Umuhimu wa Mfumo Dume (Ubaba)

Sasa mbona ni kama unakubaliana na mimi sasa? Au unakubaliana na Companero kwamba 'pesa ndiyo msingi mkuu wa mapenzi'?

yaani naona upolyglot wa ngabu senior unakuathiri mpaka unafocus sana on semantics, haya tubadili hiyo sentensi iwe hivi:

fedha ndio injini ya mapenzi
 
Huko kujifunga unakuona wewe tu, mimi sioni. Wewe unadai pesa ndiyo injini ya penzi, mimi nakataa. Injini ya penzi ni penzi la kweli, kwenye shida na raha.

tautology hiyo eti injini ya penzi ni penzi, gibberish
 
U ar just in ur usual difficukt mood Ngabu boy! Kuwa na msingi ni muhimu, japo kuwa na paa na madirisha ndo kinachofanya nyumba. Tunaongelea the same thing from different angles. Kua na pesa sio kuwa provider! Lakini ili uweze ku-provide unahitaji kiasi flani cha hela kwa level yako. Wakati wewe unamnunulia mkeo a gold chain, mie mpenzi wangu ananiletea chain ya ubungo hapo tshs 1500. Naivaa occasionally isipauke, but I feel it kuwa nimeletewa na kipenzi. Kuna mijitu ina hela lakini haisaidii familia zao.

I'm not being difficult or anything. I just don't agree with the claim that money is the be-all and end-all of love.

But I see you are also going around in circles so let me get you on record. Je, pesa ndiyo msingi mkuu wa mapenzi? Nataka jibu la ndiyo au hapana. Usilete siasa zako....
 
Baba, hakuna 'uhakika wa kipato', ndivyo ninavyoamini. Kama unajua hadithi ya Ayubu, alivyotendwa utanielewa kwa nini partly nakubaliana na angle ya NN. Lakini tunatoka kwenye mada, kuwa 'PROVIDER'! Mambo yakichacha si ndo unalima viazi ama unafagia McDonald's afu unaendelea kuwa providor? Kutokuwa na pesa sio tatizo, tatizo ni unafanya nini kujikwamua? Hicho ndo kipimo cha uanaume sasa!
asante kwa angalizo, namaanisha uhakika wa kipato/pesa/uwezo wakati wote, nadhani kuna lile neno linalopendwa kutumiwa i.e. security.
 
yaani naona upolyglot wa ngabu senior unakuathiri mpaka unafocus sana on semantics, haya tubadili hiyo sentensi iwe hivi:

fedha ndio injini ya mapenzi

Kama umeamua kutumia analogy ya injini basi pesa ni sawa na radiator
 
Do u know I can also be difficult? Tena kwa makusudi tu? Hebu ngoja nilale mie manake 'I have a provider', lol! Kura imeharibika hii!
I'm not being difficult or anything. I just don't agree with the claim that money is the be-all and end-all of love.

But I see you are also going around in circles so let me get you on record. Je, pesa ndiyo msingi mkuu wa mapenzi? Nataka jibu la ndiyo au hapana. Usilete siasa zako....
 
hela nazitafuta mimi mwenyewe.kwa kujituma,huna tabia ya kumtegemea mtu,kwa the way nilivyolelewa.mapenzi kwangu,naangalia kikubwa tabia.
sawa, lakini mwisho wa siku sheria ya nchi ya mahusiano rasmi ya 1971, CAP 29 RE. 2002, inasema dume ndio linatakiwa litoe mshiko!

Mi' ngoja ni pasue jipu.....

Wanawake wengi tunaogopa kusema pesa muhimu kwa sababu tunaogopa kuitwa materialistic, lakini kimsingi hasa wengi wanataka mwanamme awe nazo hizo [p] tatu

Binafsi nisingependa kuwa breadwinner wa familia maisha yangu yote. Kimsingi hata kipato ningependa chake kiwe kikubwa kuliko changu (ili nijiskie mwanamke???)
kumbe huo ndio mzizi wa fitina, sasa nimeng'amua kwa nini nimenyimwa namba ya simu, nilipokwambia Voda kwa Airtel sipigi na dinner za Serena Hotel zisiwezi. Ngoja nikatafute wale ninaowazidi kipato.
 
Baba, hakuna 'uhakika wa kipato', ndivyo ninavyoamini. Kama unajua hadithi ya Ayubu, alivyotendwa utanielewa kwa nini partly nakubaliana na angle ya NN. Lakini tunatoka kwenye mada, kuwa 'PROVIDER'! Mambo yakichacha si ndo unalima viazi ama unafagia McDonald's afu unaendelea kuwa providor? Kutokuwa na pesa sio tatizo, tatizo ni unafanya nini kujikwamua? Hicho ndo kipimo cha uanaume sasa!

Hebu skiza 21 questions ya 50 Cent

Last edited by a moderator:

Naona sasa unaanza kuzungukazunguka kama NN, kuwarahishia kazi ngoja niipanua hiyo sentensi isomeke hivi:

K TATU NDIO MISINGI MIKUU WA MAPENZI: KUTOA, KULINDA NA KUONGOZA

THREE P ARE THE KEYS OF LOVE: PROVIDING, PROTECTING AND PRESIDING

Sasa kama mnaweza kutoa, kulinda na kuongoza bila pesa haya we!
 
