UN kuamua hatima ya kumbukumbu za ICTR

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
Jumamosi, Septemba 08, 2012 08:36 Na Mwandishi wa Hirondelle, Arusha

MSAJILI wa Taasisi ya Kimataifa itakayorithi kazi za Mahakama za Kimataifa (MICT), John Hocking, amesema hatima ya mahali pa kuhifadhi kumbukumbu za Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) iko mikononi mwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Rwanda imekuwa ikidai haki ya kuhifadhi kumbukumbu za ICTR, baada ya kuhitimisha kazi zake kwa maelezo yenyewe ndiyo yenye haki ya kiasili ya kupokea kumbukumbu hizo, kutokana na ukweli kwamba mauaji ya kimbari yalifanyikia nchini Rwanda.

Wakati wa uzinduzi rasmi wa MICT, Tawi la Arusha, Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Rwanda, Martin Ngoga, alisema wanahitaji majadiliano ya wazi katika masuala mbalimbali, likiwamo la uhifadhi wa kumbukumbu.

Hata hivyo, Hocking, alisema: “Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa namba 1966 litafanyiwa tathimini baada ya miaka minne ijayo na siwezi kujua nini kitatokea baada ya miaka minne.

“Ni wazi kwamba sina mwelekeo kamili juu ya hili, lakini kwa hivi sasa ninachokifanyia kazi ni Azimio la Baraza la Usalama, ambalo limeelekeza kwamba kumbukumbu hizo zihifadhiwe mahali zilizopo mahakama hizo za Umoja wa Mataifa.’’

Kwa mujibu wa azimio hilo lililoidhinishwa mwishoni mwa mwaka 2010, kuanzishwa kwa MICT ni kwa ajili ya kurithi kazi zitakazoachwa na ICTR, yenye makao yake makuu Arusha na mahakama nyingine ya Umoja wa Mataifa ya Uhalifu wa Kivita Katika Yugoslavia ya zamani (ICTY) iliyopo The Hague, Uholanzi.

“Katika azimio hilo, Baraza la Usalama lilieleza kwamba kumbukumbu za ICTR zihifadhiwe Arusha na zile za ICTY zihifadhiwe The Hague,’’ alisema Hocking.

Alisema tawi la MICT la Arusha lilipoanza kazi Julai Mosi, mwaka huu, shughuli mbalimbali za ICTR zilihamishiwa kwa taasisi hiyo mpya ikiwa ni pamoja na kumbukumbu za baadhi ya kesi zilizokwisha hitimishwa na ulinzi wa watu waliotoa ushahidi katika kesi hizo.

Alisema shughuli nyingine zilizohamishiwa katika taasisi hiyo mpya ni pamoja na kusaidia juhudi za mataifa yanayofanya uchunguzi dhidi ya watuhumiwa wa mauaji hayo nchini mwao na kuendelea kuwasaka watuhumiwa tisa ambao bado hawajatiwa mbaroni.

Alisema jukumu la kusimamia adhabu walizopewa wafungwa waliopo Mali na Benin pia lilihamishiwa katika taasisi hiyo kuanzia tarehe hiyo.

Alipoulizwa juu ya usalama wa wafungwa wanaotumikia adhabu zao nchini Mali kutokana na tishio la hali ya usalama nchini humo, alisema Idara ya Ulinzi na Usalama ya Umoja wa Mataifa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Mali wamemhakikishia kwamba wafungwa wote wako salama.

[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
 
Back
Top Bottom