Una maoni gani kuhusu hii picha

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,948
709
IMG_3275.jpg


Je hawa watu walikuwa wana-smile kwa ajili ya kamera au wameridhika na maisha waliyonayo.............toa maoni.

Maoni yangu: Naamini watanzania wanaridhika na kile walichonacho ingawa gap ya walionacho na wasionacho ni kubwa sana
 
Mpiga picha anawambia "smile..." ndo kila mtu kaonyesha meno yake, hakuna anoridhika na shida tunastahamili tu.
 
Wamefrahia kupata ugeni wa wazungu nyumbani kwao,na wazungu nao wamefrahi ukarimu wa waafrika.
 
Inaonyesha wana-smile midomo peke yake lakini usoni wanagugumia kimya-kimya kwa machungu ya maisha.
 
Inaonyesha wana-smile midomo peke yake lakini usoni wanagugumia kimya-kimya kwa machungu ya maisha.

Kweli man, nakusupport
Hawa hawana raha yoyote, ndo hivyo kutembelewa na wazungu, wanaishi kwa matumaini kwamba huenda mzungu akatoa ahadi yoyote ya kuboresha.
Ila comment yangu nyingine ni juu ya nyumba hiyo walimo.
Nyumba za dizaini hiyo ni zile za typical kwa akina Indume jene.
Huyu bwana amechukua picha za kumbukumbu kwao bila shaka.
Si ndio mzee?
 
gema from school of stjude she doin a great job kaulizieni arusha watoto wanakula elimu nzuri bure......hapo alikuwa kaenda kuwatembelea wazazi wa moja ya wanafunzi wa shule yake....
 
hio furaha ni ya moyoni kabsaa jamani ingawa hao wazungu wakiondoka machungu line yanarudi mahali pake,nakumbuka nilipokuwa mdogo nshawai kupiga picha kama hii na wafini fulani hivi kweli kama mdau hapo juu alivyosema furaha ni ya kutembelewa na wazungu kwani mama nae akajibana angalau tukala msosi wa maana na kupiga picha,na je unajua nguo za kutokea ili nipige picha ilikuaje?kama huyo dogo hapo aliyepiga na uniform,sio kwamba katoka shule kakuta picha inapigwa kaunganisha no,huyo hiyo uniform ndio nguo nzuri ambayo amevaa kwaajili ya picha na mimi ndivyo nilivyofanya kwa kuamriwa nikaulamba
 
Inaonyesha wana-smile midomo peke yake lakini usoni wanagugumia kimya-kimya kwa machungu ya maisha.

ila ujue pamoja na shida walizo nazo, watu wa vijijini wana enjoy sana maisha yao. mara nyingi huku mjini ndiyo tunalalamika
 
ila ujue pamoja na shida walizo nazo, watu wa vijijini wana enjoy sana maisha yao. mara nyingi huku mjini ndiyo tunalalamika

Nilitaka kuuliza swali moja lakini naona mzee utakuwa umejibu. Swali lilikuwa maisha ya vijijini yanaweza kumfanya mtu akawa stress hadi akapata BP?
 
Mwenyezi mungu ni mwema sana kampa kila mwanadamu namna yake ya kufurahia maisha awe tajiri ama maskini kila mtu kwa uwezo wake na nafasi yake anafurahia maisha na siku zinakwenda na mwisho wake wote tunakwenda sehemu moja.
 
Alafu hawa ukiongea nao ndio utasikia wanashabikia sisiem kuwa imeleta amani na utulivu
 
Mwangalieni yule mtoto mwenye tshirt nyekundu na kofia. Mtazamo wake umemaliza kila kitu.
 
Hawa watu wanatakiwa wawe vijijini kujenga taifa lakini huko nako hakukaliki kabisa wote wanakimbilia mijini kutafuta ajira na matokeo yake ndiyo kama hivi tunavyowaona,sijui viongozi wetu hawayaoni haya,watu wa ccm maneno mengi sana tumewaachia wenyewe mpaka kutufikisha hapa tulipo.Naomba watu wote tujitolee kwa hali na mali kuwapiga vita hawa majambazi mpaka tuwang'oe madarakani mwaka huutuanze mapema sana hizo juhudi .
 
Unuseful post. God bless these people, we all have to smile once in a while, whats wrong with that?
 
mambo ya kujinafasi na kuipa uhuru nafsi walau kwa dakika.maana hao ndugu wakiondoka,mambo yetu ya dagaa,kama kawa.
 
Back
Top Bottom