Umebanwa hadi umeachia....hahahahahaa. Sasa hata ile namba ya yule nitakutafutia. Au umeshaghairi?
 
Hebu skiza 21 questions ya 50 Cent

Da bado uko kwenye fairytales za cupid, huyo 50 Cent si atoe pesa zake zote kwa wale watoto aliowatembelea Afrika tuone hilo penzi kama litaendesheka
 
Last edited by a moderator:
[SIZE=+2]Malaika[/SIZE][SIZE=+2]Angel[/SIZE]
Malaika, nakupenda Malaika.Angel, I love you Angel.

Nami nifanyeje, kijana mwenzio,And I, your young lover, what can I do.
Nashindwa na mali sina, we,Was I not defeated by the lack of fortune,
Ningekuoa Malaika.I would marry you Angel.

Pesa zasumbua roho yanguMoney is troubling my soul

Nami nifanyeje, kijana mwenzio,And I, your young lover, what can I do,
Ningekuoa Malaika.I would marry you angel.
Nashindwa na mali sina, we,Was I not defeated by the lack of fortune,
Ningekuoa Malaika.I would marry you Angel.
Kidege, hukuwaza kidege.Little bird, I dream of you little bird.
Kidege, hukuwaza kidege.Little bird, I dream of you little bird.
Nami nifanyeje, kijana mwenzio,And I, your young lover, what can I do,
Nashindwa na mali sina, we,Was I not defeated by the lack of fortune,
Ningekuoa Malaika.I would marry you Angel.
Nashindwa na mali sina, we,Was I not defeated by the lack of fortune,
Ningekuoa Malaika.I would marry you Angel.
 
Umebanwa hadi umeachia....hahahahahaa. Sasa hata ile namba ya yule nitakutafutia. Au umeshaghairi?

Hapo nimewarahishia tu ila unajua fika huwezi kutoa bila pesa wala huwezi kulinda bila pesa achilia mbali kuongoza.

Hiyo namba basi, ngoja nitafute kwanza pesa maana hata nauli ya kwenda kumtembelea huko alipo sina-pesa noma!
 
kumbe huo ndio mzizi wa fitina, sasa nimeng'amua kwa nini nimenyimwa namba ya simu, nilipokwambia Voda kwa Airtel sipigi na dinner za Serena Hotel zisiwezi. Ngoja nikatafute wale ninaowazidi kipato.

Hahaha wewe Bht alisema haisumbui nibebe ndizi na pilipili kwenye handbag ukinitoa lunch kwa Mama Ntilie

Kisha wanaume wenye kukata tamaa kirahisi wanaashiria hawana 3P....badala ya kusema utatafuta zinizidi unakuja na habari ya kutafuta wa kipato cha chini yako!
 
Pesa inachoweza kukupa ni 'MAHUSIANO' na sio 'MAPENZI' toka kwa mtu mwingine. Yani pamoja na kwamba ina nafasi yake katika mahusiano ili maisha yasonge na muda wa kupendana uwepo huwezi kusema eti ndio 'MSINGI' wa mapenzi. Nyie ndio wale mnaotongozaga kwa pesa, na wadada wenye fikra hizo ndio wale ambao hua wanakimbia pale wallets/bank accounts/mifuko inaponyong'onyea maana mahusiano(sio mapenzi) yanayotegemea pesa kama msingi/kiungo kikuu cha kuwezesha mahusiano hayo hayawezi kuwepo pale pesa inapokosekana.

Mapenzi kama mapenzi hayanunuliwi kwa pesa. Ndio maana wapo watu ambao kwenye milima na mabonde bado wanasimama na wake/waume zao. Tofauti na hao "wafanya biashara"ambao as soon as the money is out of the door, so are they. Wanachofuata na kinachowaweka kwenye mahusiano ni pesa na sio mapenzi.
 
Ila inategemea, kuna wanaume wengine hawana hela na akili zao mbovu. Huyo kumwacha afanye hizo 3Ps ni kumuonea. Bora mwanamke achakarike.
 
Pesa inachoweza kukupa ni 'MAHUSIANO' na sio 'MAPENZI' toka kwa mtu mwingine. Yani pamoja na kwamba ina nafasi yake katika mahusiano ili maisha yasonge na muda wa kupendana uwepo huwezi kusema eti ndio 'MSINGI' wa mapenzi. Nyie ndio wale mnaotongozaga kwa pesa, na wadada wenye fikra hizo ndio wale ambao hua wanakimbia pale wallets/bank accounts/mifuko inaponyong'onyea maana mahusiano(sio mapenzi) yanayotegemea pesa kama msingi/kiungo kikuu cha kuwezesha mahusiano hayo hayawezi kuwepo pale pesa inapokosekana.

Mapenzi kama mapenzi hayanunuliwi kwa pesa. Ndio maana wapo watu ambao kwenye milima na mabonde bado wanasimama na wake/waume zao. Tofauti na hao "wafanya biashara"ambao as soon as the money is out of the door, so are they. Wanachofuata na kinachowaweka kwenye mahusiano ni pesa na sio mapenzi.

jitahidi kusoma posti zote kwa tuo, ni ushauri tu
 
Back
Top Bottom