Umoja wa upinzani? Lini utakuwepo

Kila chama kina ideology yake kwa hiyo kuunda alliance ni kukosa dira. Cha maana kila chama wajitahidi kuuza sera zao kwa wananchi wapate wafuasi wengi kipatikane chama strong. Vinginevyo ni kuwadanganya wananchi wawape madaraka bila kujua mtawafanyia nini kwa maisha yao.
 
Da watu wanakurupuka tu kujibu thread bila hata ya kupima kuwa inaletwa na nani na kwa lengo gani. Ndiyo maana hoja hizi za ovyo zinakuwa nyingi sana.

Inawezaekanaje mtu anayebomoa sana upinzani humu mpaka kwa kutumia udini anakuja na thread eti inayodai muungano wa upinzani na watu wala hawajiulizi?

Ndugu yangu wewe endelea na kazi yako uliyotumwa ya kuboa upinzani!
 
Wataungana vp wakati ndani mwa nyama vyao humo humo kuna makundi, hadi watakapoyamaliza ndo wanaweza kuingi next stage ya kuunda muungano wa pamoja, may be next 20 years! i bet
 
Kulikuwa na jitahada za kuwepo umoja wa vyama vya upinzani Tanzania, wakati fulani niliona Chadema, CUF, NCCR-mageuzi na TLP wakisema wameunda umoja wa vyama vinne?

Swali umoja huu bado upo? na nani alikuwa mwanzilishi na malengo yao yalikuwa nini?

Kipi kimeshindakana au kimekwamisha muungano huu je muungano utakuwepo huko tunakoenda? if yes when?

Ukishasema upinzani, inamaana kupingana. Si rahisi kwa viongozi tulio nao kwenye vyama vya upinzani kuungana, maana wao kwa wao wanapingana ndani ya vyama vyao, kwa hiyo ni vigumu sana kwa vyama vya upinzani kuungana. Kila kiongozi atahitaji awe juu ya mwingine- (Awe na nafasi nzuri kuliko mwingine)
 
kwani biashara ya Pombe ni haramu...wewe ni mjinga na punguani .
kudaiwa na NSSF kwani ni wizi.....hauko kisasa.
Lakini ni kiongozi makini mwenye historia ya kua mbunge.......
Sikila msomi anakarama ya uongozi, unadhani kuwa profesa ni uongozi.
Bado naamini Libumba ni kiongozi asie faaa katika siasa na ndio maana muungano hauwezi kufanikiwa.

Lipumba si kiongozi bali anategemea hisani ya Maalim seif ili aweze kuwa mahali alipo, vinginevyo Lipumba ni boya tu, hawezi kuwaunganisha wapinzani. kwanza habari za ndani ni kwamba hata yeye na mwenzake Mbatia wako kwenye payroll ya Rostam. Sitashangaa Zitto Kabwe akiungana nao!!!
 
Da watu wanakurupuka tu kujibu thread bila hata ya kupima kuwa inaletwa na nani na kwa lengo gani. Ndiyo maana hoja hizi za ovyo zinakuwa nyingi sana.

Inawezaekanaje mtu anayebomoa sana upinzani humu mpaka kwa kutumia udini anakuja na thread eti inayodai muungano wa upinzani na watu wala hawajiulizi?

Ndugu yangu wewe endelea na kazi yako uliyotumwa ya kuboa upinzani!

Huyu Tumaini hajawahi kuwa mpinzani. Ni chama la kijani.
 
Hapana bwana aiwezekani kabisa Zitto nae umuweke huko; si ni juzi tu Mh katuhamasisha na OPERATION SANGARA. Leo nae umchanganye huko mmh mmh.

Na kasema uongozi wa CCM sasa una nusu karne tusiuchague tena; hila akutuambia nani tumachague kwani chama chao so far awajataja mgombea wao.

Au labda wanasubiri wiki moja kabla ya uchaguzi ndio watupe option maana nao hata sijui kama wanaelewa ni maana ya campaign haya bwana tunasubiri chadema 'Doyens' wa make their decision.

