Umuhimu wa wosia

Bishanga

JF-Expert Member
Jun 29, 2008
15,323
10,050
Hivi ninavyofungua huu uzi kuna kijana jirani yangu yamemkuta. Yeye ni mmoja wa wale wanaoitwa 'watoto wa nje' (neno hili silipendi kabisa,kwangu mtoto ni mtoto tu). Mzee wake amefariki hakuacha wosia. Sasa mke wa marehemu na wanae wa kuzaa wamegangamala wanasema mtoto wa 'nje' kisheria hana haki ya kurithi chochote.It is too sad maana hata baba yake alikuwa anampenda sana kijana huyu na bado hajamaliza shule.Kwa wale watu wazima chonde chonde jamani tuandike will ili mali yetu tuigawe kulingana na utashi wetu. Na kwa vijana wakumbusheni wazazi wenu kuandika will wala msiogope kuwambia,ni kwa faida ya wanandugu wote na kupunguza mizozo isiyo na lazima.
 
nakubaliana na wewe mkuu
 
Wezetu wa mbele huko (wazungu)ni kitu cha muhimu sana lkn huku kwetu wazee wakiambiwa wanaona km wanchuriwa kufa au watoto wana tamaa ya mali, ila kiukweli ni muhimu sana kuandika wosia.
 
taratibu za kuandika wosia zikoje hususani kwa walio mikoani
 
Hivi ninavyofungua huu uzi kuna kijana jirani yangu yamemkuta. Yeye ni mmoja wa wale wanaoitwa 'watoto wa nje' (neno hili silipendi kabisa,kwangu mtoto ni mtoto tu). Mzee wake amefariki hakuacha wosia. Sasa mke wa marehemu na wanae wa kuzaa wamegangamala wanasema mtoto wa 'nje' kisheria hana haki ya kurithi chochote.It is too sad maana hata baba yake alikuwa anampenda sana kijana huyu na bado hajamaliza shule.Kwa wale watu wazima chonde chonde jamani tuandike will ili mali yetu tuigawe kulingana na utashi wetu. Na kwa vijana wakumbusheni wazazi wenu kuandika will wala msiogope kuwambia,ni kwa faida ya wanandugu wote na kupunguza mizozo isiyo na lazima.

Kwa sheria ilivyo sasa watoto wa nje wanapoteza haki ya kurithi hasa kama baba hakuwatambulisha/ama kuwaweka wazi kuwa ni wanawe....na kwa kusema ukweli mimi naona hii ni fair tu. Kama una mtoto wa nje ni vema ukamchukuwa na kukaa nae/au kuhakikisha anatambulika formally kuwa ni mwanao/mtegemezi wako.

Kutegemea na dini ya muhusika, wosia peke yake unaweza usiwe na nguvu.....kama kuna vitu unataka 'kumrithisha' mtu ambaye kisheria hana haki ya kukurithi ni vema ukamgawia sehemu yake akaanza kuimiliki kabla wewe hujafa.
 
Mimi nasema hivi wanaume mnashindwa kuandika wosia mnadai mnachuriwa hili gumu, Jamani mie nawaomba wababa wale wenye mali zingine zile za pembeni ambazo mke hajui tafadhali muache mchezo huo. Binamu zangu wamekuwa maskini kwelikweli sababu tu ya usiri wa baba, watu wengine wanafaidi inasikitisha sana.
 
nami pia kuna watu ninaowafahamu, ukweli ni kwamba sio mali tu bali inasaidia hata mambo ya mazishi (tumeona maiti zinagombewa kidini), sehemu ya kuzikwa nk. Lakini kwa suala hili mkuu mkuu linatukumbusha pia kuwa integrity ya mtu ni muhimu, sio kitu kizuri kuwa na watoto wengi wa nje kwa maana ni kielelezo cha kutokuwa mwaminifu kwa familia. Ni changamoto!

