadi hizo hazijatekelezwa hadi sasa.

"Hata Serikali yetu ya Tanzania haionyeshi kama hili ni eneo muhimu maana hakuna jitihada zozote zinazofanyika kutunza majengo haya,"alisema Nambole.

Nambole anasema Wizara ya Maliasili na Utalii, pia iliwahi kuaihidi kwamba ingeliendeleza eno hilo ili kulinda historia yake lakini ahadi hiyo haijatekelezwa hadi sasa.

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo yeye anasema hali ya majengo hasa lile alimokuwa akiishi Marehemu Machel ni mbaya kwani yemeanza kubomoka hasa barabara ya chini ya ardhi ambayo inahitaji kufanyiwa ukarabati mkubwa.

Chonjo anasema katika njia hiyo ya chini kwa chini, ukarabati unaopaswa kufanyika ni kuweka umeme na taa kuanzia kwenye nyumba hadi lilipo handaki ambako alikuwa akijificha Machel.

"Tunakiomba kitengo cha mambo ya kale kukarabati lile jengo na kusafisha pango na kuweka taa ili kuvuta watalii, kama tukipaendeleza tunaweza kupata watalii wengi ambao naamini wanapenda kuona sehemu hii,"anasema Chonjo.

Aidha mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa kupitia halmashauri ameigiza kutenga kiasi cha fedha kwenye bajeti yake ili kutengeneza eneo hilo wakati wakisubiri wizara husika kuliendeleza.

Mkazi wa kijiji cha Farm 17 Judith Bathromeo alisema kuwa iwapo eneo hilo litaboreshwa, litazalisha ajira kwa wananchi wa kijiji hicho kwani lingevuta watalii kutoka maeneo mbalimbali Duniani na pia kuchangia pato la taifa.

"Tunashangaa watu kila siku tunalia ajira hakuna, ajira hakuna, maisha magumu kama hapa wangepatengeneza ingekuwa nafasi ya wengi wetu kujipatia ajira, lakini ndiyo hivyo kama unavyoona hakuna jitihada yeyote ya kulienzi eneo hili,"alisema Balthoromoe.

Alidai kuwa mabalozi na viongozi ambao waliwahi kutembelea eneo hilo na kuahidi kusaidia ukarabati wake ni Balozi wa Msumbiji nchini, Jose Rui Amaral wa Msumbiji, aliyekuwa Balozi wa Zimbabwe nchini, Chipo Zindoga, Waziri Mkuu wa Msumbiji Carlos Cassa na Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo, Josenio Henriques.

Hata hivyo Balthoromeo anasema ahadi hizo hazijawahi kutekelezwa.

Afisa mtendaji wa kijiji cha Farm 17 Juma Alli alisema kuwa serikali ya kijiji hicho imejiwekea mikakati ya kulinda na kuheshimu mipaka ya maeneo kwa kutofanya shughuli za zozote za kibinadamu.

Historia ya Farm 17

Eneo la Farm 17 lipo umbali kilometa zipatazo 34 nje kidogo ya makao makuu ya wilaya ya Nachingwea, barabara inayoelekea Kilimarondo, ikipakana na wilaya ya Masasi.

Wapigania uhuru wa nchi za Msumbiji, Zimbabwe, Angola na Afrika ya Kusini walipata mafunzo na mbinu za kupambana na wakoloni na makaburu hadi nchi zao zilipofanikiwa kupata uhuru.

Waliacha majengo mbalimbali ya kihistoria likiwemo jengo alilokuwa anaishi Rais wa Msumbiji Marehemu Machael ambalo lilikuwa na njia ya chini ya ardhi yenye urefu wa kilometa zipatazo kumi.

Njia hii inaazia kwenye jengo hilo hadi kwenye handaki ambalo linasemekana ndipo alipokuwa anaishi, kisha kuendelea hadi kwenye uwanja mdogo wa ndege ambao alikuwa anautumia pale alipokuwa akisafiri.

Historia ya Farm 17 inaanzia miaka ya 1947 baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, wakati Serikali ya wakoloni wa Uingereza iliamua kufuta baadhi ya ajira kwa waliokuwa askari wa vita hyo na kuamua kuwatafutia ajira mbadala.

Serikali hiyo ya wakoloni iliamua kuwatafutia ajira kwa kuwakopesha wapiganaji hao fedha na kuanzisha mashamba ya karanga katika maeneo ya Nachingwea kupitia kampuni ya John Molem.

Kupitia mpango huo mashamba 18 yalianzishwa yakipewa majina kuanzia mashamba kuanzia Farm one hadi Farm 18. Hata hivyo kutokana na sababu mbalimbali mashamba hayo hayakuendelea na Waingereza hao kuamua kuondoka na kwenda kuishi Afrika ya Kusini.