No need for campaign watanzania watapiga kura tu kisa chadema kaazi kweli kweli.
 
You can be better than this crap, stay away kama huna hoja..
 
Huyu Tumaini hajawahi kuwa mpinzani. Ni chama la kijani.
Inasemekana walitaka kuungana issue ikiwa mode of payment, wakakubaliana kwamba 40%,30% and 30% operation cost za ushirikiano zilipwe na CUF, Chadema and TLP/NCCR respectively..kama kawaida..watu wa north kwa mihela...chadema wakazira kulipa cost..mfarakano ukaanza...(CUF website)

In BTWN, huku JF chama gani hakitakiwi? any way good guess folk
 
Hapana bwana aiwezekani kabisa Zitto nae umuweke huko; si ni juzi tu Mh katuhamasisha na OPERATION SANGARA. Leo nae umchanganye huko mmh mmh.

Na kasema uongozi wa CCM sasa una nusu karne tusiuchague tena; hila akutuambia nani tumachague kwani chama chao so far awajataja mgombea wao.

Au labda wanasubiri wiki moja kabla ya uchaguzi ndio watupe option maana nao hata sijui kama wanaelewa ni maana ya campaign haya bwana tunasubiri chadema 'Doyens' wa make their decision.

No need for campaign watanzania watapiga kura tu kisa chadema kaazi kweli kweli.

Wewe huwajui wanasiasa!! Subiri and watch this space utaniambia kama huyo mhamasishaji wako hayuko kwenye payroll ya Rostam. It s a matter of time
 
Kuna chochote mdadala kama ujumbe wa mwaka mpya kutoka upinzani..au bado wamelala...JK kashatoa hutuba ya mwisho wa mwaka..wapinzani za kwao ziko wapi?
 
umoja wa wapinzani hautowahi kutokea kwa vile viongozi wa upinzani hawana nia ya kuikomboa nchi yetu wana nia ya kukomboa matumbo yao kama ccm.

Mwangalie Mrema anavyotangatanga. Miezi 10 kabla ya uchaguzi mkuu badala ya kuwa pamoja na wenzie wa upinzani kupanga mikakati ya kuisinda CCM, yeye yuko busy kumpigia debe Kikwete.

Mwangalie Zitto, mguu mmoja nje mguu mmoja ndani ya CHADEMA. CCM wakimuahidi kumpa uwaziri basi hakitakuwa kitu cha kushangaza kusikia na yeye kuvaa jezi zenye rangi mbaya za CCM, Upinzani nao unastahili lawama chungu nzima kwa hali ya nchi yetu.
 
wewe ni mgonjwa ....nenda kaongee na wajinga wenzako hukooo, tunaongelea umoja wa upinzani wewe unaongelea ugomvi wako na lipumba umetumwa?

Tumain nafikiri wewe ndo umeleta thread hii lakini unakosa uvumilivu, jaribu kutafuta lugha nzuri kumwelewesha mwenzako kama amepotoka au ameteleza kidogo maana tunatofautiana kimawazo na hata uwasilishaji wenyewe.
 
Kuna chochote mdadala kama ujumbe wa mwaka mpya kutoka upinzani..au bado wamelala...JK kashatoa hutuba ya mwisho wa mwaka..wapinzani za kwao ziko wapi?

CHADEMA wako busy kugombana na kufukuzana ndani ya chama. Sijui nani atakuwa wa kwanza ndani ya chama hicho kurudisha kadi ya chama 2010. TLP ndiyo hivyo tena wako busy kujibaraguzabaraguza kwa Kikwete labda chama hicho kimeshakuwa tawi la CCM, CUF wako busy kufuatilia muafaka wao na CCM ili 2010 iundwe Serikali ya mseto kule Visiwani na vilivyobaki sijui kama vina hadhi hata ya kuitwa "vyama vya upinzani"
 
