Umoja house experience!

Starworld

Member
May 3, 2009
18
1
Wadau wa Umoja House salaam!
Nimeona nisilifumbie macho suala hili maana linaharibu uzuri wa Mjengo mzima na kitendekacho humo ndani.

Awali ya yote napenda kuzipongeza balozi za Uingereza, Uholanzi na Ujerumani kwa kujipanga vizuri na kushirikiana kuweka jengo zuri, safi na la kisasa ili kufanyia shughuli za kibalozi na pia ushirikiano wa kimaendelea unaosaidia nchi yetu kusukuma gurudumu la maendeleo.

Aidha niwapongeze pia kwa kutoa ajira lukuki kwa watanzania wenzetu pale kuanzia ulinzi hadi visa na usimamizi wa miradi ya maendeleo kupitia taasis kama DFID n.k.

Kero yangu inahusiana sana na walinzi walioajiriwa kulinda pale getini.Hawa ni kero kubwa na kwa kiasi kikubwa wanazidhalilisha balozi husika.Ukiingia tu eneo la karibu kuanzia parking ambazo kwanza siyo za UMOJA HOUSE unakumbana na hawa Ultimate Security- wataanza kukutishia maisha kisa parking ili uwape kitu kidogo!

Ukiingia eneo sasa la mjengo ndio balaa.Wakijua umefuata visa utaipata fresh.Wataanza kukuzungusha kuwa muda bado.. mara hujajaza fomu husika, mara huwezi kupata visa..mradi wakupandishe presha tu.Ukifanikiwa kuingia na kufanya shughuli zako, ukitoka lazima wakutoe upepo na kisingizio chao eti hawana kitu kabisa na kuwa watakusaidia ili mambo yako yawe fresh! LOL MAKUBWA! Kuna ushirika gani kati ya walinzi hawa na wafanyakazi wa ubalozi kwenye kutoa viza?KWANI BALOZI HAMLIPI VIZURI ILI WALINZI HAWA WAWEZE KUMUDU MAISHA?

Kero nyingine hasa inaelekezwa kwa ubalozi wa Uingereza. Kabla ya kulalamika, nawapongeza sana kwa mfumo wao mpya wa ku apply kupitia mtandao ( online) maana hili limewezesha kuondokana na zile foleni za kulala pale nje ya ubalozi ili kukesha uwahi nafasi kesho yake.Hili lilikuwa linatudhalilisha sana watanzania hivyo tunashukuru kuturudishia utu wetu.

Hata hivyo, utaratibu wao wa kutokuwa na mahojiano ya ana-kwa ana au kwa wafanyakazi wao kutokuwa na msaada kwa waombaji ili angalau kuwaonyesha wapi kuna upungufu katika application ili mapungufu hayo yarekebishwe kabla ya karatasi za maombi na passport kwenda Nairobi ni kitu ambacho hakiwapi maksi ubalozi.

Haiyumkini kwa jinsi watanzania walivyo, bado wanahitaji human touch katika mambo mengi. Inashangaza na kusikitisha pale passport yako inapopelekwa Nairobi baada ya kulipa malaki ya fedha, inakaa huko karibu mwezi halafu unakuja kuambiwa kuwa maombi yako hayakukamilika - kwamba hukuweka barua ya mwajiri wako, au hukuambatanisha hati mbalimbali etc! Hivi kama maafisa viza pale wangemwambia muombaji alete hati hizo , si ingewezekana kurekebisha na kuokoa pesa za mhusika?

Jamani Ubalozi wa Uingereza mjirekebishe kwenye hili kwa maana mnapochukua 450,000/ au 150,000/- za muombaji( kutegemeana na muda anaoomba) huku mkijua kabisa angeweza kurekebisha hati zake akapewa viza, hamuoni mnawaibia watanzania? Kwanini nyie mkija kwetu tunawapa viza zenu pale eapot na hatuwahangaishi kama mnavyotufanyia? Kwamba watanzania ni maskini hivyo hamuwahitaji kule kwenu, kumbukeni siyo kila mtanzania anataka kuzamia uingereza! Wengine wana maisha yao mazuri sana Tanzania, huko kwenu wanaenda kibiashara kama na nyie watu wenu wanavyokuja hapa kwetu hivyo acheni dharau!