Baada ya Tanganyika kupata uhuru Desemba 9, 1961 Serikali iliamua kutumia eneo la Farm 17 kuwa kituo cha kufundishia wapigania uhuru wa nchi zilizo Kusini mwa Afrika.

Viongozi mbalimbali wapigania uhuru katika nchi hizo wakiwamo Komredi Mondlane, Komredi Machel na Komred Mugabe waliishi kwa kujificha na kupewa mbinu mbalimbali, hivyo walichana kumbukumbu ambazo ni muhimu kwa historia ya ukombozi wa Afrika.

Baada ya nchi hizo kufanikiwa kujipatia uhuru eneo hilo lilikabidhiwa kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kikosi cha 41, baadaye wanajeshi hao waliondoka.

Hatua ya JWTZ kuondoka ilitoa mwanya wa majengo hayo kuhujumiwa kwani watu wasiofahamika walianza kuiba baadhi ya vifaa ikiwa ni pamoja na kung'oa mabati, huku eneo hilo likizungukwa na msitu mnene.
 
Historia Nzuri Ya Eneo Hilo
Mugabe Yupo Hai Ashiriishwe Anaweza Kufanya Jambo Jema Kwa Hilo Eneo
 
ingekuwa vyema kama ingependekezwa rasmi kuwa eneo la kihistoria na kuwekwa taarifa mbalimbali za kipindi cha harakati za kupigania uhuru kwa nchi za SADC...

Tatizo maeneo kama hayo yanasahulika taratibu na kubadilishiwa matumizi ivyo kupoteza uhalisia wake... kama mazimbu, morogoro.
 
Tatizo Kubwa Ni Kuyabadilishia Matumizi Hayo Maeneo Maana Yake Kila Kilichopo Kitaharibika Na Uhalisia Kutoweka. Mugabe Akipewa Taarifa Anaweza Kutoa Neno La Kuendeleza Eneo Hilo
 
Nimefika huko mwezi wa tano 2016!
Barabara iendayo huko inaitwa KIPARA MTUA-FARM 17.
Niliingia kwenye nyumba aliyokuwa akiishi Samora Machel, nikaishia kwenye geti la handaki lisilofunguka!
Ile nyumba pamoja na handaki vikarabatiwe!
 
shamba namba 17 wangeliendeleza na kuwa eneo la kihistoria kuliko kulitelekeza.
Mi nilifika huko mwaka 2010, hali ilikuwa mbaya, je sasa? Chumba cha zege alichoishi Samora kimebomoka. Njia ya chini ya ardhi upande wa kusini kuelekea uwanja wa ndege haifai kabisa. Na njia nyingine ya chini kwa chini upande wa kaskazini nayo siyo. Kwa ujumla historia ya pale itafutika kabisa.
 
Nimeishi Nachingwea kwa miaka miwili lakini sikubahatika kuyajua haya pengine kipindi hicho ulimwengu wa teknolojia bado ulikuwa nyuma manake ningeyajua haya wallah ningeenda kutalii,ila NITARUDI NACHINGWEA.

Japo nami niseme machache kwa niliyoshuhudia NACHINGWEA.

1.Kuna makambi mengi sana ya majeshi mbalimbali kila upande kuzunguka makao makuu ya wilaya.
2.Ng'e wengi sana kipindi cha mvua,nilipouliza ni kwanini niliambiwa kuwa enzi za mashamba ya karanga wazungu waliona kuna wadudu wanaharibu karanga na hivyo baada ya kuhangaika na mbinu mbalimbali za kuwaangamiza hao wadudu waharibifu kugonga mwamba ndipo walipoibuka na kuzakisha ng'e ambao walionekana kumaliza tatizo na ndiyo maana mpaka leo kuna ng'e wengi sana.WANAOJUA ZAIDI WANAWEZA KUSEMA LOLOTE JUU YA HILI JAMBO.
 
MC Chere,
Kuna nyaraka nyingi tu ambazo zilikuwa chini ya KAMATI YA UKOMBOZI BARANI AFRIKA. Anayetaka kujua vizuri suala la FARM 17 anaweza kwenda pale Nyaraka za Taifa atapata msaada mzuri maana kuna catalogue za documents za wapigania uhuru kutoka nchi za Msumbiji, Angola, Afrika Kusini nk
 
Kama serikali imeshindwa kuendeleza atafutwe investor ambae ataweza kukarabati na kulifanya eneo la kiutalii wa kisasa zaidi.
 
Back
Top Bottom