Tumain
Ni umoja gani wa upinzani unaosema, wa vyama vya siasa wa viongozi au wa wananchi?
Kama ni wa vyama, vyama vyenyewe CUF+Chadema+TLP+UDP+NCCR+... kifupi hautakuwepo i dont see light at the end of the tunnel, opposition alliance is like a dream especially in Tanzania, Lengo la umoja nikusaidiana lakini kama unaona mwenzako hakusaidii anakusaliti umoja hauna haja tena na hakuna mtu atakayekulaumu, mfano wakati wa uchaguzi mdogo Tarime vyama tulivyokuwa tunategemea visaidiane ndivyo vikawa mpinzani mkuu wa CHADEMA kuliko hata CCM wenyewe.
Umoja hautakuwepo kwa sababu kila chama kina ideology yake malengo yake madhumuni yake na sera zake. Chadema kina sera ya majimbo sijui kama CUF wana sera hiyo hata kama wakiwa na sera hiyo watatofautiana wakati wa kuiuza kwa wananchi. Afterall viliwahi kuunda umoja ukaitwa UDETA matokeo yake ukaingiliwa na virus ukafa lilikuwa ni somo tosha kwa upinzani.

Kama unasema umoja wa Viongozi, viongozi wenyewe ni Lipumba+Mbowe+Mrema+Cheyo+Mbatia+Mtikila+... nawaheshimu sana hawa viongozi kwa sababu si kila mtu anaweza kujitolea na kuwa mstari wa mbele kutetea masilahi ya Taifa tusiwalaumu, ukimulaumu Lipumba au Mbowe utakuwa hujawatendea haki jaribu wewe kuwa mwenyekiti uone. Ingawa lengo lao ni moja lakini kila kiongozi niliowataja ana maslahi yake, wengine wako kweli kwa maslahi ya wananchi lakini wengine wako kwa maslahi binafsi hiyo ni hulka ya binadamu.

Kwa mawazo yangu kwavile kila mmoja anajali maslahi yake sidhani kama watakuja kuwa kwenye chungu samahani chama kimoja. Kila mtu atataka awe ndiye na sauti kuu (boss) nani atakubali? hebu niambie wakiungana Mtikila atataka awe msemaji mkuu Cheyo mtunza fedha Mbatia naye atazitaka mwisho ni kushikana mashati kugombea uenyekiti kama yaliyotokea kati ya Mrema na Marando wakati wa NCCR kule Raskazone Tanga. Kwa hiyo ni vigumu sana kwa viongozi wetu tulionao kuungana unahitajika ukomavu hasa wa akili kisiasa si lazima uwe wa darasani hekima na busara kubwa.

Kama unasema Umoja wa wananchi, kwa mawazo yangu nafikiri unawezekana, unawezekana kwa misingi ifuatayo; Ni rahisi kuwaunganisha wananchi wa kawaida (wanachama) kuliko kuwaunganisha viongozi. Lengo kuu la wananchi 'ninaposema wananchi namaanisha wanachama vilevile' si muungano wa vyama ni kuwa na maendeleo kwenye jamii zao kwenye familia zao. Wanataka kiongozi au chama kimoja chenye kuwapa matumaini iwe kwa vitendo au hata kwa ahadi. Chama kimoja chenye nguvu na itikadi moja chama kinachoonekana kuwajali kuwasikiliza na kuwa karibu nao ni kama mtoto anavyopenda. Chama kitakachowasemea kiwe kama kipaza sauti chao pindi wanapokuwa na tatizo wapweke. Kwa sasa wanajiona kama wapweke chama walichokuwa wanakitegemea CCM hakiwajali tena kimewasahau. Hawahitaji muungano wanahitaji chama chenye nguvu hata kikiwa pekee.

Nirahisi kuwaunganisha na kuwaongoza wananchi wa kawaida milioni 5 kuliko kuwaunganisha viongozi wawili au vyama viwili.
 
Kuna chochote mdadala kama ujumbe wa mwaka mpya kutoka upinzani..au bado wamelala...JK kashatoa hutuba ya mwisho wa mwaka..wapinzani za kwao ziko wapi?

