Una miaka 30 au chini? Kachukue fomu ya BAVICHA

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Mnyika1(6).jpg

Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, John Mnyika

Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (Bavicha) ngazi ya taifa, linatarajia kufanya uchaguzi mwezi ujao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya chama hicho, John Mnyika, nafasi zitakazogombewa ni pamoja na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mratibu wa Uhamasishaji, Mweka Hazina, Wawakilishi wa Bavicha kwenye Mkutano Mkuu wa chama na wawakilishi wa Bavicha kwenye Baraza Kuu la chama.

Alitaja umri unaoruhusiwa kugombea kwa mujibu wa Katiba umri wa ujana ni kati ya Miaka 18 na 35.

Alisema mgombea anatakiwa kugombea kwenye umri unaomruhusu kumaliza kipindi chake cha uongozi akiwa bado na umri wa Ujana; hivyo wagombea wenye umri wa zaidi ya miaka 30 hawataruhusiwa kugombea ili kufanya viongozi wa vijana wasiwe zaidi ya miaka 35 katika kipindi chao chote cha utumishi katika Bavicha.

" Wagombea watachukua na Kurudisha Fomu kuanzia tarehe 4 Aprili hadi tarehe 26 Aprili. Fomu zitatolewa kuanzia ngazi ya Mkoa, Makao Makuu ya chama," alisema Mnyika.

Alisema kwa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mratibu wa Uhamasishaji na Mwekahazina watalipia shilingi elfu thelathini.

Alisema waliogombea uchaguzi wa awali uliofutwa watajaza na kulipia upya hata kama waliogombea nafasi hizo hizo wanazogombea sasa kwa mujibu wa kanuni za chama.

Alisema mikutano ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wawakilishi wa Bavicha kwenye Baraza Kuu na Mkutano Mkuu watachaguliwa na Mkutano Mkuu wa Bavicha kwa mujibu wa katiba, kanuni na taratibu.

Alisema Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mratibu wa Uhamasishaji na Mwekahazina watapendekezwa na Kamati ya Utendaji ya Bavicha na uteuzi wao utathibitishwa na Kamati Kuu ya chama.

Kuhusu kampeni, Mnyika alisema kampeni za uchaguzi zitafanywa kwa kuzingatia kanuni za chama, maadili ya uongozi/viongozi pamoja na muongozo juu ya uendeshaji wa uchaguzi ndani ya chama uliopitishwa na Baraza Kuu la Chama unafafanua mambo yanayopaswa kufanywa na yasiyopaswa kufanywa wakati wa kampeni na uchaguzi ndani ya chama kwa lengo la kujenga mshikamano na umoja ndani ya chama na kufanya uchaguzi uwe huru na wa haki.
 
Nitachukua Fomu,Nitatangaza Rasmi...Rafu zimeshaanza kuchezwa,lakini......
 
Mgombea anatakiwa kugombea kwenye umri unaomruhusu kumaliza kipindi chake cha uongozi akiwa bado na umri wa Ujana; hivyo wagombea wenye umri wa zaidi ya miaka 30 hawataruhusiwa kugombea ili kufanya viongozi wa vijana wasiwe zaidi ya miaka 35 katika kipindi chao chote cha utumishi katika BAVICHA

Ndugu wapenda mabadiliko katika nchi hii, kipenga cha BAVICHA kimepulizwa. Naomba kuuliza kutokana na tafsiri ya hapo juu, je mtu aliyezaliwa tarehe 29 mei 1980 je ataruhusiwa kugombea uongozi wa BAVICHA au ndiyo basi tena.
 
Nadhani ataruhusiwa ili mradi hadi siku ya Uchaguzi uwe below 30,sina uhakika sana lakini chama kinaweza kutoa ufafanuzi zaidi kwa hilo
 
To make things easier waseme waliozaliwa kuanzia tarehe xxx mwezi xxx mwaka xxxx ndio ambao wanaweza kugombea.

Everything should be transparent
 
Anza kampeni huku JF basi, jina lako Ben nani? linafanana na yule Rais Mstaafu wa Tz


Mkuu Sita Sita,

Hata jina lako linafanana na la Spika wa Bunge wa Zamani,lol
Nashukuru,ila kuna miongozo ambayo wagombea wanatakiwa kufuata linapokuja suala la kampeni kwa ajili ya chaguzi za ndani.Nitakapochukua fomu Rasmi nitaanza kampeni Rasmi


 
Una miaka 30 au chini? kachukue fomu ya BAVICHA leo..

Kwa hiyo sifa ni kuwa na miaka 30 or less, bila ya kujali kama wewe ni mwanachama? Kwa hiyo CCM tunaruhusiwa kuchukua fomu pia?
 
