Una soko? Au waweza tafuta soko la wazalishaji elfu 5?

kibananhukhu

JF-Expert Member
Jul 6, 2009
366
161

Mimi ninafundisha Ujasiriamali. Nimekwisha fundisha wanafunzi zaidi ya elfu tatu ambao nimewaweka katika "data bank" ya chuo changu pamoja na aina za biashara wanazozifanya. Wengi wao ni wanachama wa SACCOS ambao wanaweza kukopa kati ya shilingi milioni mbili hadi milioni 30 kutegemea mishahara yao na hupashwa kulipa mikopo hiyo kwa kipindi hadi miaka mitatu.

Nina wazo la kuwatafutia masoko kwa pamoja, kuwashauri wazalize kwa makundi na washirikiane katika mengi kibishara kukabiliana na madalali na walanguzi wa kati. Nina wazo pia la kuwashauri waagize bidhaa nje kwa pamoja, na ikibidi hata kuwa na duka moja wafanyabiashara watano watano wale wanaoelewana vizuri marafiki ili kuchangia gharama.

Ninaomba mwenye uwezo wa kutafuta masoko kwa bidhaa zozote hususani zinazopatikana tanzania wanishauri au waniunganishe kwani nina watu wanaokopesheka. Ushauri wowote kuhusu mada hii utapelekea kujikomboa kiuchumi. Kwani hadi mwishoni mwa mwaka huu nitakuwa nimewafundisha wanachama wa SACCOS zaidi ya elfu 5 katika taasisi yetu na wote watakuwa katika data bank zetu pamoja na biashara zao.

Naamini pia wao watakuwa ni soko la wao kwa wao kwa baadhi ya bidhaa hivyo soko kubwa litahitajika pia.

Je, Nishaurini, wazo hili ni zuri? Kuna wazo mbadala? Kuna ushauri wowote katika mafunzo ninayoyafanya kwani mwisho wa siku lengo ni asilimia kuwa ya wanafunzi waboreshe na kuanzisha biashara kitaaluma.

Asanteni sana kwa mawazo yanu mtakayonipatia na nipo tayari kushirikiana na yeyote.

 

Mimi ninafundisha Ujasiriamali. Nimekwisha fundisha wanafunzi zaidi ya elfu tatu ambao nimewaweka katika "data bank" ya chuo changu pamoja na aina za biashara wanazozifanya. Wengi wao ni wanachama wa SACCOS ambao wanaweza kukopa kati ya shilingi milioni mbili hadi milioni 30 kutegemea mishahara yao na hupashwa kulipa mikopo hiyo kwa kipindi hadi miaka mitatu.

Mkulu hongera sana kwa kazi yako ubarikiwe na uzidi kuendelea



Nina wazo la kuwatafutia masoko kwa pamoja, kuwashauri wazalize kwa makundi na washirikiane katika mengi kibishara kukabiliana na madalali na walanguzi wa kati.

Mkulu ungetupa ufafanuzi kidogo hapa...Je ni wanazalisha nini?...Je wanazalisha kiasi gani? na Je ni kwa miezi au mwaka?
 
Wanazalisha bidhaa za aina mbali mbali, lakini bado hawajawekwa sawa. Wanafuga kuku wa kienyeji, kuku wa mayai ya kienyeji na kisasa, wanazalisha na kuuza asali, mafuta ya nafaka, wanauwezo wa kuwekeza kwenye kilimo lakini tatizo kubwa ni soko, wanaweza kulima mpunga, miwa, mahindi, alizeti, matunda.

Kimsingi tunahitaji kujua tuwekeze wapi. Katika awamu ya kwanza tumewahamishisha waanze biashara kwani wengi wao ni wafanyakazi hivyo hutumia mikopo yao kujengea nyumba, kusomeshea, kutumia katika starehe na maraha. Sasa hivi wapo tayari kuwekeza katika biashara.

Mfano, tunampango wa kupata hekari elfu moja mahali na kila mwanachama atakaye penda atapata hekari kumi. Hapo tutaweza lima chochote na kuuza mazao katika soko la ndani. Lakini kuna watu kwa mfano wapemba wanauza mchele nje. Wanauza wapi? Tunataka kwenda huko.

Tunasikia kwa mfano, kuna soko zuri la samaki DRS la nyama, samaki, mchele na vyakula kwa ujumla hata ndizi. Lakini sisi tunafundisha tu. Tukipata wenzetu wenye uwezo wa kutuunganisha na masoko hayo, twaweza fanya utaratibu.

Kwa kifupi, tulidhani tusaidiwe katika utaratibu wa kupata masoko ya aina yoyote ya bidhaa kama mazao ya kilimo, uvuvi, mifugo, na viwanda vya kuzalisha juices, tomato, chili, Jam, kwani tuna uwezo wa kuwafundisha kilimo bora na ufugani na yote hayo. Kwani wanakopesheka kirahisi. Asante.
 
Mkuu. Kwanza nikupe hongera kwa kukusanya record ya watu unawafundisha njia zote mbadala za ujasilimali. Nitakusaidia kama Business Developer ambae nina zaidi ya miaka 5 kwenye development katika sector ya Mafuta na Gesi (O&G). Soko kubwa nchi za Ulaya na North America halipo kwenye nafaka/chakula sababu ya intensive sheria za kuingiza chakula, na vile vile tatizo kubwa la wasambazaji wa Africa ni kwamba hawako predictable. Maana ya kwamba product yako inaweza kuja kwenye market, kisha ikapendwa lakini mkawa mna limited supply.

Lakini bado opportunity kwenye chakula ni kubwa sana, haswa kusini mwa jangwa la sahara. Cha muhimu ni kuwekeza kwenye product nzuri zenye ushindani, pili kuboresha pacage na tatu ni kuwa na marketing strategy nzuri.
 
Asanteni sana kwa Ushauri. Mtanganyika, nina wanachama wa madini pia hasa dhahabu na sasahivi shaba inapatikana kwa baadhi ya wanafunzi wangu. Uzalishaji unaweza ongezeka kama tutapata soko la shaba. Kuhusu dhahabu nashangaa kidogo. Sijui ni kwa nini sehemu kama geita na nyarugusu wananunua karibu au zaidi kidogo ya bei ya dunia. Maana yake nini? Nitashukuru kupata msaada wowote.
 
kibananhukhu

je umefikia wapi nawazo hili, iam very anxious toknow the preogress

humu katika jamvi hili kumekuwa na posts nyingi na ushauri mwingi sana wa sourcing na demand ya market ya Agri-products especially for export
 
Back
Top Bottom