Mkuu SMU una maana will ambayo imeandikwa vizuri ikawa na ushahidi wa saini kwa mujibu wa sheria (nasikia ni watu wawili) mtu akifariki bado inaweza kuwa contested? Kivipi?
 
ni jambo zuri sana, hata mimi kuna kanyumba nakafuatilia huko mbeya kwa kuwa baba yenu kampa mtoto wake aliyezaa na mama mwingine, ndo niko kwenye process na kuonana na mwanasheria wangu.
 
Kwa mfano katika uislamu kuna utaratibu maalumu wa kurithi/kurithisha (very detailed, kwa mtizamo wangu). Na pia will ambayo muhusika anatoa mali yake yote kwa watoto wa nje (au watu ambao kisheria sio warithi) halafu wale wa ndani wakose chochote....naamini inaweza kuwa contested.....hasa kama kwa mfano watoto bado ni tegemezi. Kwa mfano hebu chukua mtu kaandika will ambayo anaitoa nyumba anayoishi yeye na familia yake kwa mtu ambaye sio mwanafamilia na kitendo hichi kufanya watoto na mama kukosa pahala pa kujihifadhi, unadhani hiyo will hata kama imesainiwa itakubalika (tuangalie kimantiki tu!)?
 
Mimi nasema hivi wanaume mnashindwa kuandika wosia mnadai mnachuriwa hili gumu, Jamani mie nawaomba wababa wale wenye mali zingine zile za pembeni ambazo mke hajui tafadhali muache mchezo huo. Binamu zangu wamekuwa maskini kwelikweli sababu tu ya usiri wa baba, watu wengine wanafaidi inasikitisha sana.

ndo haya nilikuwa nalalamikia.
 
nami pia kuna watu ninaowafahamu, ukweli ni kwamba sio mali tu bali inasaidia hata mambo ya mazishi (tumeona maiti zinagombewa kidini), sehemu ya kuzikwa nk. Lakini kwa suala hili mkuu mkuu linatukumbusha pia kuwa integrity ya mtu ni muhimu, sio kitu kizuri kuwa na watoto wengi wa nje kwa maana ni kielelezo cha kutokuwa mwaminifu kwa familia. Ni changamoto!

Mkuu sina ubishi na hiyo red,ila ikishatokea ndo hivo tena unawajibika.Ahsante kwa kwa angalizo hilo muhimu.
 
ni jambo zuri sana, hata mimi kuna kanyumba nakafuatilia huko mbeya kwa kuwa baba yenu kampa mtoto wake aliyezaa na mama mwingine, ndo niko kwenye process na kuonana na mwanasheria wangu.

hahahahaha Mamndenyi,mtoto wa mwenzio ni mwanao,mwachie bana!
 
Kwa mfano katika uislamu kuna utaratibu maalumu wa kurithi/kurithisha (very detailed, kwa mtizamo wangu). Na pia will ambayo muhusika anatoa mali yake yote kwa watoto wa nje (au watu ambao kisheria sio warithi) halafu wale wa ndani wakose chochote....naamini inaweza kuwa contested.....hasa kama kwa mfano watoto bado ni tegemezi. Kwa mfano hebu chukua mtu kaandika will ambayo anaitoa nyumba anayoishi yeye na familia yake kwa mtu ambaye sio mwanafamilia na kitendo hichi kufanya watoto na mama kukosa pahala pa kujihifadhi, unadhani hiyo will hata kama imesainiwa itakubalika (tuangalie kimantiki tu!)?

Mkuu sibishani na hii mantiki lakini jamani si mali yangu? watu kibao wametoa nyumba zao waqfu,baadae watoto wananuna,wananuna nini sasa wakati mwenye mali kaamua? na mitoto mingine ukiiangalia pamoja na kwamba umeizaa mwenyewe imekaa kihasarahasara tu bange mtindo mmoja unajua kama hili nikiliachia nyumba au magari litauza tu linunulie msuba si bora mali zako uliachie Kanisa au Msikiti?
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Back
Top Bottom