Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,604
- 1,704
- Thread starter
- #41
Wewe hueleweki! Weka mada yako vizuri ili usije kueleweka visivyo na ulivyokusudia. Unaposema pesa ndiyo msingi mkuu wa mapenzi wengine hatukuelewi kwa sababu tuna ndugu na tumeshawahi kuwa na ndugu ambao kwa kweli hawana na hawakuwa na chochote zaidi ya mapenzi ya kweli.
Wengine wameishi kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 50! Sasa ni wazi walikuwa hawashindi wala kulala njaa lakini pia hawakuwa na 'pesa'. Sasa pesa ndiyo msingi mkuu wa mapenzi...pesa kiasi gani? Za kutosha tu kujipatia mahitaji muhimu au nyingi za kusaza na kumwagia radhi?
Weka kiwango watu tujue unachokiongelea. Kama ni mshahara wa milioni kumi kwa mwezi sema, usiogope.
nimeshakwambia pesa sio kipande cha karatasi au chuma tu, kama hilo huelewi basi tumia tafsiri hii: kuwa na pesa = kuwa na uwezo wa kujikimu/kujitosheleza kiuchumi