Kwani CCM wametoa ujumbe gani? ujumbe uliotolewa ni wa rais kama unataka kutuambia rais Kikwete ni wa CCM tu tuambie, sasa kama hata humu JF tunashindwa kutofautisha viongozi wa kitaifa kama rais na chama uuuuwiiiiii......itakuwaje mtu ambaye hakuuona mlango wa darasa atafikiri hata katibu kata ni wa CCM, kweli tuna safari ndefu.
 
Fikra kama zako za kuwabeza wenzako ndiyo tatizo.
Kinachotakiwa ni kuwa vyama vya upinzani [at least vile vikubwa] Viwe na vision moja kwanza halafu view na common strategy na vitekeleze mipango yao kama watakavyo kubaliana na viongozi viache umimi. Kwa maoni yangu viongozi wa upinzani kila wanavyo kaa pamoja na kupanga mikakati kila mmoja anafikiria atakuwa katika nafasi gani na akiona kuwa hafaidiki huanzisha malumbano na nafasi ya kushirikia inayayuka. Hivyo adui mkubwa wa upinzani na wapinzani wenyewe lakini kwa sababu wako obssessed na self interests wanatafuta scape goats. Hali hii ikiendelea watakuwa backbenchers siku zote sijui hii generation ya kina zitto lakini nayo vilevile inawekewa mizengwe kwani kila wanapokuwa na mawazo mbadala basi wanapewa labels za ajabu IDUMU TANZANIA WHERE TUNABISHANA BILA KUUANA
 
CHADEMA wako busy kugombana na kufukuzana ndani ya chama. Sijui nani atakuwa wa kwanza ndani ya chama hicho kurudisha kadi ya chama 2010. TLP ndiyo hivyo tena wako busy kujibaraguzabaraguza kwa Kikwete labda chama hicho kimeshakuwa tawi la CCM, CUF wako busy kufuatilia muafaka wao na CCM ili 2010 iundwe Serikali ya mseto kule Visiwani na vilivyobaki sijui kama vina hadhi hata ya kuitwa "vyama vya upinzani"

CCM wako bize kuunda tume za kuchunguzana wenyewe kwa wenyewe, nasikia hata kwenye tume ya Mwinyi hawaamianiani Msekwa hawaamini wenzake itabidi CCM waunde tume nyingine kuichunguza tume ya Mwinyi ile ya watu wanne, makubwa kweli kweli.
 
Kulikuwa na jitahada za kuwepo umoja wa vyama vya upinzani Tanzania, wakati fulani niliona Chadema, CUF, NCCR-mageuzi na TLP wakisema wameunda umoja wa vyama vinne?

Swali umoja huu bado upo? na nani alikuwa mwanzilishi na malengo yao yalikuwa nini?

Kipi kimeshindakana au kimekwamisha muungano huu je muungano utakuwepo huko tunakoenda? if yes when?

Rudi Nyuma shetani!
 
Ukishasema upinzani, inamaana kupingana. Si rahisi kwa viongozi tulio nao kwenye vyama vya upinzani kuungana, maana wao kwa wao wanapingana ndani ya vyama vyao, kwa hiyo ni vigumu sana kwa vyama vya upinzani kuungana. Kila kiongozi atahitaji awe juu ya mwingine- (Awe na nafasi nzuri kuliko mwingine)

Chukua tano! Hawa jamaa wala hawaeleweki, sijui wanapingana wao kwa wao au wanaipinga CCM. Ila kwa imani yangu ni kwamba huko upinzani kuna vyama vya upinzani kweli na pia kuna vyama vilivyoanzisha na CCM kuvipinga vyama vya upinzani. Na kwa mtindo huo wala tusitarajie wapinzani kushinda uchaguzi, manake wengi wao wapo kwa ajili ya kuitengenezea njia CCM. Na hapo ndipo ambapo mimi hujiaminisha kwamba upinzani wa sasa hauwezi kushika nchi. Upinzani utakaoshika nchi ni ule wa kumeguka kwa CCM, jambo ambalo wengi wenu huwa mnanipinga, lakini huo ndo ukweli na ndilo ninaloliona mimi.
 
Back
Top Bottom