Umuhimu wa Kiarabu kuwa lugha Rasmi Tanzania

blessings

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
6,983
6,237
Huku Taifa likipokea wawekezaji wengi kutoka nchi zinazozungumza lugha ya kiarabu duniani na pia kuwepo kwa fursa za ajira na biashara katika nchi zinazozungumza kiarabu (Morocco, Algeria, UAE, Saudi Arabia, Misri, Libyan n.k) Nafikiri ni busara sasa Lugha ya Kiarabu irasimishwe kwa kuingizwa kwenye mitaala ya elimu kama lugha rasmi ya mawasiliano nchini Tanzania.
 
Ikija kwenye mambo ya uwekezaji bora tujifunze Ki China. Anyway tunatakiwa kuwa na curriculum inayowaruhusu watoto mashuleni kujifunza lugha mbali mbali.
Kifaransa, Kigermani, Kiitaliano Kiarabu , Kijapan etc.

Muhimu kabisa waweke mkazo kwenye English.
Tutake tusitake dunia ya leo ni ngumu Kama hujui English.

Sio lazima kuwe na darasa wanafunzi wanaweza kufanyanya hayo masomo "through correspondence ".
 
Muhimu kitumike kiswahili kufundishia elimu ya juu kwanza kiarabu ni kama lugha nyengine za kigeni. Wakihitajika wazungumzaji wa kiarabu Zanzibar wamejaa kule wanafundishwa mashuleni. Kujua kuongea lugha tofauti ni kitu kizuri.
kiswahili hakiwezi kuwa medium of instruction Tanzania, watu tutakua hata hatuwezi kugusa computer manake computer yenyewe kuijua mpaka uwe na kaung'eng'e ka mbaliii. halafu waTz tutashindwa kupata ajira nje.
 
Kwa upande wa lugha, Tanzania tumechelewa sana sana. Baada ya kuchelewa tumelewa kasumba lugha inayohitajika ni Kiingereza tu. Kwa kweli tulihitaji lugha zaidi mashuleni. Na kwa best practices narejelea watu wa Yuropa. Wale watu wanajifunza lugha nyingi sana mashuleni. Na uelewa wao wa mambo ya kimataifa ni mkubwa zaidi.
 
Wamewekeza lugha unayoitumia sasa, Kiswahili.

Hata wewe ni mwarabu kwa asilimia fulani, zile zile ambazo utasema ni asilimia ya maneno yaliyomo kwenye Kiswahili.

Kiswahili ni Kibantu at large percent na kilikwepo hata kabla ya kuja kwa Arabs.

Percent ya Waarabu katika lugha sio kubwa kuzidi percent ya Bantu languages katika kiswahili. Pili kilikwepo kabla ya Arabs kuja na hata wao wamesema katika documents zai kuwa Azania ilikuwa na Lugha moja kutoka katika branches za tribal languages.

Hatuwezi kusema kiswahili ni kiarabu kwa sababu ya uwepo wa maneno ya kiarabu. Kila lugha ina words kutoka lugha nyingine especially when a new item or object is new to another language au popularity yake.
 
Hata kichina nacho kimeshika hatam yaani bidhaa zao nyingi lazima waweke japo kaneno kamoja ka kichina
 
Back
Top Bottom