Nawapongeza sana Ubalozi wa Ujerumani hasa wafanya kazi wa viza maana wao kwa kweli hawako kama kikwazo kama wenzao ubalozi wa Uingereza bali wapo pale kama wawezeshaji na hiki ndicho kinachotakiwa na inashangza iweje majirani walio karibu vile kiofisi na hata ki nchi kuwa na utendaji tofauti vile.
HONGERA UJERUMANI.... muendelee hivyohivyio maana hii ndio haswa ushirikiano wa kimataifa ambapo nchi zote tunaheshimiana.

HILI SIO JUNGU BALI NI UJUMBE MAHUSUSI..JIREKEBISHENI MAANA NAJUA HUWA MNAINGIA HUMU JF.
 
hao alinziwa ULTIMATE ni kweli wanapiga mizinga na kama unavyojua mara nyingi unaenda pale kwa appointment ( hasa visa section) kwa hiyo mtu anapokuletea longolongo hapo nje some times unatoa hata elfu ili aachane na wewe uwahi kuingia,ila kwa kweli wanaboa, nimeshuhudia nilipokuwa nafuatilia visa yangu, its terrible, waelewe kila mtu ana shida zake, they need to change
 
Ndugu Starworld

Ninavyofahamau kwenye ile website all the requirements are stipulated + ukijaza zile fomu online kwa ukamilifu ndio unaweza ku-print mwishoni.....kama kuna important fields hujajaza sidhani kama utaweza kwenda next page.

Cha msingi kuwa na all the requirements as your check list, kabla ya ku-submit hakikisha imekamilika..........

Pili, utaratibu wa sasa umewekwa na Home Office UK, pengine ungeweka copy ya ujumbe wako kwa lugha yao pia ili uwatumie nakala yao huko
 
Hata hivyo, utaratibu wao wa kutokuwa na mahojiano ya ana-kwa ana au kwa wafanyakazi wao kutokuwa na msaada kwa waombaji ili angalau kuwaonyesha wapi kuna upungufu katika application ili mapungufu hayo yarekebishwe kabla ya karatasi za maombi na passport kwenda Nairobi ni kitu ambacho hakiwapi maksi ubalozi.

Starworld, umenena ndugu yangu. Halafu uwakute wadada fulani hivi wawili, hasa yule mwenye dreads. Afadhali na yule mkaka mnene angalau ana utu.

Yaani, ingesaidia SANA kama, pamoja na ubize wao, walau wangepitia makabrasha na muombaji ili kucheki kama kila kitu kipo.
 
Ndugu Starworld

Ninavyofahamau kwenye ile website all the requirements are stipulated + ukijaza zile fomu online kwa ukamilifu ndio unaweza ku-print mwishoni.....kama kuna important fields hujajaza sidhani kama utaweza kwenda next page.

Cha msingi kuwa na all the requirements as your check list, kabla ya ku-submit hakikisha imekamilika..........

Pili, utaratibu wa sasa umewekwa na Home Office UK, pengine ungeweka copy ya ujumbe wako kwa lugha yao pia ili uwatumie nakala yao huko

Kama alivyosema Ogah, ni kweli utaratibu umewekwa na haina ubishi kuwa ndicho kinachopaswa kufuatwa.Lakini kama alivyosema mtoa mada, ubalozi hauoni haja ya kumsaidia Mtanzania kufanikisha azma yake hasa pale wanapoona kabisa kuwa pesa ya viza itaenda bure ilhali wanaona kuwa fomu hazijakamilika? kwanini wapokee pesa na fomu huku wakijua kuwa hazitafika popote?
Je swala la rushwa?
 
Kwa kawaida kwenye balozi mbali mbali huwa kuna taratibu za ku-vet docs kama zimekamilika kabla hata hujalipia........kama hili halifanyiki kwa balozi ya Uingereza, ni bora wakashauriwa ili warekebishe...........
 
Haya malalamiko mnayaandika formally kwenye balozi husika au ndiyo yanaishia hapa JF?

