Umri gani wa kupishana kati ya watoto?

Ulimakafu

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
29,026
10,673
Wanajamvi hivi ni umri/muda gani wa watoto wanaozaliwa wanastahili kupishana kati yao ili waweze kupata vizuri huduma stahiki na mpango mzima wa afya zao?Je kuzaa nako kunastahili kuzingatia umri?
 
Wanajamvi hivi ni umri/muda gani wa watoto wanaozaliwa wanastahili kupishana kati yao ili waweze kupata vizuri huduma stahiki na mpango mzima wa afya zao?Je kuzaa nako kunastahili kuzingatia umri?

Mi nawapishanisha kwa mwaka mmoja na nusu kisha napiga mimba ingine hivyo hivyo
 
Murefu inategemea kweli ila hata kama ni mipangilio isizidi sana mpaka mnasahau issue ya watioto then ghafla mnapata mwingine
sawa ila kwa hv sasa ukisema umwambie mtu azae kila baada ya miaka mi5 au sita inakuwa ngumu kwan inagetemea kipato na yupo kwny hali gan wakat huo. Hvyo bas ni vizur mtu azae pale anapoona anaweza kuwamudu na kuwalea ni hvyo tuu ila wataaramu wanasema nivizur uzae kila baada ya miaka mitatu au sita ili uwe na trade nzur ya age kwa watoto ila ukifuata hvyo je maisha ya hv sasa utaweza kuvumilia. Na je wewe na mwenzio mnaumri gan?
 
Murefu hapo umenena vyema
Ila mkuu inategemea sana haya mambo na kama kwenye familia hakuna mpango wa kufanya mambo mengine ya maisha kama kusoma au kujiendekeza kielimu. Maana ukisema mzae kila baada ya miaka sita au mitano unafikiria na mwenzako pia nae ana mipango gani. Ila kwa miaka mitatu mitatu sio mbaya sana kupishana maana hapo ujiwekee na malengo yenu kama familia ni nini mnataka kufanya na mipango yenu ya kimaendeleo
 
ni kweli ila kwa mwanamke kama uliolewa una miaka my be 33 ukizaa mara moja tu basi unakuwa umri umeenda sana na ukisema unazaa baada ya miaka mitano inamaana utazaa ukiwa na miaka 39 umri ambao unatakiwa kumpuzika, ila mie nimeolewa nikiwa na miaka 21 nimezaa watoto watatu kwa kuachanisha miaka miwili miwili na sasa first born ana miaka 9,7 5 nakula raha sana.
 
it depend na ratiba na umri.kama umechelewa hata dogo akiwa na miez mi4 unakanyaga moto mpya
 
mimi wa kwangu wanapishana mwaka mmoja tu ili wanyanganyane uji vizuri na pia mama apumzike causd nina mpango wa kuwa na watoto wawil tu
 
Inategemea mnataka kuwa na watoto wangapi. (Mtizamo wangu tu, watoto wawili watatu wanatosha ili kupata muda na nafasi ya kulea na kuhangaikia maisha, sio mnazaaa tu mpaka uzeeni. Mkizaa mapema, mnapumzika mapema. Watoto wenu wanakuwa na kufikia umri wa kujitegemea mkiwa bado hamjazeeka kabisa).

Watoto wakiwa hawakupishana sana umri (kati ya miaka 2 na 3), inakuwa rahisi katika malezi kwani huduma zao zinalingana, mnakuwa mnatatua mataatizo na mahitaji mawili kwa wakati mmoja: vyakula, mavazi, elimu, afya...michezo n.k.

Kuhusu umri mzuri wa kupata watoto, ni kati ya miaka 25 na 35. Mara nyengine inaweza kushuka hadi 20 kwa mwanamke na kupanda hadi 40 kwa mwanamume. Chini au zaidi ya umri huo ni hatari kwa afya, sio ya mama tu bali hata malezi yanakuwa tabu kidogo. Fikiria mnazaa na 45, mtoto wenu wa kwanza akifika 20 nyinyi mko above 60. Jaribuni tafauti kati yenu na watoto isizidi miaka 25, mfano, wewe uko na 40 mtoto yuko 15.
 
Back
Top Bottom