Umoja wa vijana bila kujali itikadi za vyama

NGUVUKAZI

New Member
Sep 8, 2009
1
0
Hello Wakulu,
Mi ni mgeni humu jamvini.Naomba ukaribisho.
Sasa kuna mpango wa kuanzisha Umoja wa vijana wenye mlengo wa Transformational state.Yaani umoja wa vijana utakao ibadilisha nchi katika nyanja mbalimbali.
JINA:Tanzania Youth Transformational Association (TAYOTA)

MALENGO:1:Kuelimisha vijana jinsi ya kujiendeleza kielimu na kuwasaidia na kuwasilisha mawazo yao panapohusika
2:Kuwaendeleza vijana kimichezo kulingana na uwezo wao na kugundua vipaji mbalimbali na kuviendeleza
3:Kusaidia vijana kwenye ujasiliamali na kutoa elimu hiyo.

Sasa wanajamii tunahitaji mchango wenu ni jinsi gani tunaweza kuiendesha huu umoja ili vijana wote nchini (walio wengi hawawezi ku access internet) waweze kupata elimu na kuendelezwa kimaisha.
Umoja huu utakuwa ndiyo sauti ya vijana kitaifa .Yaani chombo cha kuwasemea vijana na kuwasaidia vijana.Hata mambo ya kutafuta ajira kitahusika moja kwa moja katika kutatua tatizo hili .
Wanajamii je,muuno wake uwe vipi? makao makuu yake yawe wapi?ni vijana wa aina gani waendeshe umoja huu?Je umoja huu ufadhiliwe na nani?jamiiforum au vijana wenyewe au serikali kupitia wizara ya vijana,wizara ya michezo,wizara ya elimu?JF the great thinkers tunaomba tusaidie kutoa maoni juu ya umoja huu .Maoni ya JF ndiyo yatakayokuwa sera ya umoja huu.
Nawakilisha.
 
umoja kuendeshwa na wizara chini ya CCM au? manake CCM wanayo uvccm sasa sijui ni nini unamaanisha.
 
jamani mweleweni kwanza, ni umoja wa vijana despite itikadi za kitaifa, mi naona ni jambo zuri na kama vijana wakiweza kuunganishwa wakapata sauti, inaweza kuwa njia ya ukombozi kwa hili taifa.
 
Back
Top Bottom