Kwa hiyo sifa ni kuwa na miaka 30 or less, bila ya kujali kama wewe ni mwanachama? Kwa hiyo CCM tunaruhusiwa kuchukua fomu pia?
Nadhani sifa mojawapo ni lazima uwe mwanachama wa CDM lakini kama wewe ni mwana CCM na unataka kugombea unakaribishwa kujiunga na CDM kwa vile muda wa kurudisha fomu ni hadi April 26.
 
To make things easier waseme waliozaliwa kuanzia tarehe xxx mwezi xxx mwaka xxxx ndio ambao wanaweza kugombea.

Everything should be transparent
Ndugu yangu SS kama hata umri wako hujui hadi ulinganishe kwa tarehe utatufaa kweli.
 
Kuhusu haki za mwanachama wa BAVICHA, Website ya CHADEMA inasomeka:

Uanachama,
Baraza la Vijana wa CHADEMA-BAVICHA


"Wanachama wa kawaida: Hawa ndio wanachama mahsusi wa BAVICHA. Ni vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 35. Watakuwa na kadi za BAVICHA, watashiriki shughuli zote za BAVICHA na watakuwa na haki zote za uanachama wa BAVICHA."

Maana yake ni kwamba ukiwa na miaka 31, mathalan, unaweza kujiunga kuwa mwanachama wa BAVICHA. Sasa utakuwaje mwanachama
"na kuwa na haki zote" bila ya kuwa na haki ya kugombea uongozi?

Kutokuwa makini katika uandishi wa taratibu, Katiba, na bylaws za chama. Mambo haya huwa yanaleta mitafaruku ndani ya vyama, kama Nape candidate wa uongozi UVCCM aliyekuwa derailed na masharti yaliyoandikwa kinyumenyume kama haya.

Inakuonyesha kwamba hawa kina Marando na Lissu, wanasheria CHADEMA, hata wangekuwa wao ndio wanasheria wakuu na mawaziri wetu wa sheria bado wangeandika miswada na mikataba ya nchi dizaini ya Celina Kombani na Andrew Chenge. Hawana tofauti kabisa. And these are supposed to be among the ablest lawyers around.
 
wagombea wenye umri wa zaidi ya miaka 30 .

Lol! hivi 32 zangu tayari nshakuwa mzee?
Kama ni ivo basi afazali kule UV-ufisadini make yule mdada anayeitwa ua la waridi lenye aibu bado anahesabika kijana.
 
Kuhusu haki za mwanachama wa BAVICHA, Website ya CHADEMA inasomeka:

Uanachama,
Baraza la Vijana wa CHADEMA-BAVICHA

"Wanachama wa kawaida: Hawa ndio wanachama mahsusi wa BAVICHA. Ni vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 35. Watakuwa na kadi za BAVICHA, watashiriki shughuli zote za BAVICHA na watakuwa na haki zote za uanachama wa BAVICHA."

Maana yake ni kwamba ukiwa na miaka 31, mathalan, unaweza kujiunga kuwa mwanachama wa BAVICHA. Sasa utakuwaje mwanachama "na kuwa na haki zote" bila ya kuwa na haki ya kugombea uongozi?

Kutokuwa makini katika uandishi wa taratibu, Katiba, na bylaws za chama. Mambo haya huwa yanaleta mitafaruku ndani ya vyama, kama Nape candidate wa uongozi UVCCM aliyekuwa derailed na masharti yaliyoandikwa kinyumenyume kama haya.

Inakuonyesha kwamba hawa kina Marando na Lissu, wanasheria CHADEMA, hata wangekuwa wao ndio wanasheria wakuu na mawaziri wetu wa sheria bado wangeandika miswada na mikataba ya nchi dizaini ya Celina Kombani na Andrew Chenge. Hawana tofauti kabisa. And these are supposed to be among the ablest lawyers around.
Taso nimekupata kabisa you are right by 100%, lakini jua kuwa haki inatolewa na katiba/sheria kwa mkono huu inachukuliwa na hiyo hiyo katiba kwa mkono ule, say unachaguliwa kuwa Menyekiti ukiwa na miaka 32 baada ya miaka mitatu tayari umevuka umri uliotajwa na katiba ukiambiwa kujiuzuru utakubali?, ili kuepuka hayo matatizo kama tunayoshuhudia UVCCM ndiyo maana CDM imeamua kutahadhalisha umri mapema.
 
Mimi naona Chama kiko right kwa sababu,tuchukulie mfano mtu ambaye atakuwa 35 tarehe 29/05/2011 akiamua kuchukua fomu bado anaweza kusema yeye ni kijana yuko below 35.Lakini keso yake yupo 35.Kuna hatari ya kuwa na mwenyekiti wa vijana mwenye umri wa kugombea urais

Hili suala nadhani chama kilitakiwa kirekebishe mwenye haki ya kuchagua na haki ya kucahguliwa
 
Back
Top Bottom