Pia si kila mtu mwenye access ya mtandao.
 
Acheni kulalamikia nchi za watu bana. Aaaah....kwani ukinyimwa viza ndo mwisho wa maisha? Kama watu hawataki wewe uende nchini kwao basi....sio kulia lia kaa mtoto aliyenyimwa peremende. Miafrika bana..
 
Starworld, ili la walinzi wa ultimate security kuomba pesa ya maji ya kunywa or nauli ni la kweli.Sometime wanalazimisha kukuzoea ili wapate gia ya kukuingia...ukiwaambia huna kitu hawakawii kusema hata kama una mia niachie itatosha kwa maji.

Nami nawapa "big five" wafanyakazi wa Germany embassy upande wa Visa kwa huduma safi.
 
Starworld, umenena ndugu yangu. Halafu uwakute wadada fulani hivi wawili, hasa yule mwenye dreads. Afadhali na yule mkaka mnene angalau ana utu.

Yaani, ingesaidia SANA kama, pamoja na ubize wao, walau wangepitia makabrasha na muombaji ili kucheki kama kila kitu kipo.

Injinia... hujakosea - kweli mkaka bonge anaonekana ana utu kuliko wadada wale.Lakini nadhani tatizo liko kwenye mfumo zaidi kuliko watendaji.Ninachokiona tatizo ni kule kutokujali kuwa watu wa nchi maskini wanapoteza pesa kwa sababu zisizo za msingi.Vetting ya application ilipaswa kufanyika DSM kabla ya kupeleka NRB.Wakati unasubiri mwezi mzima only kuja kuambiwa hukukamilisha ungeweza kutafuta safari nchi nyingine hasa kwa wafanyabiashara maana siyo lazima kwenda Uingereza tu.
 
Haya malalamiko mnayaandika formally kwenye balozi husika au ndiyo yanaishia hapa JF?

Pia si kila mtu mwenye access ya mtandao.

Unajua Mkuu, malalamiko yanayotolewa kwa njia ya alternative/new media huwa na faida ya kupata maoni mengi zaidi kuliko kuandika barua ya mtu mmoja kuipeleka ubalozini.Nina uhakika kabisa kuwa kila ubalozi unakuwa na mtu wa media ambaye kazi yake ni kuangalia yasemwayo na eneo mojawapo nijualo huliangalia ni pamoja na popular blogs kama JF.Nina uhakika kabisa haya maoni watayaona na kuyatolea ufafanuzi na hata kuchukua hatua kurekebisha.Mifumo na taratibu hubadilika maana siyo msahafu.
 
Acheni kulalamikia nchi za watu bana. Aaaah....kwani ukinyimwa viza ndo mwisho wa maisha?

Miafrika ndivyo yalivyo sijawahi sikia mtu kanyimwa visa ya kwenda Palestina, Iraq, Somalia, Sudan huko mbona watu hamlilii kwenda au mntaka kwa wazungu tu?
 
Acheni kulalamikia nchi za watu bana. Aaaah....kwani ukinyimwa viza ndo mwisho wa maisha? Kama watu hawataki wewe uende nchini kwao basi....sio kulia lia kaa mtoto aliyenyimwa peremende. Miafrika bana..

Julius una point kabisa halina ubishi.Huwezi kulazimisha kwenda kwa watu.Lakini unasahau kitu kimoja - hapa hakuna anayelialia... bali tunatoa maoni yetu kwa tatizo ambalo lipo.Hapa kuna watu wana sababu za msingi kutaka kwenda nchi fulani na kushindwa kwao kwenda hakutokani na kitu kingine bali uzembe wa hao wenye kuprocess viza.Hakuna ubaya kuwaambia ukweli.
 
Miafrika ndivyo yalivyo sijawahi sikia mtu kanyimwa visa ya kwenda Palestina, Iraq, Somalia, Sudan huko mbona watu hamlilii kwenda au mntaka kwa wazungu tu?

Wewe sasa unachekesha lol
Kusafiri kuna malengo ati... sasa utaenda Iraq au Somali kufanya nini? Somalia utaenda kusoma au biashara?
 
Mkuu Starworld,

Mimi nafikiri suala lililopendekezwa na mkuu Ogah ni zuri sana.

Unachotakiwa kufanya ni kufanya hio "online application" kwa kujaza fomu yote kwa ukamilifu na ukiishafanya hivyo unakuwa una uhakika wa kuitwa kwenye interview.

Cha msingi ni kuhakikisha kwamba umetimiza "requirements" zote na hutarajii kurudishiwa maombi yako kwa namna yoyote ile.

Maombi mengi siku hizi yanakuwa "scrutinized" sana na wewe uwe na nia hasa ya kwenda mamtoni.

Kuhusu hao walinzi wa Ultimate Security ni kwamba wao wanaona kwamba hapo ubalozini tayari wapo Ulaya na wana nafasi ya kukejeli na kudhalilisha watu ama kisaikolojia au kwa nafasi yao, lakini hawajui kuwa wanafanya moja ya kazi ya chini sana.

Cha kufanya ni kwamba inabidi ukienda hapo uwape wanachotaka na uandae mpango na ubalozi kwa kusaidiana na TAKUKURU.

Ni hayo tu.
 
Mkuu
Asante kwa ushauri wako.Napenda kukuhakikishia kabisa kuwa nilifanya online application na nika submit maombi yangu na viambatanisho husika.Nikaonyesha tarehe ninayotaka kusafiri, wakaniambia nitaweza kupata viza kwa wakati ijapokuwa siku niliyopanga kusafiri ndio siku walisema passport itatoka kutoka NRB.Nilipoenda siku yenyewe wakati na ticket nimeshakata, naambiwa documents zangu zimerudishwa hazijakamilika! Hebu nikuulize, je walipokuwa wanaangalia hati zangu na kuniambia nitapata viza siku hiyo ya safari hawakuwa wameona upungufu?Kwanini wakae na passport yangu wiki 3 halafu warudishe na jibu la utata namna ile? Kama ni fursa ya biashara je itakuwa inangoja? wangenikatalia palepale si ningetafuta nchi nyingine? Yako mengi sana ya kuuliza ila sitaki kuanika kila kitu hapa maana ni mambo binafsi.Ujumbe ninaotaka ufike ni kuwa1. Wakomeshe rushwa kwa walinzi 2. Waweke uchujaji wa hati hapo ubalozini viza section ili mtu asipoteze muda.Waige mfano wa ubalozi wa Marekani ambapo kama hutapata viza au karatasi hazijakamilika unajua hapo hapo na kurekebisha hati zako au kupanga safari nyingine.Tusipotezeane muda na pesa maana vyote ni rasilimali adimu.
 
Mkuu pole sana kwa hilo.

Cha kufanya ni kuwasiliana na huo ubalozi kwa kuwasilisha malalamiko yako na wazungu (sio waafrika) wanaweza kusoma na kuelewa na pengine kupitia upya maombi yako provided kwamba umetimiza masharti yote.

Mimi napendelea mtindo wa kusailiwa case worker huku akiwa na documents zote mkononi, na mawazo yangu ni kwamba unapofanya online application baadae ndio unaitwa kwa interview huku wao wakiwa na documents zako zote na baada ya hapo utajua kuhusu decision yao.

Sasa ulioeleza hapo juu yana utata kidogo na inabidi uwasiliane na ubalozi ukieleza dhamira yako ya kwenda Ulaya na pia kulalamika kuhusu hao walinzi.
 
Ultimate security nao wamekuwa kama G4S. uchuro mtupu!. Jana nilikuwa ninasoma gazeti moja nchini Kenya, juu ya skendo za G4S, njaa njaa njaa tupu. Makaburu wamekuja kuchota kwenye migongo ya wa Tzs, ndiyo maana mishahara ya walinzi wao, uchuro mtupu!
 
dah wale walinzi wapale wanapenda sana kutoa watu upepo.....eti wanaomba hela ya chai.....wapuuzi kabisa.....utawala wa pale lazima wafanye kitu kuzuia hali hii isiendelee kwani ni kero kabisa!
 
Back
Top Bottom