UN: Mikataba mibovu yakwaza wananchi kunufaika na rasilimali

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,109
Kaou.jpg

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, akizungumza wa Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Alberic Kacou (kushoto) wakati alipomtembelea Mengi ofisini kwake jijini Dar es Salaam.


Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Alberic Kacou, amesema Tanzania ina fursa nyingi za kiuchumi ambazo zingeifanya ipige hatua katika maendeleo lakini imeshindwa kuzitumia na kujikuta ikiendelea kuwa chini.

Aliyasema hayo jana alimtembelea Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, alipomtembea ofisini kwake jana.

Kacou alitaja baadhi ya fursa hizo kuwa ni pamoja na madini, gesi mafuta na mbuga za wanyama na kwamba vyote hivyo vimeshindwa

kuwanufaisha wananchi kutokana na mikataba isiyokuwa mibaya inayoingia serikali na wawekezaji.

Alisema serikali inashindwa kuingia mikataba mizuri katika sekta ya madini na rasilimali zingine na kwamba hatua hiyo ndiyo inayowafanya wawekezaji waendelea kuzinyonya nchi za Afrika ikiwemo Tanzania. Alitaja baadhi ya nchi za Afrika zinazokumbwa na

tatizo hilo kuwa ni pamoja na Ethiopia, Msumbiji na Ghana ambapo alisema raslimali nyingi haziwanufaishi watu wake.

Alifafanua kuwa sababu nyingine ni ulegevu wa sheria ambapo serikali za nchi husika zinashindwa kuyabana makampuni ya wawekezaji ili yaweze kulipa kodi kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya nchi zao.

Aidha, Kacou alisema tatizo la umeme wa uhakika pamoja na ubovu wa miundominu ni miongoni mwa sababu zinazowakatisha tamaa wawekezaji na hivyo kushindwa kuwekeza katika baadhi ya nchi nyingi za Afrika.


Alitaka vyombo vya habari na serikali kupitia Bunge vitumike kutoa elimu kwa umma kuhusu rasilimali za nchi na namna zinavyotumika. Aidha, alishauri fursa zote za nchi na rasilimali zake viwekwe katika tovuti ili wananchi waweze kuviona na kuvielewa.

Kuhusu suala la Umoja wa Mataifa kuwa na mpango maalum wa kuwasaidia watu wenye ulemavu, Kacou alisema mpango huo upo na

kwamba kundi hilo linasaidiwa kwa kupatiwa elimu ma kuwa wakipatiwa elimu watakuwa na uwezo wa kujikomboa kwa kuwa wataweza kujiajiri wenyewe.


Kwa upande wake, Mengi alisema hakuna sababu kwa wawekezaji kuja nchini na kuwaelekeza Watanzania kwamba sehemu fulani ya nchi kuna madini, gesi pamoja mafuta.



Aidha, Mengi alimueleza Mratibu huyo kuwa nchi nyingi za Afrika zinatoa rasilimali zake kwa bei ndogo na kusisitiza umuhimu wa wananchi kujua kinachoendelea kuhusu rasilimali zao. Pia alizungumzia umuhimu wa VICOBA na kusema kuwa mpango huo unawafaidisha wananchi wengi hususani wenye kipato cha chini na wanaoishi vijijini kwa ajili ya kupata mikopo.




CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom