Umma unataka majibu ya kina sakata la Jairo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
Mkutano wa sita wa Bunge ulimaliza wiki iliyopita huku serikali ikiomba kupewa muda zaidi wa kufanyia kazi maazimo ya Bunge juu ya taarifa teule ya kamati ya Bunge uliyoundwa kuchunguza vitendo vya kuchangisha fedha vilivyofanywa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, David Jairo. Maazimio hayo pia yaliwagusa Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Philemon Luhanjo na

Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu wa serikali, Lodovick Utouh.
Luhanjo na Utouh wanadaiwa kuwa ama walijaribu kumsafisha Jairo baada ya Luhanjo kumwagiza Utouh kufanya ukaguzi juu ya

tuhuma dhidi ya Jairo zilizokuwa zimewasilishwa bungeni kwamba alikuwa amechangisha mamilioni ya fedha kutoka taasisi zilizochini ya wizara yake kwa madhumuni ya kufanikisha upitishwaji wa bajeti, bila kuwa na kibali cha kufanya hivyo.

Taarifa ya utekelezaji wa maazimio hayo yalitarajiwa kuwasilishwa katika mkutano uliomalizika wiki iliyopita, lakini serikali iliomba muda zaidi kwa kuwa kuna mambo kadhaa ambayo bado ilikuwa haijakamilisha kuyafanyika kazi, kwa maana hiyo sasa taarifa hii itawasilishwa bungeni katika mkutano wa Aprili mwaka huu.

Pamoja na ukweli kwamba ni haki ya serikali kuomba muda wa kujipanga kabla ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge bungeni; kwanza, ili kutoa taarifa ya kina na isiyokuwa ya kiubabaishaji, tungependa kuchukua fursa hii kutoa angalizo juu ya mwenendo wa ujumla wa serikali katika kutekeleza maazimio ya Bunge, si wakati huu wa sasa tu hata huko tulikotoka wakati wa mfumo wa chama kimoja.

Aghalab serikali imejisikia vibaya inabosukumw a na Bunge kutekeleza maazimo ambayo ni ya kinidhamu zaidi kwa watumishi wake; hii ilipata kutokea mara nyingi, lakini iliyopo kwenye kumbukumbu za hivi karibuni ni utekelezwaji wa maazimio ya Richmond. Wapo watumishi wa serikali waliotajwa kwenye ripoti ile na wakaonekana kuwa walikuwa wamezembea na kwa maana hiyo walistahili kuadhibiwa kama azimio la Bunge lilivyoelekeza.

Kwa bahati mbaya, hatua hazikuchukuliwa kwa baadhi ya maofisa hao, na kilichokuja kugundulika baadaye ni mvutano katika kutekelezaji wa maazimio ya Bunge. Katika hali hiyo, waliokuwa wanadaiwa kuzembea na uzembe huo ukasaidia kwa njia moja au nyingine kufanikiwa kwa kilichoikumba Richmond, walilindwa mno na kile watawala walichosema ni taratibu za sheria na kanuni za kiutumishi serikalini.

Imetokea mara kadhaa watumishi wa umma kuonekana dhahiri kuwa wamefanya uzembe ambao umeligharimu taifa, lakini kwa kutumia kisingizio cha sheria na kanuni za utumishi serikalini, wameachwa huru bila kufanywa lolote, sana sana wamehamishwa vituo vya kazi.

Kuna mambo mengi yanatokea ndani ya mfumo wa serikali ambayo kwa hakika ni vigumu kujua wanaoyatenda wanakuwa wamejishikiza wapi. Ingwa ni vigumu kupata jibu moja juu ya ujasiri wa maamuzi na matendo ya baadhi ya watumishi wa umma

dhidi ya haki za wananchi kwa ujumla, hususan matumizi bora na sahihi ya kodi, sheria ya watumishi wa umma namba nane ya mwaka 2002 inatajwa kuwa moja ya vichaka vya watumishi kuwa na ujasiri huo.

Tungependa ieleweke wazi kwamba hatushauri watu kuonewa na kwa kweli si nia yetu hata siku moja kuchagiza ukiukaji wa sheria katika kuwaadhibu watu, hususan watumishi mabingwa wa kupindisha taratibu na sheria, lakini kwa kweli umekuwa ni wito wetu kuwa kila inapofaa ni vema taratibu, kanuni na sheria zetu zikauhuishwa ili zisaidie kutatua matatizo ya kiutawala na kiutendaji ambayo yamekuwa ni kikwazo kwa taifa hili kusonga mbele.

Tunasema haya kwa kuwa pamoja na ulazima wa kuwalinda watumishi wa umma wakati wa utekelezaji wa majukumu yao kisheria, lakini inapotokea sheria husika zimetengenezwa kwa nia ya kuwafanya wasiguswe, basi kuna tatizo. Itakumbukwa kuwa

ilipata kutokea mkurugenzi wa idara moja katika wizara ya serikali kumvimbia waziri wake hata pale mkuruhenzi huyo alipokuwa anafanya madudu katika ofisi yake; huyu alifanya hivyo kwa kuwa alijua kuwa analindwa na sheria na taratibu mbovu ambazo

kwa hakika hazisaidii sana taifa hili kuoandokana na vitendo viovu katika ofisi ya umma.
Tunakumbusha yote hata kwa kuwa tunajua serikali katika kushughulikia siala la Jairo itakuja na maelezo yaliyofungwa kwenye

sheria, kanuni na taratibu za watumishi wa umma, mara nyingi kuendeleza kile ambacho kimeshuhudiwa huko nyuma, yaani kuendeleza dhana ya kukwepa watumishi wa umma hasa wale vigogo kuadhibiwa na Bunge. Ni kwa hali hii tunatamani na kutaraji kuwa katika mkutano wa Bunge ujao serikali italeta taarifa yake yenye mashiko ili kujenga uwajibikaji katika ofisi za umma.

CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom