Umuhimu wa messenger

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
SAITI kama vile yahoo, hotmail/msn kwa hivi sasa zina huduma inayoitwa
‘messenger’ ambayo huwawezesha watu wawili au zaidi kuzungumza papo kwa hapo
potelea umbali kati yao.
Mathalani, asubuhi hii nilikuwa nikiwasiliana na Dennis David alyeko Hudson,
Texas huko Marekani.
Katika mazungumzo yetu kwa kifupi nilitaka kujua amefikia wapi kuhusu ‘ishuu’
fulani ya kibiashara na tukaweza kuelekezana mengi ya kuweza kulifanikisha jambo
hilo kwa haraka zaidi.
Hiyo ilikuwa ni saa 11 alfajiri ambapo kwa saa za Kimarekani pengine ilikuwa
ndio kwanza saa mbili usiku.
Huduma hii ya mesenja ni muhimu sana kwa wafanyabiashara, wasafiri, wanafunzi na
watu mbalimbali wanaoweza kusaidiwa kufanya kazi yao vizuri zaidi kwa kuwa na
mawasiliano ya papo kwa hapo.
Ili kuweza kuwa na huduma hii lazima kwanza uwe mwanachama wa yahoo au hotmail.
Haitoshi tu hivyo lazima uwe na programu hiyo ya mesenja kwenye kompyuta yako.
Programu hii ni bure na uunachotakiwa kukifanya wewe ni ‘ku-dowload’ au
kuiteremsha programu hiyo toka kwenye mtandao na kuipa hifadhi kwenye kompyuta
yako.
Ukishakuwa na programu hiyo kinachotakiwa sasa ni wewe kuwaandikisha watu
unaotaka kuwasiliana nao ambao huitwa ‘contacts’ zako.
Ili uweze kuwasiliana na mtu unachotakiwa kufanya ni kumtumia ujumbe. Kama yeye
pia yupo kwenye kompyuta yake wakati huo huo ataupata ujumbe huu na kompyuta
yako itaonesha kuwa na yeye pia yuko ‘online’.
Mkishaonana hivi kupitia kwenye kompyuta sasa unatuma ujumbe wako kupitia
kiboksi maalumu cha mesenja katika hotmail au yahoo.
Kiboksi hicho kinakuruhusu wewe kuandika ujumbe na kuutuma papo kwa hapo.
Ukiutuma tu ujumbe ule unaosemeka katika ubao ulioko kwenye kiboksi hicho
ukionyesha mawasiliano kati yako na huyo unayeteta naye.
Kila ukiandika na kutuma ujumbe wako huonekana na yeye anapokujibu ujumbe wake
unaousoma. Yeye huko aliko anaona vivyo hivyo wewe unavyoona upande huu
mwininge.
Wote yahoo na hotmail wanakuruhusu kutumia aina ya maandishi na saizi ya
maandishi unayotka. Kazi kwako ni kuchagua na kuiambia kompyuta jinsi utakaqvyo.
Kwa wale wanaofanya biashara na nchi za nje huduma ya mesenja ni muhimu kwao
ikiwa wana watu maalum wanaoweza kuwasiliana nao.
Kwa mfano kama unataka kununua kitu fulani toka Dubai na una mtu unayemfahamau
huko Dubai basi kwa kutumia mesenja unaweza kumuuliza je, kitu chenyewe
kinapatikana, bei yake ni kiasi gani na nini gharama za kukisafirisha hadi
Tanzania.
Ikiwa unapenda kwenda mwenyewe huko Dubai huduma ya mesenja bado inaweza kuwa ni
ya maadada kwako. Unaweza kumuarifu mtu ikiwa yamebakia masaa machache tu na
ukawa na uhakika wa ni nani atakayekupokea, utafikia mahala gani na kadhalika na
kadhalika.
Kwa wasafiri, mesenja inaweza kuwasaidia kwa njia mbalimbali. Mathalani, kama
unataka kitu fulani au maelezo fulani kuhusiana na anwani au kitu fulani
ulichopoteza unaweza ukawa Nairobi lakini hujui namba ya simu ya mjomba au
shangazi yako nchini Kenya. Unachopaswa kukifanya ni kwenda kwennye internet
café ya karibu na kucheki kama wanaruhusu huduma hiyo bila mikwara na kisha
kuangalia kama kuna jamaa yako kwenye mtandao kwa wakati huo anayeweza
kukusaidia. Huna ulazima wa kurudi tena Tanzania ili uweze kupata simu ya mjomba
huko uliko.
Kwa wanafunzi mifano halisi inaonyesha kuwa wanaokuwa na tatizo kuhusu kupata
maelezo au ‘data’ fulani kwa kutumia mesenja na njia nyingine za mazungumzo
kwenye intaneneti wameweza kutatua shida yao kiurahisi na mara moja.
Mara kadhaa nimeandikiwa na watu na vile vile watu kujiingiza katika mazungumzo
yangu na watu wengine dunaini juu ya hili au lile kuhusu Tanzania na nikawajibu
kwa chini ya dakika moja.
Mana katika dunia hii tuna maktaba nyingi zinazotembea. Yaani kuna watu wanaojua
mengi usiyoyajua wewe. Watu hao kama wako kwenye kompyuta zao ukiuliza chochote
wanaweza kukupa jibu la haraka zaidi kuliko kwenda kutafuta kitabu usichokijua
jina lake wala jina la mwandishi wake.
Katika ofisi zetu mara kwa mara tumekuwa na matatazio ya aina mbalimbali
kuhusiana na intaneneti na kompyuta zetu.
Awali tulijiona pweke na tulilazimika kutoka nje ya ofisi na kwenda kutafuta
msaada nje. Lakini hivi sasa tumegundua kuwa kwa kukaa pale pale kwenye kompyuta
na kutafuta watu wanaojua juu ya ufumbuzi wa tatizo fulani na kuwaomba msaada ni
kitu rahisi na cha gharama nafuu zaidi kuliko kutoka nje ya ofisi.
Kwa hakika sio tu imekuwa rahisi kutatua matatizo yetu lakni vilevile tumekuwa
wanafunzi wazuri zaidi katika kujifunza mambo ambayo zamani tulikuwa tunaona ni
rahisi tu kuwaachia wengine kutafuta na kuyafanyia kazi na sio kukunguja
ufumbuzi wake mezani.
Hivi leo kupitia mesenja na aina nyingine za mazungumzo kwenye intaneti
tunapaswa kujua kitu gani cha kuuliza; kufuatilia maelekezo kwa undani na kisha
kuanza kuyaweka maelezo hayo katika vitendo ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo moja
au jingine.

Utaratibu huu wa kufanya kazi umetufanya sisi kuwa bora zaidi na mahala petu pa
kazi pia kuwa mahala penye mazingira mazuri ya kikazi na hususan katika kutafuta
ufumbuzi wa matatizo fulani fulani.
Kifamilia mesenja inaweza ikatumika badala ya simu na kuweza kutosheleza haja ya
ukaribu kwa wana familia au wale wapendanao na kadhalika.
Kwa mfano, kama baba amesafiri anaweza akazungumza na mkewe, watoto na wana
familia wengine endapo nyumbani kwao wana kompyuta yenye intaneti na wana huduma
hiyo ya mesenja.
Katika mazungumzo yao maama, watoto na wengineo wanaweza kupata maelekezo
mbalimbali ambayo hujiandika yenyewe kwenye kompyuta na kama kuna ‘printa’
inakuwa ni kazi rahisi kuchapa na kuwa na kumbukumbu ingawa bado unaweza
ukahifadhi yote yaliyoendelea kama faili katika kompyuta yako kama huna chombo
hicho cha ‘printa’!
Uzuri wa njia hii ni kuwa hutakuwa unalipa bili ya simu za kimataifa kwa kufanya
hivyo. Wewe utalipa bili ya kawaida ya humu humu ndani kwani huduma ya mesenja
sio simu ya kimataifa. Ni huduma ya bure na ni ule muda wako unaokuunganisha
wewe na anayekupa huduma za intaneti hapa nchini ndio unaostahili kulipiwa.
Watu wengi hawalijui hili na hivyo hulazimika ama kubaki bila mawasiliano wawapo
safarini au kuingia gharama kubwa kuwasiliana na jamaa zao wawapo nje ya nchi.
Kwa wale wenye kompyuta na simu nyumbani kwao wafikirie pia kuwa na intaneti
maana wanaweza kujikuta wanaongeza ndio gharama fulani kwa kuanzia lakini
kutokana na unafuu wa mawasiliano ya mesenja wakajikuta wanaokoa kiasi kikubwa
zaidi cha fedha.
Kiofisi, ni dhahiri kuwa mawasiliano yanayoonekana kuchukua mwaka sasa kufika
mahala yanaweza yakafika wakati huo huo kwa kutumia huduma ya mesenja.
Shida za Wananchi wa Tanzania mikononi mwa vyombo kama mawakala wa huduma
mbalimbali, polisi, mahakama na kadhalika kwa kiasi kikubwa zinaweza kupungua
sana kama kompyuta na huduma kama hizi zikipatikana humo.
Kuna aina ye mesemja pia inayoweza kutumika katika mitandao ya ndani kwa ndani
katika taasisi na hivyo kufanya siri za taasisi zisifuje kirahisi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom